1 Samweli 29:1-11, 1 Samweli 30:1-31, 1 Samweli 31:1-13 NEN

1 Samweli 29:1-11

Akishi Amrudisha Daudi Huko Siklagi

29:1 1Sam 28:1; 4:1; Yos 17:16; 1Fal 18:45; 21:1; 2Fal 9:30; Yer 50:5; Hos 1:4; 5:11; 2:22; Yos 12:18Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki, nao Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli. 29:2 1Sam 28:2Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi. 29:3 1Nya 12:19; 1Sam 27:7; Dan 6:5; Yn 19:6; 1Pet 3:16Majemadari wa Wafilisti wakauliza, “Vipi kuhusu hawa Waebrania?”

Akishi akajibu, “Huyu si Daudi, aliyekuwa afisa wa Sauli mfalme wa Israeli? Ameshakuwa pamoja nami kwa zaidi ya mwaka, naye tangu alipomwacha Sauli hadi sasa, sikuona kosa lolote kwake.”

29:4 1Nya 12:19; 1Sam 14:21Lakini majemadari wa Wafilisti wakamkasirikia na kusema, “Mrudishe mtu huyu, apate kurudi mahali pale ulipompangia. Haimpasi kufuatana pamoja nasi vitani, asije akageuka, akawa kinyume chetu vitani. Ni kwa njia ipi bora zaidi angeweza kujipatia tena kibali kwa bwana wake, isipokuwa kwa vichwa vya watu wetu wenyewe? 29:5 1Sam 18:7; 21:11Je, huyu si ndiye Daudi walioimba kumhusu katika ngoma zao, wakisema:

“ ‘Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake’?”

29:6 1Sam 27:8-12; Hes 27:17; 2Sam 3:25; 2Fal 19:27; Za 121:8; Isa 37:28Basi Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Kama vile Bwana aishivyo, wewe umekuwa mtu mwaminifu, nami ningependa utumike pamoja nami katika jeshi. Tangu siku ile uliyofika kwangu hadi sasa, sijaona kosa lolote kwako, lakini hao watawala hawakukubali. Rudi na uende kwa amani; usifanye chochote cha kuwakasirisha watawala wa Kifilisti.”

Daudi akamuuliza Akishi, “Lakini mimi nimefanya nini? Je, umeona nini kibaya juu ya mtumishi wako tangu siku ile niliyokuja kwako hadi leo? Kwa nini nisirudi na kupigana na adui za bwana wangu mfalme?”

29:9 2Sam 14:17, 20; 19:27Akishi akamjibu Daudi, “Mimi ninajua ya kuwa wewe umekuwa wa kupendeza machoni pangu kama vile malaika wa Mungu. Lakini hao majemadari wa Wafilisti wamesema, ‘Huyu haimpasi kwenda vitani pamoja nasi.’ 29:10 1Nya 12:19Sasa amka mapema, pamoja na watumishi wa bwana wako waliofuatana nawe, nanyi ondokeni asubuhi mara kutakapopambazuka.”

29:11 Za 37:23; 73:2; Mit 16:9; 20:24; Isa 30:21; Yer 10:23; 1Kor 10:23; 10:13; 2Sam 4:4Hivyo Daudi na watu wake wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda zao kurudi katika nchi ya Wafilisti, nao Wafilisti wakapanda kwenda Yezreeli.

Read More of 1 Samweli 29

1 Samweli 30:1-31

Daudi Aangamiza Waamaleki

30:1 1Sam 27:6-8; 29:4, 11; 15:7; Kut 17:8-16; Hes 24:20; Kum 25:17, 19; 1Nya 4:43; Eze 25:15Daudi na watu wake wakafika Siklagi siku ya tatu. Basi Waamaleki walikuwa wamevamia Negebu na Siklagi. Wakawa wameshambulia mji wa Siklagi na kuuteketeza kwa moto, 30:2 Ay 38:11; Za 76:10; 89:9; Isa 27:8; Hab 3:2nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua yeyote, bali waliwachukua wakaenda zao.

30:3 Mwa 31:26Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zao wamechukuliwa mateka. 30:4 Mwa 27:38; Hes 14:1Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia. 30:5 1Sam 25:43; 2Sam 2:2Wake wawili wa Daudi walikuwa wametekwa: yaani Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. 30:6 Kut 17:4; Yn 8:59; Za 27:14; Rut 1:13; Rum 4:20; Amu 18:25; 2Sam 17:8; Za 17:8; Yer 17:7, 17; Yoe 3:16; Rum 4:20Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.

30:7 1Sam 22:20; 2:28; 23:9Kisha Daudi akamwambia kuhani Abiathari mwana wa Ahimeleki, “Niletee kisibau.” Abiathari akamletea, 30:8 1Sam 23:2; Mwa 14:16; Kut 2:17naye Daudi akamuuliza Bwana, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?”

Bwana akajibu, “Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa.”

30:9 1Sam 27:2Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori, mahali ambapo wengine waliachwa nyuma, kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia.

30:11 Za 11:2; Mit 3:5, 6Wakamkuta Mmisri katika shamba fulani, nao wakamleta kwa Daudi. Wakampa huyo Mmisri maji ya kunywa na chakula; 30:12 Amu 15:19; 1Sam 14:27kipande cha andazi la tini na andazi la zabibu zilizokaushwa. Akala naye akapata nguvu, kwa kuwa hakuwa amekula chakula chochote wala kunywa maji kwa siku tatu usiku na mchana.

30:13 1Sam 14:48Daudi akamuuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?”

Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita. 30:14 2Sam 8:18; 15:18; 20:2, 23; 1Fal 1:38, 44; 1Nya 18:17; Sef 2:5; Yos 14:13; 15:13Tulivamia Negebu ya Wakerethi, na nchi ya Yuda, na Negebu ya Kalebu. Nasi tulichoma moto Siklagi.”

30:15 Kum 23:15Daudi akamuuliza, “Je, unaweza kuniongoza kufikia kundi hili la uvamizi?”

Akajibu, “Niapie mbele ya Mungu kwamba hutaniua wala kunikabidhi mikononi mwa bwana wangu, nami nitakupeleka hadi waliko.”

30:16 Lk 12:19; Yos 22:830:16 Kut 32:6; 1Sam 25:36-38; 2Sam 13:28; Dan 5:1-4; Lk 12:19-20; 21:34; 1The 5:3; Ufu 11:10, 13Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda. 30:17 1Sam 11:11; 2Sam 1:1; 15:3; 1:830:17 Ay 20:5Daudi akapigana nao kuanzia machweo ya jua hadi kesho yake jioni, na hakuna yeyote miongoni mwao aliyetoroka, isipokuwa vijana wanaume 400 waliopanda ngamia na kutoroka. 30:18 Mwa 14:16; Za 34:9Daudi akarudisha kila kitu Waamaleki walikuwa wamechukua, pamoja na wake zake wawili. Hakuna chochote kilichopotea: kijana au mzee, mvulana au msichana, nyara au kitu kingine chochote walichokuwa wamechukua. Daudi akarudisha kila kitu. Akachukua makundi yote ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, nao watu wake wakawaswaga wanyama hao mbele ya wanyama wengine wa kufugwa, wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.”

30:21 Amu 18:9Kisha Daudi akafika kwa wale watu 200 waliokuwa wamechoka sana kumfuata na ambao waliachwa nyuma kwenye Bonde la Besori. Wakatoka kwenda kumlaki Daudi na wale watu aliokuwa nao. Daudi na watu wake walipowakaribia, akawasalimu. 30:22 Kum 13:13; Amu 19:22; 1Sam 22:2; 25:17; 1Fal 21:10Lakini watu wote waovu na wakorofi miongoni mwa wafuasi wa Daudi wakasema, “Kwa sababu hawakwenda pamoja nasi, hatutagawana nao nyara tulizorudisha. Lakini, kila mtu aweza kuchukua mkewe na watoto wake na kuondoka.”

Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Bwana ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu. 30:24 Hes 31:27; Amu 5:30; Yos 22:8Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyekwenda vitani. Wote watashiriki sawa.” Daudi akafanya hili liwe amri na agizo kwa Israeli kutoka siku ile hata leo.

30:26 Mwa 33:11Daudi alipofika Siklagi, akatuma baadhi ya nyara kwa wazee wa Yuda, waliokuwa rafiki zake, akasema, “Tazama, hapa kuna zawadi kwa ajili yenu kutoka nyara za adui za Bwana.”

30:27 Yos 7:2; 10:40; 15:48; 19:8; Mwa 12:8; Yos 7:2; 10:40Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri; 30:28 Hes 32:34; Yos 13:16; 1Nya 27:27; Yos 15:50kwa wale walioko Aroeri, Sifmothi, Eshtemoa 30:29 1Sam 27:10; Amu 1:16; 1Sam 15:6na Rakali; kwa wale waliokuwa katika miji ya Wayerameeli na ya Wakeni; 30:30 Hes 13:22; Yos 10:36; 14:13; 2Sam 2:1-4na kwa wale walioko Horma, Bori-Ashani, Athaki, 30:31 Hes 13:22; Yos 10:36; 14:13; 2Sam 2:1-4na kwa wakazi wa Hebroni; na kwa wale waliokuwa mahali pengine pote ambako Daudi na watu wake walitembelea.

Read More of 1 Samweli 30

1 Samweli 31:1-13

Sauli Ajiua

(1 Nyakati 10:1-12)

31:1 1Sam 28:4; 1Nya 10:1-12; 1Sam 29:1; 1Nya 8:33Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika Mlima Gilboa. 31:2 1Sam 28:19; 18:1; 14:49; 1Nya 8:33Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 31:3 1Sam 28:4; 2Sam 1:6Mapigano yakawa makali sana kumzunguka Sauli, nao wapiga upinde wakampata na kumjeruhi vibaya.

31:4 Amu 9:54; Mwa 34:14; 1Sam 14:6; 2Sam 1:6, 10Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja wanichome na kunidhalilisha.”

Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. Mchukua silaha wake alipoona Sauli amekufa, naye pia akaangukia upanga wake akafa pamoja naye. 31:6 1Sam 26:10; 12:25; 1Nya 10:6; Rum 6:23Basi Sauli, wanawe watatu, mbeba silaha wake na watu wake wote wakafa pamoja siku ile ile.

Waisraeli waliokuwa kandokando ya bonde na wale waliokuwa ngʼambo ya Yordani walipoona kuwa jeshi la Waisraeli limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, wakaacha miji yao na kukimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.

31:8 2Sam 1:20Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe watatu wameanguka katika Mlima Gilboa. 31:9 1Sam 1:20; 4:4; Amu 16:24Wakamkata Sauli kichwa na kumvua silaha zake, nao wakatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari katika hekalu la sanamu zao na miongoni mwa watu wao. 31:10 Amu 2:12-13; 1Sam 7:3; Yos 17:11; 2Sam 21:12; 1Sam 21:9; Amu 1:27Wakaweka silaha zake katika hekalu la Maashtorethi, na kukifunga kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-Shani.

31:11 Amu 21:8; 1Sam 11:1Watu wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yale Wafilisti walichomfanyia Sauli, 31:12 Za 76:5; Mwa 38:24; Amo 6:10; 2Nya 16:14; 1Sam 11:1-11; 2Sam 2:4-7; Yer 34:5; Amo 6:10mashujaa wao wote wakaenda usiku hadi Beth-Shani. Wakauchukua mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka kwenye ukuta wa Beth-Shani na kurudi hadi Yabeshi, mahali ambapo waliiteketeza kwa moto. 31:13 2Sam 21:12-14; Mwa 21:33; 2Sam 3:35; 12:19-23; 1:12; Mwa 50:10; 1Sam 22:6; Mwa 50:10; Ay 2:13Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.

Read More of 1 Samweli 31