1 Samweli 5:1-12, 1 Samweli 6:1-21, 1 Samweli 7:1-17 NEN

1 Samweli 5:1-12

Sanduku La Agano Huko Ashdodi Na Ekroni

5:1 1Sam 4:1; Yos 11:22; 13:3; 1Sam 7:12Baada ya Wafilisti kuteka Sanduku la Mungu, walilichukua kutoka Ebenezeri mpaka Ashdodi. 5:2 Amu 16:23; Isa 2:18; 19:1; 46:1Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni. 5:3 Isa 40:20; 41:7; Yer 10:4; Isa 46:7; Kut 12:12; 18:11; 1Nya 16:24-26; Za 95:3; 97:9; Isa 19:1; 46:1, 2, 7; Nah 1:14Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. 5:4 Eze 6:6; Mik 1:7; Isa 40:18; Yer 50:2Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta huyo Dagoni ameanguka chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa navyo vimelala kizingitini, ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki. 5:5 Sef 1:9Ndiyo sababu mpaka leo makuhani wa Dagoni wala wengine waingiao katika hekalu la Dagoni huko Ashdodi hawakanyagi kizingiti.

5:6 Za 32:4; 78:66; Mdo 13:11; 2Sam 6:7; Kum 28:27; 1Sam 6:5Mkono wa Bwana ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi na vijiji jirani, akaleta uharibifu juu yao na kuwatesa kwa majipu. Watu wa Ashdodi walipoona kile kilichokuwa kikitokea, wakasema, “Sanduku la Mungu wa Israeli kamwe lisikae hapa pamoja na sisi, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya Dagoni mungu wetu.” 5:8 Amu 16:18; Yos 11:12Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kuwauliza, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Mungu wa Israeli?”

Wakajibu, “Sanduku la Mungu wa Israeli na liende Gathi.” Basi wakalihamisha Sanduku la Mungu wa Israeli.

5:9 Kut 14:24; Kum 2:15Lakini baada ya kulihamisha, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi ya huo mji wa Gathi, akiuweka katika fadhaa kuu. Mungu akawatesa watu wa huo mji, vijana kwa wazee, kwa kuwaletea majipu. 5:10 Yos 13:3Basi wakapeleka Sanduku la Mungu Ekroni.

Wakati Sanduku la Mungu lilipokuwa linaingia Ekroni, watu wa Ekroni walilia wakisema “Wamelileta Sanduku la Mungu wa Israeli kwetu ili kutuua sisi na watu wetu.” Basi wakawaita watawala wote wa Wafilisti pamoja na kusema, “Liondoeni Sanduku la Mungu wa Israeli na lirudishwe mahali pake, la sivyo litatuua sisi na watu wetu.” Kwa kuwa kifo kilikuwa kimeujaza mji hofu; kwani mkono wa Mungu ulikuwa mzito sana juu yake. 5:12 1Sam 4:8; Kut 11:6; Mit 21:13; Isa 15:3; Yer 25:34; Amo 5:17; Yak 2:13Wale ambao hawakufa walipatwa na majipu, na kilio cha mji kilikwenda juu hadi mbinguni.

Read More of 1 Samweli 5

1 Samweli 6:1-21

Sanduku La Mungu Larudishwa Israeli

Sanduku la Bwana lilipokuwa limekaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba, 6:2 Kut 7:11; Isa 44:25; Mwa 41:8; Dan 2:2; 5:7; Mit 2:4Wafilisti waliwaita makuhani wa Dagoni na waaguzi, na kuwaambia, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Bwana? Tuambieni jinsi tutakavyolirudisha mahali pake.”

6:3 Kut 22:29; 34:20; Law 5; 15; Kum 16:16Wakajibu, “Kama mtalirudisha Sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe mikono mitupu bali kwa vyovyote mpelekeeni sadaka ya hatia. Kisha mtaponywa, nanyi mtafahamu kwa nini mkono wake haujaondolewa kwenu.”

6:4 Yos 13:3; Amu 3:3; 2Sam 24:25Wafilisti wakawauliza, “Ni sadaka gani ya hatia tutakayompelekea?”

Wakajibu, “Majipu matano ya dhahabu na panya wa dhahabu watano, kulingana na idadi ya watawala wa Wafilisti, kwa sababu tauni iyo hiyo imewaua ninyi na watawala wenu. 6:5 1Sam 5:6; Yos 7:19; Ufu 14:7; Isa 42:12; Yn 9:24; 1Nya 16:28; Mal 2:2; Kut 9:3; Za 39:10; Mdo 13:11Tengenezeni mifano ya majipu na ya panya wale wanaoharibu nchi yenu, nanyi mheshimuni Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka kwenu na kwa miungu yenu na nchi yenu. 6:6 Kut 4:21; 10:2; 12:33; 7:13; 9:34; Za 105:38Kwa nini ninyi mnafanya mioyo yenu migumu kama Wamisri na Farao walivyofanya? Je, alipowatendea kwa ukali, hawakuwaachia Waisraeli wakaenda zao?

6:7 2Sam 6:3; 1Nya 13:7; Hes 19:2“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ngʼombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ngʼombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na mwaweke zizini. Chukueni hilo Sanduku la Bwana na mliweke juu ya gari la kukokotwa, na ndani ya kasha kando yake wekeni hivyo vitu vya dhahabu mnavyompelekea Bwana kama sadaka ya hatia. Lipelekeni, 6:9 Yos 15:10; 21:16lakini liangalieni kwa makini. Iwapo litakwenda katika nchi yake lenyewe, kuelekea Beth-Shemeshi, basi tutajua kwamba Bwana ndiye alileta haya maafa makubwa juu yetu. Lakini kama halikwenda, basi tutajua kwamba haukuwa mkono wa Bwana uliotupiga na kwamba iliyotokea kwetu ni ajali.”

Basi wakafanya hivyo. Wakachukua ngʼombe wawili wa aina hiyo, wakawafungia hilo gari la kukokotwa, nao ndama wao wakawekwa zizini. Wakaliweka Sanduku la Bwana juu ya hilo gari la kukokotwa pamoja na lile kasha lenye ile mifano ya panya wa dhahabu na ya majipu ya dhahabu. Kisha hao ngʼombe wakaenda moja kwa moja kuelekea Beth-Shemeshi, wakishuka bila kugeuka kuume au kushoto, huku wakilia njia yote. Watawala wa Wafilisti waliwafuata hao ngʼombe hadi mpakani mwa Beth-Shemeshi.

6:13 Mwa 30:14; Rut 2:23; 1Sam 12:17Wakati huu watu wa Beth-Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao huko bondeni, walipoinua macho yao na kuona lile Sanduku, wakafurahi kuliona. 6:14 1Sam 11:7; 2Sam 24:22; 1Fal 9:21Lile gari la kukokotwa lilikuja mpaka kwenye shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi, nalo likasimama kando ya mwamba mkubwa. Watu wakapasua mbao za lile gari la kukokotwa na kutoa dhabihu wale ngʼombe kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 6:15 Yos 3:3; 21:16Walawi walilishusha Sanduku la Bwana, pamoja na lile kasha lililokuwa na vile vitu vya dhahabu na kuviweka juu ya ule mwamba mkubwa. Siku ile watu wa Beth-Shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa Bwana. 6:16 Yos 13:3; Amu 16:23; 1Sam 29:2Wale watawala watano wa Wafilisti waliona haya yote, nao wakarudi siku ile ile mpaka Ekroni.

6:17 Yos 13:3Haya ndiyo yale majipu ya dhahabu Wafilisti waliyotuma kama sadaka ya hatia kwa Bwana, moja kwa ajili ya Ashdodi, moja kwa Gaza, moja kwa Ashkeloni, moja kwa Gathi, na moja kwa Ekroni. Nayo hesabu ya wale panya wa dhahabu ilikuwa kulingana na idadi ya miji ya Wafilisti ya watawala watano wa Wafilisti: miji yao iliyozungukwa na maboma, pamoja na vijiji vya miji hiyo. Ule mwamba mkubwa, ambao juu yake waliliweka lile Sanduku la Bwana, ni ushahidi hadi leo katika shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi.

6:19 2Sam 6:7; Kut 19:21; Hes 4:5; Law 10:1-3; 2Sam 6:7; Kol 2:8; 1Pet 4:17Lakini Mungu aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-Shemeshi, akiwaua watu sabini miongoni mwao kwa sababu walichungulia ndani ya Sanduku la Bwana. Watu wakaomboleza kwa sababu ya pigo zito kutoka kwa Bwana, 6:20 2Sam 6:9; Za 130:3; Ufu 6:17; Mal 3:2; Law 11:45nao watu wa Beth-Shemeshi wakauliza, “Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu aliye mtakatifu? Sanduku litapanda kwenda kwa nani kutoka hapa?”

6:21 Yos 9:17; 15:9, 60; 1Nya 13:5-6; Amu 18:12Kisha wakatuma wajumbe kwa watu wa Kiriath-Yearimu, wakisema, “Wafilisti wamerudisha Sanduku la Bwana. Shukeni na mlipandishe huko kwenu.”

Read More of 1 Samweli 6

1 Samweli 7:1-17

7:1 Yos 6:7; 2Sam 6:3; 1Nya 13:7; 1Sam 6:21; Za 132:6Kisha watu wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la Bwana. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu juu kilimani na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la Bwana.

Samweli Awatiisha Wafilisti Huko Mispa

7:2 1Nya 13:5; Za 132:6; 1Nya 13:3Sanduku la Bwana lilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, yaani jumla ya miaka ishirini, nao watu wa Israeli wakaomboleza na kumtafuta Bwana. 7:3 Kut 30:10; 2Fal 18:5; 23:25; Yer 24:7; Mwa 31:19; Amu 2:12-13; 1Sam 12:10; 31:10; Yoe 2:12; Yos 24:14; Kum 6; 13; Mt 4:10; Lk 4:8; Amu 2:18Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa Bwana na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.” Hivyo Waisraeli wakaweka mbali Mabaali yao na Maashtorethi, nao wakamtumikia Bwana peke yake.

7:5 1Sam 1:20; Za 99:6; Yer 15:1; Yos 11:3; Amu 21:5; 1Sam 10:17; Mwa 20:7; Kum 9:19Kisha Samweli akasema, “Wakusanyeni Israeli wote huko Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa Bwana.” 7:6 Yos 11:3; Mao 2:19; Amu 2:16; 16:31; Neh 9:1, 2; 2Sam 14:14; Dan 9:3; Yoe 2:12; Law 26:40; Amu 10:10; 1Fal 8:47; Ay 33:27, 28; Za 106:6Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele za Bwana. Siku hiyo walifunga na wakaungama, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana.” Naye Samweli alikuwa kiongozi7:6 Kiongozi hapa maana yake mwamuzi. wa Israeli huko Mispa.

7:7 1Sam 17:11Wafilisti waliposikia kwamba Israeli wamekusanyika huko Mispa, watawala wa Wafilisti wakapanda ili kuwashambulia. Waisraeli waliposikia habari hiyo, waliogopa kwa sababu ya Wafilisti. 7:8 Kut 32:30; Hes 21:7; 1Sam 12:19, 23; 1Fal 18:24; Isa 37:4; Yer 15:1; 27:18Wakamwambia Samweli, “Usiache kumlilia Bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu, ili apate kutuokoa na mikono ya Wafilisti.” 7:9 Za 99:6; Kut 32:11; Kum 19:9; Yer 15:1Kisha Samweli akamchukua mwana-kondoo anyonyaye na kumtoa mzima kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. Akamlilia Bwana kwa niaba ya Israeli, naye Bwana akamjibu.

7:10 Kut 9:23; 14:24; 1Sam 2:10; Mwa 35:5; 2Sam 22:14-15; Yos 10:10Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ile Bwana alinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka hivi kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli. Watu wa Israeli wakatoka mbio huko Mispa na kuwafuatia Wafilisti, wakiwachinja njiani hadi mahali chini ya Beth-Kari.

7:12 Mwa 28:22; Kum 27:2; Yos 4:9; 1Sam 4; 1Ndipo Samweli akachukua jiwe na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita Ebenezeri,7:12 Ebenezeri maana yake jiwe la usaidizi. akisema, “Hata sasa Bwana ametusaidia.” 7:13 Amu 13:5; 1Sam 13:5Basi Wafilisti wakashindwa na hawakuvamia nchi ya Israeli tena.

Katika maisha yote ya Samweli, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi ya Wafilisti. 7:14 Yos 13:3; Amu 1:34Miji kuanzia Ekroni hadi Gathi, ile ambayo Wafilisti walikuwa wameiteka kutoka Israeli, ilirudishwa kwake, naye Israeli akazikomboa nchi jirani mikononi mwa Wafilisti. Kukawepo amani kati ya Israeli na Waamori.

7:15 1Sam 12:11; Amu 2:16-18Samweli akaendelea kama mwamuzi juu ya Israeli siku zote za maisha yake. 7:16 Mwa 12:8; Yos 10:43; 1Sam 10:8; Amo 5:5; Mdo 13; 20Mwaka hadi mwaka aliendelea kuzunguka kutoka Betheli mpaka Gilgali na Mispa, akiamua Israeli katika sehemu hizo zote. 7:17 Yos 18:25; 1Sam 8:4; 15:34; 19:18; 25:1; 28:3; 9:12; 14:35; 20:6; 2Sam 24:25Lakini kila mara alirudi Rama, kulikokuwa nyumbani kwake, huko pia aliwaamua Israeli. Naye huko alimjengea Bwana madhabahu.

Read More of 1 Samweli 7