1 Samweli 8:1-22, 1 Samweli 9:1-27, 1 Samweli 10:1-8 NEN

1 Samweli 8:1-22

Israeli Waomba Mfalme

8:1 Kum 16:18-19; Amu 10:4; 12:14Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. 8:2 1Nya 6:28; Mwa 22; 19; 1Fal 19:3; Amo 5:4-5Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba. 8:3 1Sam 2:12; Neh 9:29; Ay 34:27; Za 14:3; 58:3; Isa 53:6; Kut 23:8; 1Sam 12:3; Mit 17:23; Kut 23:2; Kum 16:19Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.

8:4 Amu 11:11; 1Sam 11:3; 7:17Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. 8:5 Kum 17:14-20; 1Sam 10:19; 12:12-13; 3:20; 12:2; Hos 13:11Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuteulie mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.”

8:6 Hos 13:10; 1Sam 12:17; 15:11; 16:1Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,” hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba Bwana. 8:7 1Sam 12:1; Hes 11:20; Kut 16:8; Mt 10:24-25; Lk 10:16; Yn 13:16; 1Sam 10:19Naye Bwana akamwambia: “Sikiliza yale yote watu wanakuambia. Si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao. 8:8 1Sam 12:10; 2Fal 21:22; Yer 2:17Kama vile walivyofanya tangu siku nilipowapandisha kutoka Misri mpaka siku hii ya leo; wakiniacha mimi na kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokufanyia wewe. 8:9 Kum 17:14-20; 1Sam 8:11-18; 10:25Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.”

8:10 Kut 19:7Samweli akawaambia wale watu waliokuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya Bwana. 8:11 1Sam 10:25; 14:52; Mwa 41:46; Kum 17:16; 2Sam 15:1; 2Nya 1:14; 9:25; Wim 3:7; 1Nya 1:5Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake. 8:12 Kum 1:15; 1Sam 22:7Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake. Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji. 8:14 1Sam 28:6; Ay 27:9; 35:12-13; Za 18:41; 66:18; Mit 1:28; Isa 58:4; 59:2; Yer 14:12; Eze 8:18; Mik 3:4; 1Sam 10:25; 1Fal 12:4Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake. 8:15 Mwa 41:34; 1Sam 17:25Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake. Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike, na ngʼombe wenu walio wazuri sana na punda kwa matumizi yake mwenyewe. Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi, na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake. 8:18 1Sam 28:6; Ay 27:9; 35:12-13; Za 18:41; 66:18; Mit 1:28; Isa 58:4; 59:2; Yer 14:12; Eze 8:18; Mik 3:4; 1Sam 10:25; 1Fal 12:4Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye Bwana hatawajibu.”

8:19 Mit 1:24; Isa 50:2; 66:4; Yer 7:13; 8; 12; 13; 10; 44:16; Mdo 13:21Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.”

8:21 Amu 11:11Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za Bwana. 8:22 Hos 13:11Bwana akamjibu, “Wasikilize na uwape mfalme.”

Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, “Kila mmoja arudi mjini kwake.”

Read More of 1 Samweli 8

1 Samweli 9:1-27

Samweli Anamtia Sauli Mafuta

9:1 Yos 18:11-20; Rut 2:1; 1Sam 14:51; 1Nya 8:33; 9:39; Es 2:5; Mdo 13:21Kulikuwako Mbenyamini mmoja, mtu maarufu, ambaye aliitwa Kishi mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia wa Benyamini. 9:2 Mwa 39:6; 1Sam 10:23-24Alikuwa na mwana aliyeitwa Sauli, kijana anayevutia sana, hakuwepo aliyelingana naye miongoni mwa Waisraeli, alikuwa mrefu kuliko wengine wote.

9:3 1Sam 10:14-16Basi punda wa Kishi baba yake Sauli walipotea, naye Kishi akamwambia mwanawe Sauli, “Mchukue mmoja wa watumishi mwende pamoja naye kuwatafuta punda.” 9:4 Yos 24:33; 2Fal 4:42; 1Sam 10:2Hivyo akapita katika nchi ya vilima ya Efraimu na katika eneo la Shalisha, lakini hawakuwapata. Wakaendelea katika sehemu ya Shaalimu, lakini punda hawakuwepo huko. Kisha wakapita katika nchi ya Benyamini, lakini hawakuwapata.

9:5 1Sam 1:1; 10:1Walipofika sehemu ya Sufu, Sauli akamwambia mtumishi aliyekuwa pamoja naye, “Njoo, sisi na turudi, au baba yangu ataacha kufikiria juu ya punda na kuanza kufadhaika kutuhusu sisi.”

9:6 Kum 33:1; Amu 13:6; 1Sam 3:19; 1Fal 13:1; 2Fal 6:6; 1Tim 6:11; 1Sam 3:19; Isa 44:26; Mt 24:35Lakini mtumishi akajibu, “Tazama, katika mji huu yupo mtu wa Mungu, anayeheshimiwa sana na kila kitu asemacho hutokea kweli. Sasa na twende huko. Huenda atatuambia twende njia ipi.”

9:7 Mwa 32:20; 1Fal 13:7; 14:3; 2Fal 4:42; 5:5, 15; Yer 40:5; Amu 6:18; 13:17Sauli akamwambia mtumishi wake, “Kama tukienda, tutampa nini huyo mtu? Chakula kimekwisha kwenye mifuko yetu. Hatuna zawadi ya kumpelekea huyo mtu wa Mungu. Je tuna nini?”

Mtumishi akamjibu Sauli tena, akasema, “Tazama, nina fedha robo shekeli.9:8 Robo shekeli ni sawa na gramu 3. Hiyo nitampa huyo mtu wa Mungu ili aweze kutuambia twende kwa njia ipi.” 9:9 Mwa 25:22; 2Sam 15:27; 24:11; 17:13; 1Nya 9:22; 21:9; 26:28; 29:29; 2Nya 19:2; Isa 29:10; 30:10; Amo 7:12; Kut 28:30; Hes 27:21; Amu 1:1; 20:18-28; 2Sam 24:11; 2Fal 17:13(Zamani katika Israeli, kama mtu alikwenda kuuliza neno kwa Mungu, angalisema, “Njoo na twende kwa mwonaji,” kwa sababu nabii wa sasa alikuwa akiitwa mwonaji.)

Sauli akamwambia mtumishi wake, “Vyema, njoo na twende.” Basi wakaenda mjini alipokuwepo huyo mtu wa Mungu.

9:11 Mwa 24:11-13; Kut 2:16Walipokuwa wakipanda mlima kwenda mjini, wakakutana na baadhi ya wasichana wanakuja kuchota maji, nao wakawauliza, “Je, mwonaji yuko?”

9:12 Hes 28:11-15; 1Sam 7:17; Law 26:30; 1Fal 3:2Wakajibu, “Yuko, yu mbele yenu amewatangulia, sasa fanyeni haraka, ndiyo tu amekuja mjini kwetu leo, kwa kuwa watu wana dhabihu huko mahali pa juu. 9:13 Mt 14:19; 1Kor 10:16; 1Tim 4:3-5Mara tu mwingiapo mjini, mtamkuta kabla hajapanda kwenda mahali pa juu kula. Watu hawataanza kula mpaka atakapofika kwa sababu ni lazima kwanza yeye abariki dhabihu, ndipo wale walioalikwa watakapokula. Pandeni sasa, mtamkuta kwa wakati huu.”

Wakapanda mjini, nao walipokuwa wakiingia mjini, tazama, Samweli alikuwa akija kuelekea walikokwenda mahali pa juu.

9:15 1Sam 24:11; Za 25:14; Mk 11:2-4; Mdo 13:11Basi siku moja kabla Sauli hajaja, Bwana alikuwa amemfunulia Samweli jambo hili: 9:16 Kut 30:25; 1Sam 2:35; 12:3; 15:1; 26:9; 2Fal 11:12; Za 2:2; 2Sam 7:8; 1Fal 8; 16; 1Nya 5:2; Kut 3:8; 1Sam 23:4; 2Sam 3:18; Mwa 16:11; Za 102:1“Kesho wakati kama huu nitakupelekea mtu kutoka nchi ya Benyamini. Umtie mafuta awe kiongozi juu ya watu wangu Israeli, ndiye atakayewakomboa watu wangu na mkono wa Wafilisti. Nimewaangalia watu wangu, kwa kuwa kilio chao kimenifikia.”

9:17 1Sam 16:12; Hos 13:11Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, “Huyu ndiye mtu niliyekuambia habari zake, kwamba yeye atawatawala watu wangu.”

Sauli akamkaribia Samweli langoni na kumuuliza, “Tafadhali, je, waweza kuniambia mahali nyumba ya mwonaji ilipo?”

Samweli akamjibu Sauli, “Mimi ndiye mwonaji, panda utangulie mbele yangu mpaka mahali pa juu, kwa kuwa leo itakupasa kula pamoja nami na asubuhi nitakuruhusu uende na nitakuambia yale yote yaliyo moyoni mwako. 9:20 1Sam 12:13; Ezr 6:8; Isa 60:4-9; Dan 2:44; Hag 2:7; Mal 3:1Kuhusu wale punda uliowapoteza siku tatu zilizopita, usifadhaike kwa habari yao; wamepatikana. Ni kwa nani ambaye shauku yote ya Israeli imeelekea, kama si kwako na jamaa yote ya baba yako?”

9:21 Za 68:27; Kut 3:11; Mt 2:6; 1Kor 15:9; Amu 6:15; 20:35, 46; 1Sam 18:18; 15:17Sauli akajibu, “Je, mimi si Mbenyamini, kutoka kabila dogo kuliko yote ya Israeli, nao ukoo wangu si ndio mdogo kuliko koo zote za kabila la Benyamini? Kwa nini uniambie jambo la namna hiyo?”

Kisha Samweli akamleta Sauli na mtumishi wake ndani ukumbini na kuwaketisha mahali pa heshima zaidi miongoni mwa wale waliokuwa wamealikwa; jumla yao walikuwa kama watu thelathini. Samweli akamwambia mpishi, “Leta ile sehemu ya nyama niliyokupa, ile niliyokuambia iweke kando.”

9:24 Law 7:24; Hes 18:18; Eze 24:4; Mdo 10:9Hivyo mpishi akachukua mguu pamoja na kile kilichokuwa juu yake akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, “Hiki ndicho ambacho kimewekwa kwa ajili yako. Ule, kwa sababu kilitengwa kwa ajili yako kwa tukio hili, tangu niliposema, ‘Nimewaalika wageni.’ ” Naye Sauli akala pamoja na Samweli siku ile.

9:25 Kum 22:8; Yos 2:8; Mt 24:17; Lk 5:19; Mdo 10:9Baada ya kushuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, Samweli alizungumza na Sauli juu ya dari ya nyumba yake. Walipoamka mapema alfajiri, Samweli akamwita Sauli darini, akamwambia, “Jiandae, nami nitakuaga uende zako.” Sauli alipokuwa tayari yeye na Samweli wakatoka nje pamoja. Hata walipokuwa wakiteremka kuelekea mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi atangulie mbele yetu.” Naye mtumishi akafanya hivyo. “Lakini subiri hapa kwa kitambo kidogo, ili nipate kukupa ujumbe kutoka kwa Mungu.”

Read More of 1 Samweli 9

1 Samweli 10:1-8

10:1 1Sam 16:1; 9:16; 2Fal 9:1; Kut 29:7; 34:9; 1Sam 9:16; 1Fal 1:39; 2Sam 20:19; Za 78:62-71; Kum 32:9; Yer 10:16Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, Bwana hakukutia mafuta uwe kiongozi juu ya watu wake Israeli? 10:2 Mwa 35:20; 1Sam 9:4-5; Yos 18:28Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na watu wawili karibu na kaburi la Raheli, huko Selsa kwenye mpaka wa Benyamini. Watakuambia, ‘Punda wale uliotoka kwenda kuwatafuta, wamekwisha kupatikana. Sasa baba yako ameacha kufikiri kuhusu punda na sasa ana hofu kukuhusu wewe. Anauliza, “Nitafanyaje kuhusu mwanangu?” ’

10:3 Mwa 35:8; 28:22; Yos 19:22; Amu 4:6, 12; 8:18; Za 89:12“Kisha utakwenda mbele kutoka hapa mpaka uufikie mwaloni wa Tabori. Watu watatu wanaopanda kwa Mungu huko Betheli watakutana nawe hapo. Mmoja atakuwa amechukua wana-mbuzi watatu, mwingine mikate mitatu, na mwingine kiriba cha divai. 10:4 1Sam 16:20; Mit 18:20; Amu 18:15Watakusalimu na kukupa mikate miwili, ambayo utaipokea kutoka kwao.

10:5 1Sam 11:4; 15:34; 13:3; Hes 11:29; 1Fal 20:35; 2Fal 2:3; 4:1; 6:1; 9:1; 3:15; Amo 7:14; Law 26:30; Mwa 31:27; Yer 31:4; 1Fal 1:40; Isa 30:29; 1Sam 16:16; 18:10; 19:9; 19:20; Za 92:3; 1Nya 25:1; 1Kor 14:1“Baada ya hayo utakwenda Gibea ya Mungu, ambapo hapo kuna kambi ya Wafilisti. Unapokaribia mji utakutana na kundi la manabii wakiteremka kutoka mahali pa juu wakiwa na vinubi, matari, filimbi na zeze vikipigwa mbele yao, nao watakuwa wakitoa unabii. 10:6 Hes 11:25; 1Sam 19:23-24; Mt 7:22Roho wa Bwana atakuja juu yako kwa nguvu, nawe utatoa unabii pamoja nao; nawe utageuzwa kuwa mtu wa tofauti. 10:7 2Sam 7:3; 1Fal 8:17; 1Nya 22:7; 28:2; 2Nya 6:7; Mhu 9:10; Amu 9:33; Yos 1:3; Lk 1:28; Ebr 13:5Mara ishara hizi zitakapotimizwa, fanya lolote mkono wako upasao kufanya, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.

10:8 Yos 4:20; 10:43; 1Sam 7:16; 11:14; 13:4“Tangulia kushuka mbele yangu mpaka Gilgali. Hakika nami nitateremka nikujie ili kutoa dhabihu za sadaka za kuteketezwa na dhabihu za amani, lakini lazima ungoje kwa siku saba hata nitakapokujia na kukuambia likupasalo kufanya.”

Read More of 1 Samweli 10