2 Nyakati 10:1-19, 2 Nyakati 11:1-23, 2 Nyakati 12:1-16 NEN

2 Nyakati 10:1-19

Israeli Wanamwasi Rehoboamu

(1 Wafalme 12:1-20)

10:1 1Fal 12:11Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wamekwenda huko kumfanya yeye kuwa mfalme. 10:2 1Fal 11:40; 2Nya 9:29Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Solomoni), akarudi kutoka Misri. Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu, yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea Rehoboamu na kumwambia, 10:4 2Nya 2:2; 1Sam 8:11-18; Mt 23:4; 1Fal 4:7; 5:15; 9:15; Mt 11:29-30; 1Yn 5:3“Baba yako aliweka nira nzito, lakini sasa tupunguzie kazi za kikatili na nira nzito aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.”

Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao.

10:6 Ay 12:12; 32:7; 8:8-9Kisha Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee ambao walimtumikia Solomoni baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri nini katika kuwajibu watu hawa?”

10:7 Mit 15:1; Neh 5:19; 1Fal 12:7; Za 112:5Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.”

10:8 2Sam 17:14; Mit 13:20; 2Nya 25:16; Mit 1:25; Mhu 10:2Lakini Rehoboamu akakataa shauri alilopewa na wazee na akataka ushauri kwa vijana wanaume rika lake waliokuwa wakimtumikia. Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu?’ ”

Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Waambie watu hawa waliokuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi,’ kuwa, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi; mimi nitawachapa kwa nge.’ ”

Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.” 10:13 Mit 12:13; 14:16Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee, akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.” 10:15 Mwa 50:20; 2Nya 25:16-20; 11:4; 1Fal 11:29; Amo 3:6; 1Sam 2:25; 1Fal 12:15, 24Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwa Mungu ili kutimiza neno ambalo Bwana alikuwa amenena kwa Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia Ahiya Mshiloni.

10:16 1Nya 9:1; 2Sam 20:1Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme:

“Tuna fungu gani kwa Daudi?

Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese.

Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli,

angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!”

Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao. Lakini kwa habari ya Waisraeli waliokuwa wakiishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado.

10:18 2Sam 20:24; 1Fal 5:14Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu10:18 Kiebrania ni Hadoramu. aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu. 10:19 1Fal 12:19; 2Fal 17:21-23; 2Nya 13:5-7; Mhu 2:9Hivyo Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo.

Read More of 2 Nyakati 10

2 Nyakati 11:1-23

Utabiri Wa Shamaya

(1 Wafalme 12:21-24)

11:1 1Fal 12:21Ikawa Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na ya Benyamini, wanaume wapiganaji 180,000, kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli na kuurudisha tena ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Solomoni.

11:2 1Sam 2:27; 1Fal 12:22-24; 2Nya 12:15; Kum 33:1; 2Nya 8:14; 1Tim 6:11Lakini neno hili la Bwana likamjia Shemaya mtu wa Mungu: “Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni mfalme wa Yuda, na Israeli wote walioko Yuda na Benyamini, 11:4 2Nya 28:8-11; 28:8-11‘Hili ndilo asemalo Bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Bwana na wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu.

Yeroboamu Ajengea Yuda Ngome

Rehoboamu akaishi Yerusalemu akajenga miji yenye ngome katika Yuda: 11:6 Mwa 35:19; Amu 15:8; 1Sam 17:12; 2Nya 20:20; 2Sam 14:2; Neh 3:5; Yer 3:5; 6:1; Amo 1:1Akajenga Bethlehemu, Etamu, Tekoa, Beth-Suri, Soko, Adulamu, Gathi, Maresha, Zifu, Adoraimu, Lakishi, Azeka, Sora, Aiyaloni na Hebroni. Hii ndiyo iliyokuwa miji iliyojengewa ngome katika Yuda na Benyamini. Akaimarisha ulinzi wake na kuweka majemadari ndani yake, pamoja na ghala za mahitaji ya vyakula, mafuta ya zeituni na divai. Akaweka ngao na mikuki katika miji na kuifanya iwe imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake.

Makuhani na Walawi kutoka sehemu zote za Israeli wakawa upande wake. 11:14 Hes 35:2-5; 1Nya 6:81; 2Nya 13:9; 1Fal 12:28-33Pia Walawi wakaacha maeneo yao ya malisho na mali zao, wakaja Yuda na Yerusalemu kwa sababu Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewakataa wasiwe makuhani wa Bwana. 11:15 1Fal 12:28-31; 13:33; Law 17:7; 2Nya 13:8; Kum 32:15-17; Hos 13:2; 1Kor 10:20; Ufu 16:14; 1Fal 12:28Naye akawa amechagua makuhani wake mwenyewe kwa ajili ya mahali pa juu pa kuabudia sanamu za mbuzi na za ndama ambazo alikuwa ametengeneza. 11:16 2Nya 15:9; Za 69:32; 2Nya 30:11Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Bwana dhabihu, Mungu wa baba zao. 11:17 2Nya 12:1; Mt 13:18; Hos 6:4Wakaimarisha ufalme wa Yuda na kumuunga mkono Rehoboamu mwana wa Solomoni miaka mitatu, wakienenda katika njia za Daudi na Solomoni katika wakati huu.

Jamaa Ya Rehoboamu

Rehoboamu alimwoa Mahalati ambaye alikuwa binti Yeremothi mwana wa Daudi, mamaye alikuwa Abihaili binti Eliabu mwana wa Yese. 11:19 1Fal 15:2Mahalati alimzalia Rehoboamu wana: Yeushi, Shemaria na Zahamu. 11:20 1Fal 15:2; 2Nya 12:16Kisha akamwoa Maaka binti Absalomu, ambaye alimzalia: Abiya, Atai, Ziza na Shelomithi. 11:21 Kum 15:17Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu zaidi kuliko wakeze wengine na masuria wake. Kwa jumla alikuwa na wake kumi na wanane na masuria sitini, wana ishirini na wanane na binti sitini.

11:22 Kum 21:15-17Rehoboamu akamweka Abiya mwana wa Maaka, kuwa mkuu wa wana wa mfalme miongoni mwa ndugu zake ili amfanye mfalme. 11:23 Kum 17:17; 1Fal 11:3Akatenda kwa busara, akiwasambaza baadhi ya wanawe katika wilaya zote za Yuda na Benyamini, pamoja na miji yote yenye ngome. Akawapa mahitaji tele na kuwaoza wake wengi.

Read More of 2 Nyakati 11

2 Nyakati 12:1-16

Shishaki Ashambulia Yerusalemu

(1 Wafalme 14:25-28)

12:1 2Nya 11:17; Kum 8:14; 1Fal 14:22-24Baada ya nafasi ya Rehoboamu kuimarika na kuwa na nguvu, yeye na Israeli yote waliiacha sheria ya Bwana Mungu. 12:2 1Nya 5:25; 1Fal 11:40; 14:24-25Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa Bwana, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu. 12:3 Mwa 10:6; Amo 9:7; 2Nya 16:8Akiwa na magari ya vita 1,200 na wapanda farasi 60,000 na idadi isiyohesabika ya majeshi ya Walibia, Wasukii na Wakushi12:3 Yaani watu kutoka sehemu ya Naili ya juu. yaliyokuja pamoja naye kutoka Misri. 12:4 2Nya 11:10Akateka miji ya Yuda yenye ngome akaendelea mpaka Yerusalemu.

12:5 2Nya 11:1; Kum 28:15; 2Nya 15:1-2Ndipo nabii Shemaya akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda waliokuwa wamekusanyika huko Yerusalemu kwa ajili ya hofu ya Shishaki naye akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, ‘Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo, mimi nami sasa ninawaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.’ ”

12:6 Law 26:40-42; Ezr 9:15; Yak 4:10; Kut 9:27; 10:3; 2Nya 33:12; 34:27; Za 78:34Viongozi wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Bwana Mungu ni mwenye haki.”

12:7 1Fal 21:29; Za 78:38Bwana Mungu alipoona kwamba wamejinyenyekeza, neno hili la Bwana likamjia Shemaya: “Maadamu wamejinyenyekeza, sitawaangamiza bali hivi karibuni nitawapatia wokovu. Ghadhabu yangu haitamwagwa juu ya Yerusalemu kwa kupitia Shishaki. 12:8 Kum 28:48; Isa 26:13Hata hivyo, watamtumikia Shishaki ili wapate kujifunza tofauti kati ya kunitumikia mimi na kuwatumikia wafalme wa nchi nyingine.”

12:9 2Nya 9:16; 1Fal 14:25Shishaki mfalme wa Misri alipoishambulia Yerusalemu, alichukua hazina za Hekalu la Bwana na hazina za jumba la kifalme. Akachukua kila kitu, pamoja na zile ngao za dhahabu ambazo Solomoni alikuwa amezitengeneza. 12:10 2Sam 8:18; 23:23; 1Nya 11:25Kwa hiyo Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba badala ya zile za dhahabu na kuzikabidhi kwa majemadari wa ulinzi wa zamu kwenye ingilio la jumba la mfalme. Kila wakati mfalme alipokwenda katika Hekalu la Bwana walinzi walikwenda pamoja naye wakiwa wamebeba hizo ngao na baadaye walizirudisha kwenye chumba cha ulinzi.

12:12 1Fal 14:13; 2Nya 19:3; Mwa 18:24Kwa sababu Rehoboamu alijinyenyekeza, hasira ya Bwana ikageukia mbali naye, hakuangamizwa kabisa. Kukawa na hali nzuri katika Yuda.

12:13 2Nya 6:6; 13:7; Kum 12:5; 1Fal 14:21; Za 48:1-3Mfalme Rehoboamu akajiweka imara katika Yerusalemu na akaendelea kuwa mfalme. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na saba, mji ambao Bwana alikuwa ameuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli ili aliweke Jina lake humo. Mama yake aliitwa Naama, alikuwa Mwamoni. 12:14 Mt 7:7; Mdo 9:11Rehoboamu akatenda maovu kwa sababu hakuuelekeza moyo wake katika kumtafuta Bwana Mungu.

12:15 2Nya 9:29; 13:22Kwa habari ya matukio katika utawala wa Rehoboamu, tangu mwanzo mpaka mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Shemaya na mwonaji Ido zinazohusiana na vizazi? Kulikuwako na vita mara kwa mara kati ya Rehoboamu na Yeroboamu. 12:16 2Nya 11:20Rehoboamu akalala na baba zake, akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Abiya mwanawe akawa mfalme baada yake.

Read More of 2 Nyakati 12