1 Wathesalonike 1:1-10, 1 Wathesalonike 2:1-16 NEN

1 Wathesalonike 1:1-10

Salamu

1:1 Mdo 16:1; 17:1; Rum 1:7Paulo, Silvano1:1 Yaani Sila. na Timotheo:

Kwa kanisa la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu na ndani ya Bwana Yesu Kristo:

Neema iwe kwenu na amani.

Shukrani Kwa Ajili Ya Imani Ya Wathesalonike

1:2 Rum 1:8; 2The 1:11; Efe 1:16; Flm 4Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima. 1:3 2The 1:11; 1The 2:13; Yn 6:29; Gal 5:6; 1The 3:6; Yak 2:17; Rum 16:6Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Yesu Kristo.

1:4 Kol 3:12; 2The 2:13Ndugu zetu mpendwao na Mungu, kwa kuwa tunajua kwamba Mungu amewachagua, 1:5 2The 2:14; Mk 16:20; 1Kor 6:6; Kol 2:2kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu. 1:6 1Kor 4:16; Mdo 17:5-10; 13:52Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu. 1:7 1The 4:10; Flp 3:7; 1Pet 5:3; 1Tim 4:12Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya. 1:8 Rum 1:8; 10:18Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lolote kwa habari yake. 1:9 1Kor 12:2; Gal 4:8Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli 1:10 Mdo 2:24; Rum 5:9na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Yesu, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.

Read More of 1 Wathesalonike 1

1 Wathesalonike 2:1-16

Huduma Ya Paulo Huko Thesalonike

2:1 1The 1:5-9Ndugu zangu, kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ya kwamba kuja kwetu kwenu hakukuwa bure, 2:2 Mdo 16:22; Flp 1:30kama vile mjuavyo, tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu wetu, tulikuwa na ujasiri wa kuwaambia Injili ya Mungu ingawa kulikuwa na upinzani mkubwa. 2:3 2Kor 2:17Kwa maana himizo letu halikutokana na hila wala nia mbaya au udanganyifu. 2:4 Gal 2:7; 1:10Kinyume chake, tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu, yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya mioyo yetu. 2:5 Mdo 20:33; Rum 1:9Kama mjuavyo, hatukuja kwenu kwa maneno ya kujipendekeza au maneno yasiyo ya kweli ili kuficha tamaa mbaya: Mungu ndiye shahidi yetu. 2:6 1Kor 9:1-2Wala hatukuwa tunatafuta sifa kutoka kwa wanadamu, wala kutoka kwenu au kwa mtu mwingine awaye yote.

Kama mitume wa Kristo tungaliweza kuwa mzigo kwenu, 2:7 1The 2:11; 1Kor 2:3; 9:22; 2Kor 1:4; 7:6, 7lakini tulikuwa wapole katikati yenu, kama mama anayewatunza watoto wake wadogo. 2:8 2Kor 12:15; 1Yn 3:16Tuliwapenda sana kiasi kwamba tulifurahia kushirikiana nanyi, si Injili ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa sababu mlikuwa wa thamani mno kwetu. 2:9 Mdo 18:3; 2Kor 11:9; 2The 3:8Ndugu zetu, mnakumbuka juhudi yetu na taabu yetu. Tulifanya kazi usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote wa kwenu wakati tulipokuwa tunawahubiria Injili ya Mungu.

2:10 2Kor 1:12Ninyi wenyewe ni mashahidi na Mungu pia, jinsi tulivyokuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama miongoni mwenu ninyi mlioamini. 2:11 1Kor 4:14Maana mnajua kwamba tuliwatendea kila mmoja wenu kama vile baba awatendeavyo watoto wake. 2:12 Efe 4:1Tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwahimiza kuishi maisha yampendezayo Mungu, anayewaita katika Ufalme na utukufu wake.

2:13 Ebr 4:12Nasi pia tunamshukuru Mungu bila kukoma kwa sababu mlipolipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu, bali mlilipokea kama lilivyo hasa, neno la Mungu, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. 2:14 Gal 1:22; Mdo 17:5; 2The 1:4Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlifanyika wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyoko ndani ya Kristo Yesu katika Uyahudi. Mlipata mateso yale yale kutoka kwa watu wenu wenyewe kama vile makanisa hayo yalivyoteswa na Wayahudi, 2:15 Mdo 2:23; Mt 5:12wale waliomuua Bwana Yesu na manabii, nasi wakatufukuza pia. Watu hao walimchukiza Mungu na tena ni adui wa watu wote, 2:16 Mdo 13:45-50; Mt 23:32wakijitahidi kutuzuia tusizungumze na watu wa Mataifa ili kwamba wapate kuokolewa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao hadi kikomo. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia.

Read More of 1 Wathesalonike 2