2 Nyakati 13:1-22, 2 Nyakati 14:1-15, 2 Nyakati 15:1-19 NEN

2 Nyakati 13:1-22

Abiya Mfalme Wa Yuda

(1 Wafalme 15:1-8)

Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 13:2 2Nya 11:20; 1Fal 15:6naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka, binti Urieli wa Gibea.

Basi kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo.

13:4 Yos 18:22; 1Nya 11:1Abiya akasimama juu ya Mlima Semaraimu, katika nchi ya vilima ya Efraimu, naye akasema, “Yeroboamu na Israeli yote, nisikilizeni mimi! 13:5 2Sam 7:13; 1Nya 17:12; Law 2:13; Hes 18:19; Amu 11:21-24; Eze 43:24; 1Sam 16:13; Za 89:20; Lk 1:31-33Hamfahamu kwamba Bwana, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi na wazao wake ufalme juu ya Israeli milele kwa Agano la chumvi? 13:6 1Fal 11:26; 12:20; 2Nya 10:19Hata hivyo Yeroboamu mwana wa Nebati afisa wa Solomoni mwana wa Daudi, aliasi dhidi ya bwana wake. 13:7 Amu 9:4; Za 26:4; Mdo 17:5; Mit 12:11Baadhi ya watu wasiofaa kitu, wabaya kabisa walimkusanyikia na kumpinga Rehoboamu mwana wa Solomoni alipokuwa kijana mdogo asiyekuwa na uamuzi, asiye na nguvu za kuweza kupingana nao.

13:8 Za 68:25; 1Nya 25:10-24; 2Nya 29:2513:8 Kut 32:4; 1Fal 12:28; Hos 8:6“Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa Bwana ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu. 13:9 2Nya 11:14-15; Kut 29:35-36; Gal 4:8; Yer 2:11Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa Bwana, wana wa Aroni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.

“Lakini kwetu sisi, Bwana ndiye Mungu wetu, wala hatujamwacha. Makuhani wanaomtumikia Bwana ni wana wa Aroni, nao Walawi wakiwasaidia. 13:11 Kut 29:39; 2Nya 2:4; Law 24:2-6; 1Nya 9:24; Kut 27:20-21Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa Bwana. Wao huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za Bwana Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu. 13:12 Hes 10:8-9; Amu 2:15; Mdo 5:39; Kum 20:4; Yos 5:4; Za 20:7; Ay 15:25-26; Mdo 9:4-5Mungu yu pamoja nasi, yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya Bwana, Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”

13:13 2Nya 20:22; Yos 8:9Basi Yeroboamu alikuwa ametuma jeshi kuzunguka nyuma ya Yuda ili kwamba akiwa mbele ya Yuda, jeshi liwavizie kwa nyuma. 13:14 1Nya 5:20; 2Nya 18:31Basi Yuda wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa mbele na nyuma. Ndipo wakamlilia Bwana. Makuhani wakapiga tarumbeta zao, 13:15 2Nya 14:12; Hes 32:4nao watu wa Yuda wakapaza sauti ya kilio cha vita. Katika kupiga kelele za vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda. 13:16 2Nya 16:8Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia Israeli mikononi mwao. Abiya na watu wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi 500,000 miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli. 13:18 1Nya 5:20; Za 22:5; Amu 8:28; 2Fal 18:5; 2Nya 16:8-9; 20:20Watu wa Israeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea Bwana, Mungu wa baba zao.

13:19 Yos 15:9; Yn 11:54Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vinavyoizunguka miji hiyo. 13:20 1Sam 25:38; Eze 24:16; Mdo 12:23; 1Sam 26:10; 1Fal 14:20Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. Naye Bwana akampiga Yeroboamu akafa.

Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.

13:22 2Nya 9:29; 12:15Matukio mengine ya utawala wa Abiya, pamoja na mambo aliyofanya na aliyosema, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.

Read More of 2 Nyakati 13

2 Nyakati 14:1-15

Asa Atawala

14:1 1Fal 15:8Naye Abiya akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake. Katika siku zake, nchi ikawa na amani kwa miaka kumi.

Asa akatenda yaliyo mema na haki machoni pa Bwana Mungu wake. 14:3 Kum 7:5; 1Fal 15:12-14; Kut 34:13; 2Nya 15:17; 1Fal 11:7Akaziondoa madhabahu za kigeni na mahali pa juu pa kuabudia miungu, akayavunja yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Maashera. Akawaamuru Yuda kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao na kutii sheria zake na amri zake. 14:5 Isa 27:9; Eze 6:4Akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu za kufukizia uvumba kwenye kila mji katika Yuda, nao ufalme ulikuwa na amani katika utawala wake. 14:6 1Nya 22:9; 2Nya 15:15Akajenga miji yenye ngome katika Yuda, wakati nchi ikiwa na amani. Hakuna mtu yeyote aliyepigana vita naye katika miaka hiyo, kwa kuwa Bwana alimstarehesha.

Mfalme akawaambia Yuda, “Tuijenge hii miji na tuizungushie kuta, pamoja na minara, malango na makomeo. Nchi bado ni yetu, kwa sababu tumemtafuta Bwana Mungu wetu, tulimtafuta naye ametupa raha kila upande.” Hivyo wakajenga na wakafanikiwa.

Asa alikuwa na jeshi la watu 300,000 kutoka Yuda, wenye ngao kubwa na mikuki na jeshi la watu 280,000 kutoka Benyamini, wenye ngao ndogo na pinde. Watu hawa wote walikuwa wapiganaji mashujaa.

14:9 2Nya 16:8; 12:3; Yos 15:44; Mwa 10:8-9; Mik 1:15Zera Mkushi akatoka kupigana dhidi yao akiwa na jeshi la watu maelfu ya maelfu na magari ya vita 300, nao wakaja mpaka Maresha. Asa akatoka kumkabili, nao wakapanga vita katika Bonde la Sefatha karibu na Maresha.

14:11 1Fal 8:44, 45; 2Nya 25:8; 13:18; Kut 14:10; 1Sam 14:6; 17:45; 1Nya 5:20; Za 22:5; Mdo 2:21; Amu 7:7; 2Kor 12:9-10; Mit 18:10; Nah 1:7Kisha Asa akamlilia Bwana Mungu wake na kusema, “Ee Bwana, hakuna yeyote aliye kama wewe wa kuwasaidia wasio na nguvu dhidi ya wenye nguvu. Utusaidie, Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, kwa kuwa tunakutumainia wewe, nasi kwa jina lako tumekuja dhidi ya jeshi hili kubwa. Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, usiwaache wanadamu wakushinde wewe.”

14:12 2Nya 13:15Bwana akawapiga Wakushi mbele ya Asa na Yuda. Wakushi wakakimbia, 14:13 Mwa 10:19; Za 46:1-11naye Asa na jeshi lake wakawafuatia mpaka Gerari. Idadi kubwa ya Wakushi ilianguka hata wasiweze kuinuka tena, wakapondapondwa mbele za Bwana na majeshi yake. 14:14 Mwa 35:5; Kum 2:25; 11:25; Kut 15:16; 2Nya 17:10; 20:29Watu wa Yuda wakachukua nyara nyingi sana, wakaangamiza vijiji vyote vinavyoizunguka Gerari, kwa kuwa hofu ya Bwana ilikuwa imewaangukia. Wakateka nyara vijiji hivi vyote, kwani kulikuwepo nyara nyingi huko. Pia wakashambulia kambi za wachunga makundi ya wanyama wakachukua na kuyaswaga makundi ya kondoo, mbuzi na ngamia. Kisha wakarudi Yerusalemu.

Read More of 2 Nyakati 14

2 Nyakati 15:1-19

Asa Afanya Matengenezo

15:1 Hes 24:4; Amu 3:10; 2Nya 24:20; 2Sam 23:2; 2Nya 20:14; 2Pet 1:21Roho wa Bwana akamjia Azaria mwana wa Odedi. 15:2 Yak 4:8; 2Nya 20:17; Kum 31:17; 1Nya 28:9; Ebr 12:25; 2Nya 33:12-13; Yer 29:13; Mt 7:7; 2Nya 12:1-3; Rum 11:1-2Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Bwana yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi. 15:3 Law 10:11; Mao 2:9; Amo 8:11; Hos 3:4Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria. 15:4 Kum 4:29Lakini katika taabu yao walimrudia Bwana, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao. 15:5 Amu 19:20; Zek 8:10; Amu 5:6Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa. 15:6 Mt 24:7; Isa 19:2; Mk 13:8Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina. 15:7 1Sam 24:19; Mit 14:14; Rut 2:12; Za 58:11; Mt 5:12-46; Lk 6:35; Kol 3:24Lakini kwa habari yenu ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.”

15:8 2Nya 13:19; 8:12; 1Fal 8:64Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Bwana.

15:9 2Nya 11:16-17Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye.

Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. 15:11 2Nya 14:13-15Wakati huo wakamtolea Bwana dhabihu za ngʼombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka zile nyara walizoteka. 15:12 2Fal 11:17; 2Nya 23:16; Neh 10:29; 1Nya 16:11; 2Fal 23:3; 2Nya 34:31Wakafanya agano kumtafuta Bwana, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. 15:13 Kut 22:20; Kum 13:9-16Wale wote ambao hawangemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. Wakamwapia Bwana kwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu. 15:15 Kum 4:29; 1Nya 22:9; 2Nya 14:7Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Bwana akawastarehesha pande zote.

15:16 Kut 34:13; 2Nya 14:2-5; 1Fal 15:2, 10Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. 15:17 2Fal 12:3; 1Fal 3:2-4; Kum 12:7; 1Fal 15:14; 2Nya 14:3-5Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Bwana kikamilifu maisha yake yote. Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.

Read More of 2 Nyakati 15