1 Samweli 21:1-15, 1 Samweli 22:1-23, 1 Samweli 23:1-29 NEN

1 Samweli 21:1-15

Daudi Huko Nobu

21:1 1Sam 22:9; Neh 11:32; Isa 10:32; 1Sam 16:1Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamuuliza, “Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu yeyote?”

21:2 Mwa 27:20-24; 1Sam 19:11; 22:22; 1Fal 13:18; Za 119:29; 141:3; Mit 29:25; Gal 2:12, 13; Kol 3:9Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, “Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi yako wala maagizo yako!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia tukutane mahali fulani. Sasa basi, una nini mkononi? Nipatie mikate mitano au chochote unachoweza kupata.”

21:4 Law 24:8-9; Mt 12:4; Kut 19:15; Law 15:18; 24:5; Zek 7:3Lakini kuhani akamjibu Daudi, “Sina mkate wowote wa kawaida kwa sasa. Hata hivyo, ipo hapa mikate iliyowekwa wakfu, iwapo watu wamejitenga na wanawake.”

21:5 Kum 23:9-11; Yos 3:5; 2Sam 11:11; 1Tim 4:4; 1The 4:4; Law 8:26Daudi akajibu, “Hakika tumejitenga na wanawake kwa siku hizi chache kama kawaida ya ninapotoka kwenda kwenye shughuli. Navyo vyombo vya wale vijana huwa ni vitakatifu hata kwenye safari ya kawaida, si zaidi sana leo vyombo vyao vitakuwa ni vitakatifu?” 21:6 Kut 25:30; 1Sam 22:10; Mt 12:3-4; Mk 2:25-28; Lk 6:1-5; Law 24:8Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwepo mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonyesho iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za Bwana na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.

21:7 1Sam 22:9; 14:47; Za 52Basi siku hiyo palikuwepo na mmoja wa watumishi wa Sauli, aliyezuiliwa mbele za Bwana; alikuwa Doegi Mwedomu, kiongozi wa wachunga wanyama wa Sauli.

Daudi akamuuliza Ahimeleki, “Je, unao mkuki au upanga hapa? Sikuleta upanga wala silaha nyingine yoyote, kwa sababu shughuli ya mfalme ilikuwa ya haraka.”

21:9 1Sam 17:51; 17:2, 4Kuhani akajibu, “Upanga wa Goliathi Mfilisti, ambaye ulimuua katika Bonde la Ela, upo hapa, umefungiwa katika kitambaa nyuma ya kisibau. Kama unauhitaji, uchukue, hakuna upanga mwingine hapa ila huo tu.”

Daudi akasema, “Hakuna upanga mwingine kama huo. Nipatie huo.”

Daudi Huko Gathi

21:10 1Sam 25:13; 27:2-3; 18:7Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi. 21:11 1Sam 18:7; 29:5; Za 50Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema:

“ ‘Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake’?”

Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi. 21:13 Za 34Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake.

Akishi akawaambia watumishi wake, “Tazameni mtu huyu! Ana wazimu! Kwa nini mnamleta kwangu? Je, mimi nimepungukiwa na wenda wazimu kiasi kwamba mmeniletea mtu huyo hapa aendelee kufanya hivi mbele yangu? Je, ilikuwa ni lazima mtu huyo aje nyumbani kwangu?”

Read More of 1 Samweli 21

1 Samweli 22:1-23

Daudi Akiwa Adulamu Na Mispa

22:1 Mwa 38:1Daudi akaondoka Gathi na kukimbilia kwenye pango la Adulamu. Ndugu zake na watu wa nyumba ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 22:2 1Sam 23:13; 25:13; 2Sam 15:20; Amu 11:3Wale wote waliokuwa katika dhiki au waliokuwa na madeni au wale ambao hawakuridhika wakamkusanyikia Daudi, naye akawa kiongozi wao. Watu wapatao 400 walikuwa pamoja naye.

22:3 Mwa 47:11; Kut 20:12; Law 19:3; Kum 5:16; Mit 10:1; 23:24; Mt 19:19; Yn 19:25-27; Efe 6:2; 1Tim 5:4Kutoka huko Daudi akaenda Mispa huko Moabu na kumwambia mfalme wa Moabu, “Naomba uwaruhusu baba yangu na mama yangu waje kukaa nawe mpaka nijue nini Mungu atakachonifanyia.” 22:4 Mwa 19:37Hivyo akawaacha wazazi wake wakae na mfalme wa Moabu, nao wakakaa naye muda wote ambao Daudi alikuwa ngomeni.

22:5 2Sam 24:11; 1Nya 21:9; 29:29; 2Nya 29:25; 23:14Ndipo nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae ngomeni. Nenda katika nchi ya Yuda.” Hivyo Daudi akaondoka na kwenda katika msitu wa Herethi.

Sauli Awaua Makuhani Wa Nobu

22:6 Amu 4:5; Mwa 21:23Basi Sauli akasikia kwamba Daudi na watu wake wameonekana. Sauli akiwa na mkuki mkononi, alikuwa ameketi chini ya mti wa mkwaju kwenye kilima huko Gibea, maafisa wake wote wakiwa wamesimama kumzunguka. 22:7 Kum 1:15; 1Sam 8:14Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia? 22:8 1Sam 18:3; 20:16; 23:21Je, ndiyo sababu ninyi mkapanga hila mbaya dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu ambaye ameniambia ni lini mwanangu alifanya agano na mwana wa Yese. Hapana hata mmoja wenu anayejishughulisha nami wala anayeniambia kwamba mwanangu amechochea mtumishi wangu kunivizia, kama afanyavyo leo.”

22:9 1Sam 21:7; 14:3; 21:1; Za 52Lakini Doegi Mwedomu, ambaye alikuwa akisimama na maafisa wa Sauli, akasema, “Nilimwona mwana wa Yese akija kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu huko Nobu. 22:10 Mwa 25:22; 1Sam 23:2; 21:6; 17:51; Hes 27:21; 27:21Ahimeleki akamuuliza Bwana kwa ajili yake; pia akampa vyakula na ule upanga wa Goliathi Mfilisti.”

Kisha mfalme akatuma watu wamwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu, na jamaa yote ya baba yake, waliokuwa makuhani huko Nobu, nao wote wakaja kwa mfalme. Sauli akasema, “Sikiliza sasa, mwana wa Ahitubu.”

Akajibu, “Naam, bwana wangu.”

Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga shauri baya dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga, tena hukumuuliza Mungu kwa ajili yake, na kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?”

22:14 1Sam 19:4; 19:5; 20:32; 24:11; Mit 31:9Ahimeleki akamjibu mfalme, “Ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliye mwaminifu kama Daudi, mkwewe mfalme, kiongozi wa walinzi wako na anayeheshimika sana katika watu wa nyumbani mwako? Je, siku hiyo ilikuwa ndiyo ya kwanza kumwomba Mungu kwa ajili yake? La hasha! Mfalme na usiwashutumu watumishi wako wala yeyote wa jamaa ya baba yake, kwa kuwa mtumishi wako hafahamu lolote kabisa kuhusu jambo hili lote.”

22:16 1Sam 2:31Lakini mfalme akasema, “Ahimeleki, hakika utakufa, wewe na jamaa yote ya baba yako.”

22:17 Kut 1:17; Mdo 4:19; 5:29Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Bwana, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.”

Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa Bwana.

22:18 1Sam 4:17; 2:18; 2:31; Za 12:5; Mit 28:15; Kut 28:40Kisha mfalme akamwagiza Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Hivyo basi Doegi Mwedomu, akageuka na kuwaua. Siku ile aliwaua watu themanini na watano wavaao visibau vya kitani. 22:19 1Sam 15:3; 21:1; Neh 11:32; Isa 10:32; Ay 20:19, 20; Za 10:1-18; Isa 26:13Pia akaupiga Nobu kwa upanga, mji wa makuhani, wakiwemo wanaume na wanawake, watoto wadogo na wale wanyonyao, ngʼombe wake, punda na kondoo.

22:20 1Sam 23:6; 30:7; 2Sam 15:24; 20:25; 1Fal 1:7; 2:22, 26-27; 2Fal 4:4; 1Nya 15:11; 27:34; 1Sam 14:3; 2:32Lakini Abiathari, mwana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akatoroka, akakimbia na kujiunga na Daudi. Akamwambia Daudi kuwa Sauli amewaua makuhani wa Bwana. 22:22 1Sam 21:7Kisha Daudi akamwambia Abiathari: “Siku ile, wakati Doegi Mwedomu alipokuwa pale, nilijua atahakikisha amemwambia Sauli. Mimi ninawajibika kwa vifo vya jamaa ya baba yako yote. 22:23 1Sam 20:1Kaa pamoja nami; usiogope. Mtu anayeutafuta uhai wako anautafuta uhai wangu pia. Ukiwa pamoja nami utakuwa salama.”

Read More of 1 Samweli 22

1 Samweli 23:1-29

Daudi Aokoa Keila

23:1 Yos 15:44; Hes 18:27; Amu 6:11Daudi alipoambiwa kuwa, “Tazama, Wafilisti wanapigana dhidi ya Keila nao wanapokonya nafaka katika sakafu za kupuria,” 23:2 1Sam 22; 10; 30:8; 2:1; 2Sam 5:19; Za 50:19; Hes 27:21; Amu 1:1; 1Sam 28:6; 30:8; 1Nya 10:14; 14:10; Za 32:8; 37:5; Mit 3:5, 6; Yer 10:23; Yak 1:5akauliza kwa Bwana, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?”

Bwana akamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uuokoe Keila.”

Lakini watu wa Daudi wakamwambia, “Hapa Yuda kwenyewe tunaogopa. Si zaidi sana, kama tukienda Keila dhidi ya majeshi ya Wafilisti!”

23:4 1Sam 9:16; Yos 8:7; Amu 7:7Daudi akauliza kwa Bwana tena, naye Bwana akamjibu akamwambia, “Shuka uende Keila, kwa kuwa nitawatia Wafilisti mkononi mwako.” Basi Daudi na watu wake wakaenda Keila, wakapigana na Wafilisti na kutwaa wanyama wao wa kutosha. Daudi akawatia hasara kubwa Wafilisti na kuwaokoa watu wa Keila. 23:6 1Sam 22:20; 2:28; Ay 1:15-19(Basi Abiathari mwana wa Ahimeleki alikuwa ameleta kisibau alipokimbilia kwa Daudi huko Keila.)

Sauli Anamfuata Daudi

23:7 Kum 32:30; Za 31:21; Kut 15:9; 1Sam 24:4-6; 26:8, 9; Za 79:11Sauli akaambiwa kwamba Daudi alikuwa amekwenda Keila, naye akasema, “Mungu amemtia mkononi mwangu, kwa kuwa Daudi amejifunga mwenyewe kwa kuingia kwenye mji wenye malango na makomeo.” Naye Sauli akayaita majeshi yake yote yaende vitani, kuishukia Keila ili kumzingira Daudi na watu wake kwa jeshi.

23:9 1Sam 22:20; 2:28; 30:7Daudi alipojua kuwa Sauli alikuwa ana hila dhidi yake, akamwambia Abiathari kuhani, “Leta kile kisibau.” 23:10 1Sam 22:19; 2Sam 20:20; Es 3:6; Za 44:22Daudi akasema, “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mtumishi wako amesikia kwa hakika kwamba Sauli anapanga kuja Keila na kuangamiza mji kwa ajili yangu. Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atateremka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.”

Naye Bwana akasema, “Ndiyo, atashuka.”

Daudi akauliza tena, “Je watu wa Keila watanisalimisha mimi pamoja na watu wangu kwa Sauli?”

Naye Bwana akasema, “Ndiyo, watafanya hivyo.”

23:13 1Sam 22:2; 25:13Basi Daudi na watu wake, wapatao 600, wakaondoka Keila wakawa wanakwenda sehemu moja hadi nyingine. Sauli alipoambiwa Daudi ametoroka kutoka Keila, hakwenda huko.

23:14 Za 55:7; Yos 15:24; Za 54:3-4; 32:7; 11:1; Yos 15:55; 1Sam 27:1; Mit 1:16; 4:16; Kum 33:3; 1Sam 2:9; Za 32:7; 33:18; Mit 2:8; Rum 8:31; 2Tim 3:11; 4:17, 18Daudi akakaa katika ngome za jangwani na katika vilima vya Jangwa la Zifu. Siku baada ya siku Sauli aliendelea kumsaka, lakini Mungu hakumtia Daudi mikononi mwake.

23:15 1Sam 20:1Daudi alipokuwa huko Horeshi katika Jangwa la Zifu, akajua kuwa Sauli alikuwa amekuja ili amuue. 23:16 1Sam 30:6; Za 18:2; 27:14Naye Yonathani mwana wa Sauli akamwendea Daudi huko Horeshi na kumtia moyo kusimama imara katika imani yake kwa Mungu. 23:17 1Sam 20:31; 24:20Akamwambia, “Usiogope, Daudi; baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, nami nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.” 23:18 1Sam 18:3; 2Sam 9:1; 21:7Wote wawili wakaweka agano mbele za Bwana. Kisha Yonathani akaenda zake nyumbani, lakini Daudi akabaki Horeshi.

23:19 1Sam 26:1; Za 54; 1Sam 26:3Basi Wazifu wakakwea kwa Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu katika ngome huko Horeshi, katika kilima cha Hakila, kusini mwa Yeshimoni? Sasa, ee mfalme, uteremke wakati wowote unapoona vyema kufanya hivyo, sisi tutawajibika kumkabidhi kwa mfalme.”

23:21 Rut 2:20; 2Sam 2:5; 1Sam 22:8Sauli akajibu, “Bwana awabariki kwa kunifikiria. Nendeni mkafanye maandalizi zaidi. Mkajue mahali ambapo Daudi huenda mara kwa mara na nani amepata kumwona huko. Wananiambia yeye ni mwerevu sana. 23:23 Mwa 31:36Jueni kila mahali anapojificha mrudi na kunipa taarifa kamili. Kisha nitakwenda pamoja nanyi; kama atakuwa katika eneo hilo, nitamsaka miongoni mwa koo zote za Yuda.”

23:24 Yos 15:55; 1Sam 26:1; 25:2Basi wakaondoka na kwenda mpaka Zifu wakimtangulia Sauli. Naye Daudi na watu wake walikuwa katika Jangwa la Maoni, katika Araba kusini mwa Yeshimoni. Sauli na watu wake wakaanza msako, naye Daudi alipoelezwa hili, akateremka mpaka mwambani na kukaa katika Jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hili, akaenda katika Jangwa la Maoni akimfuata Daudi.

23:26 Za 17:6; 1Sam 19:12; 20:38; 2Sam 15:14; Za 31:22; 2Nya 20:12; 2Kor 1:8Sauli alikuwa akienda upande mmoja wa mlima, naye Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima, wakiharakisha kumkimbia Sauli. Wakati Sauli na majeshi yake walipokaribia kumkamata Daudi na watu wake, 23:27 Kum 32:36; 1Sam 14:6; 2Sam 22:1-51; 2Fal 19:9; Za 18:1-50; Isa 37:6-9; 59:1; Yer 15:20, 21mjumbe alikuja kwa Sauli, akisema, “Njoo haraka! Wafilisti wanaishambulia nchi.” Ndipo Sauli akarudi akaacha kumfuata Daudi na kwenda kukabiliana na Wafilisti. Ndiyo sababu wanaiita sehemu hii Sela-Hamalekothi.23:28 Sela-Hamalekothi maana yake Mwamba wa Kutengana. 23:29 1Sam 24:22; Yos 15:62; 2Nya 20:2; Wim 1:14Naye Daudi akakwea kutoka huko na kuishi katika ngome za En-Gedi.

Read More of 1 Samweli 23