2 Wakorintho 11:16-33 NEN

2 Wakorintho 11:16-33

Paulo Anajivunia Mateso Yake

11:16 2Kor 11:1; 12:6, 11Nasema tena, mtu yeyote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata kama mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. 11:17 1Kor 7:12, 25; 2Kor 11:21; 1Kor 7:6Ninayosema kuhusiana na huku kujisifu kwa kujiamini, sisemi kama vile ambavyo Bwana angesema, bali kama mjinga. 11:18 2Kor 5:16; 10:4; Flp 3:3-4Kwa kuwa wengi wanajisifu kama vile ulimwengu ufanyavyo, mimi nami nitajisifu. 11:19 1Kor 4:10; 2Kor 11:1Ninyi mwachukuliana na wajinga kwa sababu mna hekima sana! 11:20 2Kor 11:1Kweli ni kwamba mnachukuliana na mtu akiwatia utumwani au akiwatumia kwa ajili ya kupata faida au akiwanyangʼanya au akijitukuza mwenyewe au akiwadanganya. 11:21 2Kor 10:1; Flp 3:4Kwa aibu inanipasa niseme kwamba sisi tulikuwa dhaifu sana kwa jambo hilo!

Lakini chochote ambacho mtu mwingine yeyote angethubutu kujisifia, nanena kama mjinga, nami nathubutu kujisifu juu ya hilo. 11:22 Flp 3:5; Rum 9:4; 11:1; Lk 3:8Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Je, wao ni Waisraeli? Mimi pia ni Mwisraeli. Je, wao ni wazao wa Abrahamu? Mimi pia ni mzao wa Abrahamu. 11:23 1Kor 3:5; 15:10; Mdo 16:23; 2Kor 6:4-5; Rum 8:36Je, wao ni watumishi wa Kristo? (Nanena kiwazimu.) Mimi ni zaidi yao. Nimefanya kazi kwa bidii kuwaliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, na nimekabiliwa na mauti mara nyingi. 11:24 Kum 25:3Mara tano nimechapwa na Wayahudi viboko arobaini kasoro kimoja. 11:25 Mdo 16:22; 14:19; 27:1-44Mara tatu nilichapwa kwa fimbo, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa, 11:26 Mdo 20:3; 21:31; Gal 2:4katika safari za mara kwa mara. Nimekabiliwa na hatari za kwenye mito, hatari za wanyangʼanyi, hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, hatari kutoka kwa watu wa Mataifa; hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini; na hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 11:27 Mdo 18:3; Kol 1:29; 1Kor 4:11-12; 2Kor 6:5Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi; ninajua kukaa njaa na kuona kiu; nimefunga kula chakula mara nyingi; nimehisi baridi na kuwa uchi. 11:28 1Kor 7:17Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa na mzigo wa wajibu wangu kwa makanisa yote. 11:29 Rum 14:1; 1Kor 2:3; Mt 5:29Je, ni nani aliye mdhaifu, nami nisijisikie mdhaifu? Je, nani aliyekwazwa, nami nisiudhike?

11:30 Gal 6:14; 2Kor 12:5-9; 1Kor 2:3Kama ni lazima nijisifu, basi nitajisifia yale mambo yanayoonyesha udhaifu wangu. 11:31 Rum 1:25; 9:5Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye anahimidiwa milele, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. 11:32 Mdo 9:24; 9:25Huko Dameski, mtawala aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliulinda mji wa Dameski ili kunikamata. Lakini nilishushwa kwa kapu kubwa kupitia katika dirisha ukutani, nikatoroka kutoka mikononi mwake.

Read More of 2 Wakorintho 11