2 Nyakati 5:2-14, 2 Nyakati 6:1-42, 2 Nyakati 7:1-10 NEN

2 Nyakati 5:2-14

Sanduku La Agano Laletwa Hekaluni

(1 Wafalme 8:1-9)

5:2 2Sam 6:12; 1Nya 15:25; 1Fal 8:1; 1Nya 29:1Kisha Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 5:3 2Nya 7:8-10; 1Fal 8:2Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba.

5:4 Yos 3:6Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano, 5:5 Hes 3:31; 1Nya 15:2nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo, naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.

5:7 Ufu 11:19Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Bwana hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. 5:8 Mwa 3:24Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea. 5:9 1Fal 8:8Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. 5:10 Ebr 9:4; Kum 10:2; Kut 16:34; 2Nya 6:11Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.

5:11 1Nya 24:1Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. 5:12 1Nya 15:16-24; 9:33Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta. 5:13 1Nya 16:34; Yer 33:11; Za 106:1; 2Nya 7:3; Za 136:1-6Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema:

“Yeye ni mwema;

upendo wake unadumu milele.”

Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu, 5:14 Kut 40:35; 19:16; 2Nya 7:2-3; Ufu 15:8; Hes 19:5; Isa 6:4; Eze 43:4; Hag 2:7; 2Kor 3:11nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu la Mungu.

Read More of 2 Nyakati 5

2 Nyakati 6:1-42

Kuweka Hekalu Wakfu

(1 Wafalme 8:12-21)

6:1 1Fal 8:12; Kut 19:9; Law 16:2; Ebr 12:18; Kut 20:21; 24:15-18; Za 18:8-11Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene. 6:2 Ezr 7:15; Za 135:21Nimejenga Hekalu zuri kwa ajili yako, mahali pako pa kukaa milele.”

Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. Kisha akasema:

“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mikono yake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, wala sikumchagua mtu yeyote kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli. 6:6 Za 78:68-70; Kum 12:5; Kut 20:24; 2Nya 12:13; 1Nya 28:4; 1Sam 16:1; Za 89:19-20Lakini sasa nimeuchagua Yerusalemu ili Jina langu lipate kuwamo humo, na nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’

6:7 2Sam 7:2; 1Nya 28:2; Mdo 7:46; 1Fal 7:3“Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 6:8 1Fal 8:18-21; 2Kor 8:12Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako. Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea Hekalu, bali mwanao, ambaye ni nyama yako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

Bwana ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile Bwana alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 6:11 Kut 40:20; 10:2; Za 50:5; 1Fal 8:9-21; 2Nya 5:10Nimeliweka humo Sanduku la Agano, ambamo ndani yake kuna lile Agano la Bwana alilofanya na watu wa Israeli.”

Maombi Ya Solomoni Ya Kuweka Wakfu

(1 Wafalme 8:22-53)

6:12 1Fal 8:22; Ebr 9:5; 1Tim 2:8Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana machoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akakunjua mikono yake. 6:13 Neh 8:4; Za 95:6Basi Solomoni alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kwelekea mbinguni. 6:14 Kut 15:11; 8:10; Mwa 5:24; Kum 7:9; Dan 9:4; 2Sam 7:22; Za 86:8Akasema:

“Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote. 6:15 1Nya 22:9-10Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umetimiza, kama ilivyo leo.

6:16 1Fal 2:4; 2Nya 7:18; Za 132:12; 2Sam 7:12-16; 1Fal 6:12“Sasa Bwana, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, kama wanao wakiangalia yote wayafanyayo kuenenda mbele zangu kama vile ulivyofanya.’ Sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, acha neno lako lile ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie.

6:18 Ufu 21:3; Isa 40:22; Mdo 7:49; Za 113:5-6; 2Nya 2:6“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga! Hata hivyo sikiliza dua ya mtumishi wako na maombi yake kwa huruma, Ee Bwana Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. 6:20 Dan 6:10; Kut 3:16; Kum 12:11; 2Nya 7:14; 30:20; Za 33:18; 34:15Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. 6:21 Isa 43:25; 55:7; Mik 7:18; Isa 44:22Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.

6:22 Kut 22:11“Mtu anapomkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili, 6:23 Isa 3:11; Rum 2:8; Mt 16:27basi, sikia kutoka mbinguni na ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimwadhibu yule mwenye hatia kwa kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie mwenye haki kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kuwa haki kwake.

6:24 Law 26:17; Kum 32:15; Amu 2:11-15; Za 51:4“Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili, basi usikie kutoka mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao.

6:26 2Sam 1:21; Lk 4:25; 1Fal 17:1; Law 26:10“Wakati mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka dhambi zao kwa sababu umewaadhibu, 6:27 2Nya 7:14; Yn 6:45; Zek 10:1; 1Fal 8:35, 36; Za 94:12basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.

6:28 2Nya 20:9“Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia, wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu zake na uchungu wake, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili, 6:30 1Sam 2:3; 1Nya 28:9; Za 11:4basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), 6:31 Kum 6:13; Za 34:7-9ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.

6:32 2Nya 9:6; Kum 4:6-8; Yn 12:20; Mdo 8:27; Kut 3:19-20; Kum 4:6-8; Za 113:3; Isa 56:3-8; Yn 10:16“Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyooshwa, atakapokuja kuomba kuelekea Hekalu hili, 6:33 Kut 12:43; 2Nya 7:14basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.

6:34 Kum 28:7; 1Nya 5:20“Wakati watu wako watakapokwenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa Bwana kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, basi usikie dua na maombi yao kutoka mbinguni, ukawatetee haki yao.

6:36 1Fal 8:46; Law 26:44; Rum 3:9; Ay 15:14-16; Mit 20:9; Mhu 7:20; Yak 3:2“Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu yeyote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi iliyo mbali au karibu 6:37 1Fal 8:48; Isa 58:3; Yer 24:6-7na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya utumwa na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa na tumetenda uovu’; 6:38 Yer 29:12-13kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na kuitetea haki yao. Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako.

6:40 Za 130:2; Isa 37:17“Sasa, Mungu wangu, macho yako na yafumbuke na masikio yako yasikie maombi yaombwayo mahali hapa.

6:41 Isa 33:10; Neh 9:25; Isa 51:10; Za 132:16; 1Nya 28:2“Sasa inuka, Ee Bwana Mungu,

na uje mahali pako pa kupumzikia,

wewe na Sanduku la nguvu zako.

Makuhani wako, Ee Bwana Mungu,

na wavikwe wokovu,

watakatifu wako na wafurahi

katika wema wako.

6:42 Za 89:24-28; Isa 55:3Ee Bwana Mungu, usimkatae

mpakwa mafuta wako.

Kumbuka upendo mkuu uliomwahidia

Daudi mtumishi wako.”

Read More of 2 Nyakati 6

2 Nyakati 7:1-10

Hekalu Lawekwa Wakfu

(1 Wafalme 8:62-66)

7:1 Kut 19:18; Mwa 15:17; Law 9:24; Kut 16:10; Dan 9:20; 1Fal 8:54; Isa 65:24; Mdo 4:31; Amu 6:21; 1Fal 18:38; 1Nya 21:26; 2Nya 5:13; Eze 10:3; Ufu 21:23Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Bwana ukalijaza Hekalu. 7:2 2Nya 5:14; Kut 29:43; 1Fal 8:11Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Bwana kwa sababu utukufu wa Bwana ulilijaza. 7:3 1Nya 16:34; Ezr 3:11; 2Nya 5:13; 20:13; 20:21; Za 103:17Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Bwana ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru Bwana wakisema,

“Yeye ni mwema;

upendo wake unadumu milele.”

7:4 1Fal 8:62Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana Mungu. Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ngʼombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu. 7:6 1Nya 15:16-24; 2Nya 5:12Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Bwana ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Bwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.

7:7 Hes 16:37; 2Nya 36:14; Ebr 13:10-12; 1Fal 8:64Solomoni akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Bwana na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka na za mafuta.

7:8 2Nya 30:26; Mwa 15:18; Neh 8:17; Yos 13:3Hivyo Solomoni akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. 7:9 Law 23:36Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi. Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Solomoni akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Bwana Mungu aliomtendea Daudi na Solomoni na kwa ajili ya watu wake Israeli.

Read More of 2 Nyakati 7