2 Wakorintho 11:1-15 NEN

2 Wakorintho 11:1-15

Paulo Na Mitume Wa Uongo

11:1 Mt 17:17; 2Kor 5:13Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo. 11:2 Hos 2:19; Efe 5:26-27Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Kristo kama mabikira safi. 11:3 Mwa 3:1-6; 1Tim 2:14; Ufu 12:5Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo. 11:4 1Kor 3:11; Rum 8:15; Gal 1:6-9Kwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Yesu mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi. 11:5 2Kor 12:11; Gal 2:6Lakini sidhani ya kuwa mimi ni dhalili sana kuliko hao “mitume wakuu.” 11:6 1Kor 1:17; 2Kor 9:7; Efe 3:4Inawezekana mimi nikawa si mnenaji hodari, lakini ni hodari katika elimu. Jambo hili tumelifanya liwe dhahiri kwenu kwa njia zote.

11:7 2Kor 12:13; Rum 1:1; 1Kor 9:18Je, nilitenda dhambi kwa kujishusha ili kuwainua ninyi kwa kuwahubiria Injili ya Mungu pasipo malipo? 11:8 Flp 4:15-18Niliyanyangʼanya makanisa mengine kwa kupokea misaada kutoka kwao ili niweze kuwahudumia ninyi. 11:9 Flp 4:15; 2Kor 12:13-16Nami nilipokuwa pamoja nanyi, nikipungukiwa na chochote, sikuwa mzigo kwa mtu yeyote, kwa maana ndugu waliotoka Makedonia walinipatia mahitaji yangu. Kwa hiyo nilijizuia kuwa mzigo kwenu kwa njia yoyote, nami nitaendelea kujizuia. 11:10 Rum 9:1; Mdo 18:12; 1Kor 9:15Kwa hakika kama vile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu yeyote katika Akaya nzima atakayenizuia kujivunia jambo hili. 11:11 Rum 1:9; 2Kor 12:15Kwa nini? Je, ni kwa sababu siwapendi? Mungu anajua ya kuwa nawapenda! 11:12 2Kor 9:12Nami nitaendelea kufanya lile ninalofanya sasa ili nisiwape nafasi wale ambao wanatafuta nafasi ya kuhesabiwa kuwa sawa na sisi katika mambo wanayojisifia.

11:13 Mt 7:15; Tit 1:10; Ufu 2:2Watu kama hao ni mitume wa uongo, ni wafanyakazi wadanganyifu, wanaojigeuza waonekane kama mitume wa Kristo. 11:14 Mt 4:10Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. 11:15 Mt 16:27; Flp 3:19Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.

Read More of 2 Wakorintho 11