1 Samweli 2:27-36, 1 Samweli 3:1-21, 1 Samweli 4:1-22 NEN

1 Samweli 2:27-36

Unabii Dhidi Ya Nyumba Ya Eli

2:27 Kum 33:1; Amu 13:6; Kut 4:14-16; 1Fal 13:1Basi mtu wa Mungu akaja kwa Eli na kumwambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Je, sikujifunua waziwazi kwa nyumba ya baba yako wakati walikuwa huko Misri chini ya Farao? 2:28 Kut 28:1; 30:7; 1Sam 22:18; 23:6-9; 30:7; Law 7:35-36; 8:7-8Nilimchagua baba yako kati ya makabila yote ya Israeli kuwa kuhani wangu, kukwea kwenye madhabahu yangu, kufukiza uvumba na kuvaa kisibau mbele yangu. Pia niliwapa nyumba ya baba yako sadaka zote zilizotolewa kwa moto na Waisraeli. 2:29 Kum 12:5; Mt 10:37Kwa nini unadharau dhabihu zangu na sadaka zile nilizoziamuru kwa ajili ya makao yangu? Kwa nini unawaheshimu wanao kuliko mimi kwa kujinenepesha wenyewe kwa kula sehemu zilizo bora za kila sadaka zinazotolewa na watu wangu wa Israeli?’

2:30 Kut 29:19; Za 50:23; 91:15; Mit 8; 17; Isa 53:3; Neh 3:6; Mal 2:9; Yer 18:10; 1Nya 15:2; Za 18:20; 91:14; Yn 5:44; 12:26; 1Pet 1:7; Hes 11:20“Kwa hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli asema: ‘Niliahidi kuwa nyumba yako na nyumba ya baba yako wangehudumu mbele zangu milele.’ Lakini sasa Bwana anasema: ‘Jambo hili na liwe mbali nami! Wale wanaoniheshimu nitawaheshimu, wale wanaonidharau mimi watadharauliwa. 2:31 1Sam 4:11-18; 22:16-20Wakati unakuja nitakapozipunguza nguvu zenu na nguvu ya nyumba ya baba yenu, ili pasiwepo mtu katika mbari yenu atakayeishi kuuona uzee 2:32 1Sam 4:3; 22:17-20; Yer 7:12-14; 1Fal 2:26-27; Zek 8:4nanyi mtaona huzuni katika makao yangu. Ingawa Israeli watafanyiwa mema, katika mbari yenu kamwe hapatakuwepo mtu atakayeishi hadi kuwa mzee. 2:33 Yer 29:32; Mal 2:12Kila mmoja wenu ambaye sitamkatilia mbali kutoka madhabahuni pangu atabakizwa tu kupofusha macho yenu kwa machozi na kuihuzunisha mioyo yenu, nao wazao wenu wote watakufa watakapokuwa wamefikia umri wa kustawi.

2:34 Kum 13:4; 1Sam 4:11; 1Fal 13:3“ ‘Kile kitakachotokea kwa wanao wawili, Hofni na Finehasi, kitakuwa ishara kwako. Wote wawili watakufa katika siku moja. 2:35 1Nya 16:39; 29:22; 2Sam 8:17; 20:25; 1Fal 2:35; 4:4; Eze 44:15-16; 1Sam 10:1; 16:13; 2Sam 2:4; 12:7; 23:1; 1Fal 1:34; Za 89:20Mimi mwenyewe nitajiinulia kuhani mwaminifu, ambaye atafanya sawasawa na kile kilichoko moyoni mwangu na akilini mwangu. Nitaifanya nyumba yake kuwa imara, naye atahudumu mbele ya mpakwa mafuta wangu daima. 2:36 Eze 44:10-14; 1Sam 3:12; 1Fal 2:27Kisha kila mmoja aliyeachwa katika mbari yenu atakuja na kusujudu mbele yake kwa ajili ya kipande cha fedha na ganda la mkate akisema, “Niteue katika baadhi ya ofisi ya ukuhani ili niweze kupata chakula.” ’ ”

Read More of 1 Samweli 2

1 Samweli 3:1-21

Bwana Amwita Samweli

3:1 1Sam 2:11; Za 74:9; Mao 2:9; Eze 7:26; Amo 8:11Kijana Samweli alihudumu mbele za Bwana chini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi.

3:2 1Sam 4:15; Mwa 27:1Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida. 3:3 Kut 25:31-38; Law 24:1-4; 1Sam 1:9; Kum 10:1-5; 1Fal 6:19; 8:1Taa ya Mungu bado ilikuwa haijazimika, na Samweli alikuwa amelala Hekaluni3:3 Hekaluni maana yake ndani ya Maskani ya Bwana. mwa Bwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako. 3:4 Mwa 22:1; Kut 3:4Kisha Bwana akamwita Samweli.

Samweli akajibu, “Mimi hapa.” Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala.

Bwana akaita tena, “Samweli!” Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.”

3:7 1Sam 2:12; Hes 12:6; Mdo 19:2; Amo 3:7Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjua Bwana. Neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.

Bwana akamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Ndipo Eli akatambua kuwa Bwana alikuwa akimwita kijana. Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake.

3:10 Kut 3:4; Za 85:8; Mdo 9:6Bwana akaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”

Kisha Samweli akasema, “Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”

3:11 2Fal 21:12; Ay 15:21; Yer 19:3Naye Bwana akamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe. 3:12 1Sam 2:27-36Wakati huo nitatimiza dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho. 3:13 1Fal 1:6; 1Sam 2:12Kwa kuwa nilimwambia kwamba ningehukumu jamaa yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua, wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa kuwazuia. 3:14 1Sam 2:25; Law 15:30-31; Isa 22:14; Hes 12:6; Yer 7:16; Ebr 10:26-31Kwa hiyo, nikaapa kuhusu nyumba ya Eli, ‘Hatia ya nyumba ya Eli kamwe haitaweza kufidiwa kwa dhabihu au sadaka.’ ”

3:15 1Sam 3:2Samweli akalala mpaka asubuhi, kisha akafungua milango ya nyumba ya Bwana. Aliogopa kumwambia Eli yale maono, lakini Eli akamwita na kumwambia, “Samweli mwanangu.”

Samweli akamjibu, “Mimi hapa.”

3:17 1Fal 22:14; Yer 23:28; 38:14; 42:4; Rut 1:17; 1:17; Mt 26:63Eli akamuuliza, “Ni nini alichokuambia? Usinifiche. Bwana na ashughulike nawe, tena kwa ukali, kama utanificha chochote alichokuambia.” 3:18 Amu 10:15; 2:16; Mwa 18:25; 1Sam 16:10-12; Isa 39:8; 1Pet 5:6Kwa hiyo Samweli akamwambia kila kitu, bila kumficha chochote. Ndipo Eli akasema, “Yeye ni Bwana; na afanye lile lililo jema machoni pake!”

3:19 Mwa 21:22; Hes 14:43; Amu 13:24; 1Sam 9:6; Mwa 39:2Bwana alikuwa pamoja na Samweli alipokuwa akikua, na hakuacha hata moja ya maneno yake lianguke chini. 3:20 Amu 20:1; Kum 18:22; Eze 33:33; Amu 20:1Nao Israeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba wakatambua kuwa Samweli amethibitishwa kuwa nabii wa Bwana. 3:21 Mwa 12:7; Hes 12:6; Amo 3:7Bwana akaendelea kutokea huko Shilo, na huko kujidhihirisha kwa Samweli kwa njia ya neno lake.

Read More of 1 Samweli 3

1 Samweli 4:1-22

4:1 1Sam 5:1; 7:12; 29:1; Yos 12:18; 1Fal 20:26Nalo neno la Samweli likaja kwa Israeli yote.

Wafilisti Wateka Sanduku La Mungu

Basi Waisraeli walitoka kwenda kupigana dhidi ya Wafilisti. Waisraeli wakapiga kambi huko Ebenezeri, nao Wafilisti wakapiga kambi huko Afeki. Wafilisti wakapanga safu za majeshi yao kupambana na Israeli, wakati vita vilipoenea, Israeli wakashindwa na Wafilisti, ambao waliwaua askari wa Israeli wapatao 4,000 kwenye uwanja wa vita. 4:3 Yos 6:7; 7:7; 18:1; 1Sam 2:32; 2Nya 13:8Askari waliporudi kambini, wazee wa Israeli wakawauliza, “Kwa nini Bwana ameruhusu leo tushindwe mbele ya Wafilisti? Tuleteni Sanduku la Agano la Bwana kutoka Shilo, ili lipate kwenda pamoja nasi, na kutuokoa kutoka mikono ya adui zetu.”

4:4 Mwa 3:24; Kut 25:23; 2Sam 6:2; Za 80:1; Hes 7:89Hivyo wakawatuma watu huko Shilo, nao wakalichukua Sanduku la Agano la Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliyekaa kwenye kiti chake cha enzi kati ya makerubi. Nao wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, walikuwako huko pamoja na Sanduku la Agano la Mungu.

4:5 Yos 6:5-10Wakati Sanduku la Agano la Bwana lilikuja kambini, Waisraeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu hata ardhi ikatikisika. 4:6 Mwa 14:13Wafilisti waliposikia makelele wakauliza, “Ni nini makelele haya yote katika kambi ya Waebrania?”

Walipofahamu kuwa Sanduku la Bwana limekuja kambini, 4:7 Kut 15:14Wafilisti wakaogopa, wakasema, “Mungu amekuja kambini, ole wetu. Halijatokea jambo kama hili tangu hapo. 4:8 Kut 12:30; 1Sam 5:12; Ufu 11:6Ole wetu! Ni nani atakayetuokoa kutoka mikononi mwa miungu hii yenye nguvu? Ni miungu ile iliyowapiga Wamisri kwa mapigo ya aina zote huko jangwani. 4:9 Amu 13:1; 1Kor 16:13; 2Sam 10:12; 1Nya 19:13Tuweni hodari, enyi Wafilisti! Tuweni wanaume, la sivyo mtakuwa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa kwenu. Kuweni wanaume, mpigane!”

4:10 2Sam 18:17; 2Fal 14:12; Kum 28:25; Law 26:17Basi Wafilisti wakapigana, nao Waisraeli wakashindwa na kila mtu akakimbilia hemani mwake. Mauaji yalikuwa makubwa sana, Israeli wakapoteza askari 30,000 waendao kwa miguu. 4:11 Za 78:64; Yer 7:12; 1Sam 2:32Sanduku la Mungu likatekwa, na hao wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, wakauawa.

Kifo Cha Eli

4:12 Eze 24:26; 33:21; Yos 7:6; Neh 9:1; 2Sam 1:2; Ay 2:12Siku ile ile mtu mmoja wa kabila la Benyamini akakimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na kwenda Shilo, nguo zake zikiwa zimeraruka na akiwa na mavumbi kichwani mwake. 4:13 1Sam 1:9Alipofika, Eli alikuwa ameketi juu ya kiti chake kando ya barabara akiangalia, kwa sababu moyo wake ulikuwa na hofu kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kueleza kilichokuwa kimetokea, mji wote ukalia.

Eli akasikia kelele za kilio, naye akauliza, “Ni nini maana ya makelele haya?”

Yule mtu akafanya haraka kwenda kwa Eli, wakati huu Eli alikuwa na miaka tisini na minane nayo macho yake yalikuwa yamepofuka na hakuweza kuona. 4:16 2Sam 1:4Akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi, nimekimbia kutoka huko leo hii.”

Eli akamuuliza, “Je, mwanangu, ni nini kimetokea huko?”

4:17 1Sam 22:18; Za 78:64; 78:61Yule mtu aliyeleta habari akajibu, “Israeli amekimbia mbele ya Wafilisti, nalo jeshi limepata hasara kubwa. Pia wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa, na Sanduku la Mungu limetekwa.”

4:18 Amu 2:16; 16:31; 1Sam 2:31Mara alipotaja Sanduku la Mungu, Eli alianguka kutoka kwenye kiti chake kwa nyuma kando ya lango. Shingo yake ikavunjika naye akafa, kwa kuwa alikuwa mzee tena mzito. Alikuwa amewaongoza Israeli kwa miaka arobaini.

Mkwewe, mke wa Finehasi, alikuwa mjamzito na karibu wakati wa kujifungua. Aliposikia habari kwamba Sanduku la Mungu limetekwa na ya kuwa baba mkwe wake na mumewe wamekufa, akapata utungu naye akajifungua lakini akazidiwa na utungu. 4:20 Mwa 35:17Alipokuwa akifa, wanawake waliokuwa wanamhudumia wakamwambia, “Usikate tamaa, umemzaa mwana.” Lakini hakujibu wala kuweka maanani.

4:21 Mwa 35:18; Kut 24:16; Za 106:26; Yer 2:11; Eze 1:28; 9:3; 10:18Alimwita yule mtoto Ikabodi,4:21 Ikabodi maana yake Utukufu wa Bwana umeondoka. akisema, “Utukufu umeondoka katika Israeli,” kwa sababu ya kutekwa kwa Sanduku la Mungu na vifo vya baba mkwe na mumewe. 4:22 Kut 24:16; Za 78:61; Yer 7:12Akasema, “Utukufu umeondoka katika Israeli, kwa kuwa Sanduku la Mungu limetekwa.”

Read More of 1 Samweli 4