2 Wakorintho 1:1-11 NEN

2 Wakorintho 1:1-11

Salamu

1:1 1Kor 1:11; Efe 1:1; Kol 1:1; 2Tim 1:1; Mdo 16:1; 1Kor 10:32; Mdo 18:1; 18:12Barua hii ni kutoka kwangu mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,

Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko Akaya yote:

1:2 Rum 1:7; 1Kor 1:3; Gal 1:3; Flp 1:2; Kol 1:2; Flp 3:1; 1The 1:1Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.

Mungu Wa Faraja Yote

1:3 Efe 1:3; 1Pet 1:3; Rum 15:5Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. 1:4 Isa 49:13; 51:12; 66:13; 2Kor 7:6-13Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu. 1:5 Rum 8:17; 2Kor 4:10; Gal 6:17; Flp 3:10; Kol 1:24; 1Pet 4:13Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo. 1:6 2Kor 4:15; 4:17Kama tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata. 1:7 2Kor 1:5; Rum 8:17; 2Tim 2:12Nalo tumaini letu kwenu ni thabiti, kwa sababu tunajua kwamba kama vile mnavyoshiriki mateso yetu, ndivyo pia mnavyoshiriki katika faraja yetu.

1:8 Rum 11:25; 1Kor 15:32; Mdo 2:9Ndugu wapendwa, hatutaki mkose kujua kuhusu zile taabu tulizopata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo sana, kiasi cha kushindwa kuvumilia, hata tulikata tamaa ya kuishi. 1:9 Yer 17:5-7; Yn 5:21Kwa kweli, mioyoni mwetu tulihisi tumekabiliwa na hukumu ya kifo, ili tusijitegemee sisi wenyewe bali tumtegemee Mungu afufuaye wafu. 1:10 Rum 15:31; 1Tim 4:10Yeye aliyetuokoa kwenye hatari kubwa ya kifo na atatuokoa tena. Kwake yeye tumeweka tumaini letu kwamba ataendelea kutuokoa. 1:11 Rum 15:30; Flp 1:19; 2Kor 4:15; 9:11Kama vile mlivyoungana kusaidiana nasi katika maombi, hivyo wengi watatoa shukrani kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka za neema tulizopata kwa majibu ya maombi ya wengi.

Read More of 2 Wakorintho 1