1 Samweli 24:1-22, 1 Samweli 25:1-44 NEN

1 Samweli 24:1-22

Daudi Amwacha Sauli Hai

24:1 Yos 15:62; 1Sam 23:28-29Baada ya Sauli kurudi kuwafuatia Wafilisti, akaambiwa kwamba, “Daudi yuko katika Jangwa la En-Gedi.” 24:2 1Sam 26:2; Za 38:12Basi Sauli akachukua watu hodari 3,000 kutoka Israeli yote kwenda kumsaka Daudi na watu wake karibu na Majabali ya Mbuzi-Mwitu.

24:3 Amu 3:24Akaja mpaka kwenye mazizi ya kondoo kando ya njia, hapo palikuwa na pango, na Sauli akaingia ndani kujipumzisha. Daudi na watu wake walikuwa wamo mle pangoni kwa ndani zaidi. 24:4 1Sam 25:28-30; 2Sam 4:8; 1Sam 23; 17; 26:8Watu wa Daudi wakasema, “Hii ndiyo siku aliyonena Bwana akikuambia, ‘Nitamtia adui yako mikononi mwako ili wewe umtendee utakavyo.’ ” Basi Daudi akanyemelea bila kuonekana na kukata upindo wa joho la Sauli.

24:5 1Sam 26:9; 2Sam 24:10Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli. 24:6 Mwa 26:11; 1Sam 12:3; 26:11; 2Sam 1:14; Ay 31:29, 30Akawaambia watu wake, “Bwana na apishie mbali nisije nikafanya jambo kama hilo kwa bwana wangu, yeye ambaye ni mpakwa mafuta wa Bwana, au kuinua mkono wangu dhidi yake; kwani yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.” 24:7 Za 7:4; Mt 5:44; Rum 12:17Kwa maneno haya Daudi akawaonya watu wake na hakuwaruhusu wamshambulie Sauli. Naye Sauli akaondoka pangoni na kwenda zake.

24:8 1Sam 20:41; 25:23-24Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi. 24:9 Za 141:6; Mit 16:28; 17:9Akamwambia Sauli, “Kwa nini unasikiliza wakati watu wanapokuambia, ‘Daudi amenuia kukudhuru’? Leo umeona kwa macho yako mwenyewe jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu huko pangoni. Watu wengine walisisitiza nikuue, lakini nilikuacha, nikisema, ‘Sitainua mkono wangu dhidi ya bwana wangu, kwa sababu yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.’ 24:11 Za 7:3; 1Sam 25:28; Za 35:7; Mwa 31:36; 1Sam 26:20; 20:1Tazama, baba yangu, ona kipande hiki cha joho lako mkononi mwangu! Nilikata upindo wa joho lako lakini sikukuua. Basi ujue na kutambua kuwa sina hatia ya kutenda mabaya wala ya kuasi. Wewe sijakukosea, lakini wewe unaniwinda mimi ili kuuondoa uhai wangu. 24:12 Mwa 16:5; 1Sam 25:38; Ay 9:15; Hes 31:3; Amu 11:27Bwana na ahukumu kati yangu na wewe. Naye Bwana alipize mabaya unayonitendea, lakini mkono wangu hautakugusa. 24:13 Mt 7:20Kama msemo wa kale usemavyo, ‘Kutoka kwa watenda maovu hutoka matendo maovu,’ kwa hiyo mkono wangu hautakugusa wewe.

24:14 1Sam 17:43; 26:20; 2Sam 9:8; Ay 32:9; Mit 5:23“Je, mfalme wa Israeli ametoka dhidi ya nani? Ni nani unayemfuatia? Je, ni mbwa mfu? Ni kiroboto? 24:15 Za 35:1, 23; Isa 49:25; Za 26:1; 35:24; 43:1; 50:4; 54:1; 135:14; 119:134; 2Sam 9:8Bwana na awe mwamuzi wetu, yeye na aamue kati yetu. Yeye na anitetee shauri langu; anihesabie haki kwa kuniokoa mkononi mwako.”

24:16 1Sam 16:17; 26:17Daudi alipomaliza kusema haya, Sauli akamuuliza, “Je, hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?” Ndipo Sauli akalia kwa sauti kuu, akisema, 24:17 Mwa 38:26; Mt 5:44; Kut 9:27; 1Sam 26:21“Wewe ni mwenye haki kuliko mimi; umenitendea mema, lakini mimi nimekutendea mabaya. 24:18 1Sam 26:23Sasa umeniambia juu ya mema uliyonitendea. Bwana alinitia mikononi mwako, lakini wewe hukuniua. 24:19 Rut 2:12; 2Nya 15:7Je, mtu ampatapo adui yake, humwacha aende zake bila kumdhuru? Bwana na akulipe mema kwa jinsi ulivyonitenda leo. 24:20 1Sam 20:31; 13:14; 23:17; 23:17; 2Sam 3:17; Ay 15:25; Mt 2:3-6, 13, 14Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na ya kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako. 24:21 Mwa 21:23; 47:31; 1Sam 18:3; 2Sam 21:1-9; 1Sam 20:14-15Sasa niapie kwa Bwana kwamba hutakatilia mbali uzao wangu wala kulifuta jina langu kutoka jamaa ya baba yangu.”

24:22 1Sam 23:29Basi Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akarudi zake nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.

Read More of 1 Samweli 24

1 Samweli 25:1-44

Daudi, Nabali Na Abigaili

25:1 1Sam 28:3; Law 10:6; Hes 20:29; Kum 34:8; Mwa 21:2; 1Sam 7:17; 2Nya 33:20Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama.

Kisha Daudi akateremka kwenye Jangwa la Maoni. 25:2 Yos 15:55; 2Sam 19:32; Mwa 31:19; 1Sam 23:24; Mwa 38:13; 2Sam 13:23Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na makao huko Karmeli, alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli. 25:3 Mit 31:10; Yos 14:13; 15:13; Rut 4:11; Mit 14:1; 24:3, 4; Isa 32:5, 7Jina la mtu huyo lilikuwa Nabali, naye mkewe aliitwa Abigaili. Alikuwa mwanamke mwenye busara na mzuri wa sura, lakini mumewe, ambaye alikuwa wa ukoo wa Kalebu, alikuwa mwenye hasira na mchoyo katika utendaji wake.

25:4 Mwa 38:13; 2Sam 13:23Daudi alipokuwa huko jangwani, akasikia kuwa Nabali alikuwa anakata kondoo manyoya. 25:5 1Sam 18:28; Lk 10:5Basi akatuma vijana kumi na kuwaambia, “Pandeni kwa Nabali huko Karmeli, mkamsalimie kwa jina langu. 25:6 Za 122:7; Mt 10:12; 1Nya 12:18Mwambieni: ‘Amani iwe kwako! Amani iwe kwako pamoja na wa nyumbani mwako! Pia amani iwe pamoja na vyote ulivyo navyo!

“ ‘Nasikia kuwa huu ni wakati wa kukata kondoo manyoya. Wachunga mifugo wako walipokuwa pamoja nasi, hatukuwatendea mabaya na wakati wote waliokuwa huko Karmeli hakuna chochote chao kilipotea. 25:8 Neh 8:10; Es 9:19Waulize watumishi wako nao watakuambia. Kwa hiyo uwatendee wema vijana wangu, kwani tumekuja wakati wa furaha. Tafadhali wape watumishi wako na mwanao Daudi chochote kitakachokuja mkononi mwako kwa ajili yao.’ ”

Watu wa Daudi walipofika wakampa Nabali ujumbe huu kwa jina la Daudi. Kisha wakangojea.

25:10 Amu 9:28; Za 73:7, 8; 123:3, 4Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, “Huyu Daudi ni nani? Huyu mwana wa Yese ni nani? Watumishi wengi wanakimbia kutoka kwa bwana zao siku hizi. 25:11 Amu 8:6Kwa nini nichukue mkate wangu, maji yangu na nyama niliyochinja kwa ajili ya wakata manyoya wangu, na kuwapa watu ambao hakuna anayejua wanakotoka?”

Watu wa Daudi wakageuka na kurudi. Walipofika, wakaarifu kila neno. 25:13 1Sam 22:2; 21:10; 23:13; 30:24; Hes 31:27Daudi akawaambia watu wake, “Jifungeni panga zenu!” Basi wakajifunga panga zao, naye Daudi akajifunga upanga wake. Watu kama mia nne hivi wakapanda pamoja na Daudi, na watu mia mbili wakabaki na vifaa.

25:14 1Sam 13:10Mmoja wa watumishi akamwambia Abigaili, mkewe Nabali: “Daudi alituma wajumbe kutoka jangwani kumpa bwana wetu salamu zake, lakini akawavurumishia matukano. Hata hivyo watu hawa walikuwa wema sana kwetu. Hawakututendea mabaya, na wakati wote tulipokuwa nje huko mashambani karibu nao, hatukupotewa na kitu chochote. 25:16 Kut 14:22; Ay 1:10; Za 139:5; Zek 2:5Usiku na mchana walikuwa ukuta wakituzunguka wakati wote tulipokuwa tukichunga kondoo zetu karibu nao. 25:17 Kum 13:13; 1Sam 20:7Sasa fikiri juu ya jambo hili na uone unaweza kufanya nini, kwa sababu maafa yanakaribia juu ya bwana wetu na nyumba yake yote. Yeye ni mtu mwovu kiasi kwamba hakuna mtu awezaye kuzungumza naye.”

25:18 Law 23:14; 1Sam 17:17; 1Nya 12:40; Mwa 42:26; 2Sam 16:1; Isa 30:6Abigaili akafanya haraka, akachukua mikate mia mbili, viriba viwili vya divai, kondoo watano waliochinjwa vipimo vitano vya bisi, vishada mia moja vya zabibu kavu, mikate mia mbili ya tini, akavipakia juu ya punda. 25:19 Mwa 32:20; 1Sam 25:36Kisha akawaambia watumishi wake, “Tangulieni; mimi nitakuja nyuma yenu.” Lakini hakumwambia Nabali mumewe.

Ikawa alipokuwa amepanda punda wake kwenye bonde la mlima, tazama, Daudi na watu wake wakawa wanateremka kumwelekea, naye akakutana nao. 25:21 Za 109:5; 1Sam 19:4; Mwa 44:4; Za 35:12; Mit 17:13; Yer 18:20; 1Pet 2:20; 3:17Daudi alikuwa amesema, “Ilikuwa ni kazi bure kuchunga kwangu kote mali za huyu mtu huko jangwani hivi kwamba hakuna chochote chake kilichopotea. Yeye amenilipa baya kwa ajili ya wema. 25:22 Rut 1:17; 1Fal 14:10; 21:21; 2Fal 9:8; 1Sam 20:13Bwana na amshughulikie Daudi, tena kwa ukali, ikiwa kesho asubuhi nitambakizia mwanaume hata mmoja aliye hai miongoni mwa watu wake wote!”

25:23 Mwa 19:1; 1Sam 20:41; Yos 15:18; Amu 1:14Abigaili alipomwona Daudi, akashuka haraka kwenye punda wake, akainama kifudifudi uso wake mpaka nchi mbele ya Daudi. 25:24 2Sam 14:9Akamwangukia miguuni pake na kusema: “Bwana wangu, kosa hili na liwe juu yangu mwenyewe. Tafadhali mruhusu mtumishi wako aseme nawe. Sikia kile mtumishi wako atakachosema. 25:25 Mit 17:12; 12:16; 14:16; 20:3; Isa 32:5Bwana wangu na asimjali huyo mtu mwovu Nabali. Yeye anafanana na jina lake; jina lake ni Mpumbavu, nao upumbavu huenda pamoja naye. Lakini kwangu mimi, mtumishi wako, sikuwaona hao watu waliotumwa na bwana wangu.

25:26 Ebr 10:30; 2Sam 18:32; 2Fal 2:2; Mwa 20:6; Rum 12:19; 2Sam 18:32“Basi sasa, kwa kuwa Bwana amekuzuia, wewe bwana wangu, kutokumwaga damu na kutolipiza kisasi kwa mikono yako mwenyewe, hakika kama Bwana aishivyo na kama uishivyo, maadui zako na wote wanaokusudia kumdhuru bwana wangu wawe kama Nabali. 25:27 Mwa 33:11; 1Sam 30:26Nayo zawadi hii ambayo mtumishi wako amemletea bwana wangu, wapewe watu wanaofuatana nawe. 25:28 2Sam 14:9; 7:11, 26; 1Sam 18:17; 24:11; 1Fal 9:5; 1Nya 17:16Tafadhali samehe kosa la mtumishi wako, kwa kuwa Bwana kwa hakika ataifanya imara nyumba ya ufalme kwa bwana wangu, kwa sababu anapigana vita vya Bwana. 25:29 1Sam 20:1; Yer 10:18; 22:26; 1Sam 17:50; 2Sam 4:8; Za 66:9; Mit 10:29, 30; Mdo 17:28Hata ingawa yuko mtu anayekufuatia kuuondoa uhai wako, usiruhusu baya lolote kuonekana kwako siku zote za maisha yako, uhai wa bwana wangu utafungwa salama kwenye furushi la walio hai na Bwana Mungu wako. Lakini uhai wa adui zako atavurumishwa kama vile jiwe kutoka kwenye kombeo. 25:30 1Sam 12:12; 13:14Bwana atakapokuwa ameshamtendea bwana wangu kila kitu chema alichoahidi kumhusu yeye na kumweka kuwa kiongozi wa Israeli, 25:31 Mwa 40:14; 2Sam 3:10bwana wangu hatakuwa na dhamiri inayolemewa na mzigo kwa kumwaga damu kusiko na sababu, au kujilipizia kisasi yeye mwenyewe. Bwana atakapomletea bwana wangu mafanikio, umkumbuke mtumishi wako.”

25:32 Mwa 24:27; Kut 18:10; Lk 1:68; Ezr 7:27; Za 41:12, 13; 72:18; 2Kor 8:16Daudi akamwambia Abigaili, “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyekutuma kunilaki leo. Ubarikiwe kwa uamuzi wako mzuri na kwa kunizuia nisimwage damu leo na kulipiza kisasi kwa mikono yangu. La sivyo, hakika kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye amenizuia nisiwadhuru, kama usingekuja haraka kunilaki, hakuna hata mwanaume mmoja wa Nabali angeachwa hai kufikia mapambazuko.”

25:35 Mwa 19:21; 2Fal 5:19; 1Sam 20:42; 2Sam 15:9; Lk 7:50Ndipo Daudi akapokea kutoka mkononi mwake kile alichokuwa amemletea, naye akasema, “Nenda nyumbani kwako kwa amani; nimesikia maneno yako na kukujalia ombi lako.”

25:36 Rut 3:7; Mit 20:1; Mhu 10:17; Isa 5:11, 22; 22:13; 28:7; 56:12; Hos 4; 11; 2Sam 13:23Abigaili alipokwenda kwa Nabali, alikuwa ndani ya nyumba yake akifanya karamu kama ile ya mfalme. Naye alikuwa ana furaha nyingi, akiwa amelewa sana. Kwa hiyo Abigaili hakumwambia mumewe kitu chochote mpaka asubuhi yake. 25:37 Kut 15:16; Kum 28:28; Ay 15:21Basi asubuhi, Nabali alipokuwa amelevuka, mkewe akamwambia mambo yote, nao moyo wake ukazimia, akawa kama jiwe. 25:38 Kum 32:35; 1Sam 24:12; 26:10; 2Sam 6:7; 12:15; Kut 12:29; 2Sam 6:7; Ay 12:10; Za 104:29; Mdo 12:23Baada ya siku kumi, Bwana akampiga Nabali, naye akafa.

25:39 Mit 22:23; 2Sam 3:28, 29; 1Fal 2:44; Es 7:10; Za 7:16Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, “Ahimidiwe Bwana, ambaye amenitetea shauri langu dhidi ya Nabali kwa kuwa alinitendea kwa dharau. Amemzuia mtumishi wake asitende mabaya na Bwana ameuleta ubaya wa Nabali juu ya kichwa chake mwenyewe.”

Kisha Daudi akatuma ujumbe kwa Abigaili kumwomba awe mke wake. Watumishi wa Daudi wakaenda mpaka Karmeli na kumwambia Abigaili, wakisema, “Daudi ametutuma kwako kukuchukua uwe mkewe.”

25:41 Rut 2:10, 13; Mit 15:33; 18:12Akainama chini uso wake mpaka ardhini, akasema, “Mjakazi wako yuko hapa, tayari kuwatumikia na kuwanawisha miguu watumishi wa bwana wangu.” 25:42 2Sam 2:2; 3:3; 1Nya 3:1Abigaili akainuka kwa haraka, akapanda punda wake, akihudumiwa na wajakazi wake watano, akaenda pamoja na wajumbe wa Daudi, naye akawa mkewe. 25:43 2Sam 3:2; 1Nya 3:1; 1Sam 30:5; 2Sam 2:2; Yos 15:56Pia Daudi alikuwa amemwoa Ahinoamu wa Yezreeli, wote wawili wakawa wake zake. 25:44 2Sam 3:15; Isa 10:30Lakini Sauli alikuwa amemwoza Mikali binti yake, aliyekuwa mkewe Daudi, kwa Palti mwana wa Laishi, kutoka Galimu.

Read More of 1 Samweli 25