1 Samweli 16:1-23, 1 Samweli 17:1-37 NEN

1 Samweli 16:1-23

Samweli Anamtia Daudi Mafuta

16:1 1Sam 8:6; 15:35; 13:14; 10:1; Rut 4:17; 2Sam 5:2; 7:8; 1Fal 8:16; 1Nya 12:23; Za 78:70; Mdo 13:22; 1Sam 9; 16Bwana akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli mpaka lini, maadamu nimemkataa asiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli? Jaza pembe yako mafuta, ushike njia uende; ninakutuma kwa Yese huko Bethlehemu. Nimemchagua mmoja wa wanawe kuwa mfalme.”

16:2 1Sam 20:29Lakini Samweli akasema, “Nitakwendaje? Sauli atasikia juu ya jambo hili na ataniua.”

Bwana akamwambia, “Chukua mtamba wa ngʼombe na useme, ‘Nimekuja kumtolea Bwana dhabihu.’ 16:3 Kut 4:15; Kum 17:15; 1Sam 9:16Mwalike Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakalofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakayekuonyesha.”

16:4 Mwa 48:7; Lk 2:4; 1Sam 21:1; 1Fal 2; 13; 2Fal 9:17; 2Sam 6:9; 1Fal 17:18; Hos 6:5; 11:10; Lk 18:11Samweli akafanya kile Bwana alichosema. Alipofika Bethlehemu, wazee wa mji wakatetemeka walipomlaki. Wakauliza, “Je, umekuja kwa amani?”

16:5 Kut 19:10, 22Samweli akajibu, “Ndiyo, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu. Jiwekeni wakfu na mje kwenye dhabihu pamoja nami.” Ndipo akamweka Yese wakfu pamoja na wanawe na kuwaalika kwenye dhabihu.

16:6 1Sam 17:13; 1Nya 2:13; 1Fal 12:26Walipofika, Samweli akamwona Eliabu, naye akafikiri, “Hakika mpakwa mafuta wa Bwana anasimama hapa mbele za Bwana.”

16:7 Za 147:10; 1Sam 2:3; 2Sam 7:20; Za 44:21; 139:23; Ufu 2:23; Isa 55:8; 55:8; 2Kor 10:7; 1Fal 8:39; 1Nya 29:8; Yer 11:20; 17:10Lakini Bwana akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. Bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana hutazama moyoni.”

16:8 1Sam 17:13Kisha Yese akamwita Abinadabu na kumpitisha mbele ya Samweli. Lakini Samweli akasema, “Hata huyu Bwana hakumchagua.” 16:9 1Sam 17:13; 2Sam 13:3; 21:21Kisha Yese akampitisha Shama, lakini Samweli akasema, “Wala huyu Bwana hakumchagua.” Yese alikuwa na wana saba aliowapitisha mbele ya Samweli, lakini Samweli akamwambia, “Bwana hajawachagua hawa.” 16:11 1Sam 17:12; Mwa 37:2; 2Sam 7:8; Za 78:70Hivyo akamuuliza Yese, “Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?”

Yese akajibu, “Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo.”

Samweli akasema, “Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike.”

16:12 1Sam 9:17; Mwa 39:6; 1Sam 17:42; Wim 5:10Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.

Ndipo Bwana akasema, “Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye.”

16:13 1Sam 2:35; 2Sam 22:51; 1Sam 18; 12; 11:6; Hes 27:18; Amu 11:29; 1Sam 6:9-10Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.

Daudi Katika Utumishi Kwa Sauli

16:14 Amu 16:20; 9:23; 1Sam 18; 10; 2Sam 7:15; 1Sam 19:9; Isa 19:14; Za 51:11Basi Roho wa Bwana alikuwa ameondoka kwa Sauli, nayo roho mbaya ikaachiwa nafasi na Bwana ili imtese.

Watumishi wa Sauli wakamwambia, “Angalia, roho mbaya imeachiwa nafasi na Bwana nayo inakutesa. 16:16 1Sam 10:5-6; 2Nya 29:26-27; 2Fal 3:15; Za 49:4Basi bwana wetu na aamuru watumishi wake walioko hapa kutafuta mtu ambaye anaweza kupiga kinubi. Atakipiga kinubi wakati roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ikujiapo, nawe utajisikia vizuri.”

Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Mtafuteni mtu apigaye kinubi vizuri mkamlete kwangu.”

16:18 Rut 4:17; 2Sam 17:8; Mwa 39:2; 1Sam 17:37; 20:13; 1Nya 22:11; Mt 1:23Mmoja wa watumishi wake akajibu, “Nimemwona mwana wa Yese Mbethlehemu ambaye anajua kupiga kinubi. Yeye ni mtu hodari na shujaa wa vita. Ni mwenye busara katika kunena, mtu mzuri wa umbo. Bwana yu pamoja naye.”

16:19 1Sam 17:15Ndipo Sauli akatuma wajumbe kwa Yese na kumwambia, “Nitumie mwanao Daudi, ambaye anachunga kondoo.” 16:20 Mwa 32:13; 1Sam 10:4; Mit 18:16Kwa hiyo Yese akamchukua punda aliyepakizwa mikate, kiriba cha divai na mwana-mbuzi, na kuvipeleka vitu hivyo kwa Sauli pamoja na Daudi mwanawe.

16:21 Mwa 41:46; Mit 22:29; 1Fal 10:8; Mit 22:29Daudi akafika kwa Sauli na kuingia kwenye kazi yake. Sauli akampenda sana, naye Daudi akawa mmoja wa wabeba silaha wake. Basi Sauli akatuma ujumbe kwa Yese, akisema, “Mruhusu Daudi abaki katika utumishi wangu, kwa kuwa ninapendezwa naye.”

16:23 Amu 9:23Kila mara roho mbaya iliyoachiwa nafasi na Mungu ilipomjia Sauli, Daudi alichukua kinubi chake na kupiga. Ndipo Sauli angetulizwa na kujisikia vizuri, nayo ile roho mbaya ingemwacha.

Read More of 1 Samweli 16

1 Samweli 17:1-37

Daudi Na Goliathi

17:1 1Sam 13:5; Yos 15:35; 2Nya 28:18; Yos 10:10, 11Wakati huu Wafilisti wakakusanya majeshi yao kwa ajili ya vita, nao wakakusanyika huko Soko katika Yuda. Wakapiga kambi huko Efes-Damimu, kati ya Soko na Azeka. 17:2 1Sam 21:9Sauli na Waisraeli wakakusanyika na kupiga kambi katika Bonde la Ela na kupanga jeshi ili kupigana vita na Wafilisti. Wafilisti wakawa katika kilima kimoja na Waisraeli katika kilima kingine, hilo bonde likiwa kati yao.

17:4 1Sam 21:9; Yos 11:21-22; 2Sam 21:19; 1Nya 20:5; 8:13; 18:1; 2Nya 26:6; Amo 6:2Shujaa aliyeitwa Goliathi, aliyetoka Gathi, akajitokeza kutoka kambi ya Wafilisti. Alikuwa na urefu dhiraa sita na shibiri moja.17:4 Dhiraa sita na shibiri moja ni sawa na mita 3, au futi 9 na inchi 8. Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani mwake, na alivaa dirii ya shaba kifuani mwake yenye uzito wa shekeli elfu tano.17:5 Shekeli 15,000 ni sawa na kilo 50. 17:6 1Sam 18:10Miguuni mwake alivaa mabamba ya shaba, na alikuwa na mkuki wa shaba mgongoni mwake. 17:7 2Sam 21:19; 1Nya 11:23; 20:5Mpini wa huo mkuki ulikuwa kama mti wa mfumaji, na ncha ya chuma yake ilikuwa na uzito wa shekeli mia sita.17:7 Shekeli 600 ni sawa na kilo 7. Mbeba ngao wake alitangulia mbele yake.

17:8 2Sam 2:12-17; 1Sam 8:17; 1Nya 21:3Goliathi alisimama na kuwapigia kelele majeshi ya Israeli, akisema, “Kwa nini mmetoka kupanga vita? Je, mimi si Mfilisti, na ninyi ni watumishi wa Sauli? Chagueni mtu na anishukie mimi. 17:9 1Sam 11:1Kama anaweza kupigana nami na kuniua, tutakuwa chini yenu; lakini kama nikimshinda na kumuua, ninyi mtakuwa chini yetu na mtatutumikia.” 17:10 2Sam 21:21; Hes 23:7-8; Neh 2:19Kisha yule Mfilisti akasema, “Siku hii ya leo nayatukana majeshi ya Israeli! Nipeni mtu tupigane.” Kwa kusikia maneno ya Wafilisti, Sauli na Waisraeli wote wakafadhaika na kuogopa.

17:12 Mwa 35:16; 48:7; Za 132:6; Rut 4:17, 22; 1Sam 16; 11; Mwa 35:19; 1Sam 16:10, 11; 1Nya 2:13Basi Daudi alikuwa mwana wa Mwefrathi jina lake Yese aliyekuwa ametoka Bethlehemu ya Yuda. Yese alikuwa na wana wanane, naye wakati wa Sauli alikuwa mzee tena wa umri mkubwa. 17:13 1Sam 16:6-9; 1Nya 2:13Wana wakubwa watatu wa Yese walikuwa wamefuatana na Sauli vitani: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Eliabu, wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama. Daudi ndiye alikuwa mdogo wa wote. Hao wakubwa watatu wakamfuata Sauli, 17:15 1Sam 16:19; Mwa 37:2lakini Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili kuchunga kondoo wa baba yake huko Bethlehemu.

Kwa siku arobaini huyo Mfilisti alikuwa akija mbele kila siku asubuhi na jioni na kujionyesha.

17:17 Mwa 37:14Wakati huo Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Chukua hii efa17:17 Efa moja ni sawa na kilo 22. ya bisi na hii mikate kumi kwa ajili ya ndugu zako uwapelekee upesi kambini mwao. 17:18 Law 19:36; 23:14; 1Sam 25:18Chukua pamoja na hizi jibini kumi kwa jemadari wa kikosi chao. Ujue hali ya ndugu zako na uniletee taarifa za uhakika kutoka kwao. Wao wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli huko kwenye Bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti.”

Asubuhi na mapema Daudi akaondoka, akaliacha kundi la kondoo pamoja na mchungaji, akapakia vitu vile na kuondoka, kama vile Yese alivyokuwa amemwagiza. Akafika kambini wakati jeshi lilikuwa likitoka kwenda kwenye sehemu yake ya kupigania, huku wakipiga kelele za vita. Israeli na Wafilisti walikuwa wakipanga safu zao wakitazamana. 17:22 Mwa 37:14Daudi akaacha vile vitu vyake kwa mtunza vifaa, akakimbilia katika safu za vita na kuwasalimu ndugu zake. 17:23 Mwa 43:27; Amu 18:15Alipokuwa akisema nao, Goliathi, yule Mfilisti shujaa kutoka Gathi, akajitokeza mbele ya safu zake na kupiga ile kelele yake ya kawaida ya matukano, naye Daudi akayasikia. Waisraeli walipomwona yule mtu, wote wakamkimbia kwa woga mkuu.

17:25 Yos 1:11; 15:16Basi Waisraeli walikuwa wakisema, “Je, mnaona jinsi mtu huyu anavyoendelea kujitokeza. Hujitokeza ili kutukana Israeli. Mfalme atatoa utajiri mwingi kwa yule mtu atakayemuua. Pia atamwoza binti yake na atasamehe jamaa ya baba yake kulipa kodi katika Israeli.”

17:26 1Sam 18:17; 8:15; Yos 15:16; Kum 5:26; Yer 10:10Daudi akauliza watu waliokuwa wamesimama karibu naye, “Je, atafanyiwa nini mtu atakayemuua huyu Mfilisti na kuondoa aibu hii katika Israeli? Ni nani huyu Mfilisti asiyetahiriwa hata atukane majeshi ya Mungu aliye hai?”

Wakarudia yale yaliyokuwa yamesemwa na kumwambia kuwa, “Hili ndilo atakalotendewa mtu yule atakayemuua.”

17:28 Mwa 27:41; Mit 18:19; Mwa 37:8, 11; Mt 10:38; Mwa 37:4; Mhu 4:4; Mk 3:21Eliabu nduguye mkubwa Daudi alipomsikia akizungumza na watu hasira ikawaka juu yake akamuuliza, “Kwa nini umeteremka kuja hapa? Nao wale kondoo wachache kule nyikani umewaacha na nani? Ninajua jinsi ulivyo na kiburi na jinsi moyo wako ulivyo mwovu; umekuja hapa kutazama vita tu.”

17:29 Mit 15:1Daudi akasema, “Sasa nimefanya nini? Je, siwezi hata kuongea.” Daudi akamgeukia mtu mwingine na kumuuliza jambo lilo hilo, nao watu wakamjibu vilevile kama mwanzo. Lile Daudi alilosema likasikiwa na kuelezwa kwa Sauli, naye Sauli akatuma aitwe.

17:32 Kum 20:3; Za 18:45; Isa 7:4; Yer 4:9; 38:4; Dan 11:30; Hes 13:30; 14:9; Ebr 12:12; Isa 30:3Daudi akamwambia Sauli, “Mtu yeyote asife moyo kwa habari ya huyu Mfilisti; mtumishi wako atakwenda kupigana naye.”

17:33 Hes 13:31; Kum 9:2Sauli akamjibu Daudi, “Wewe hutaweza kwenda kupigana dhidi ya huyu Mfilisti; wewe ni kijana tu, naye amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake.”

17:34 Ay 10:16; Isa 31:4; Yer 49:19; Hos 13:8; Amo 3:12Lakini Daudi akamwambia Sauli, “Mtumishi wako amekuwa akichunga kondoo wa baba yake. Wakati simba au dubu alikuja na kuchukua kondoo kutoka kundi, 17:35 Amu 14:6nilifuatia, nikampiga na nikampokonya kondoo kwenye kinywa chake. Aliponigeukia, nilimkamata nywele zake, nikampiga na kumuua. 17:36 1Nya 11:22Mtumishi wako ameshaua simba na dubu pia; huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wa hao, kwa sababu ameyatukana majeshi ya Mungu aliye hai. 17:37 2Kor 1:10; 2Tim 4:17; 1Sam 16:18; 18:12; 1Nya 22:11, 16; 1Sam 7:12; Za 18:16, 17Bwana ambaye aliniokoa toka katika makucha ya simba na makucha ya dubu ataniokoa kutoka mikono ya huyu Mfilisti.”

Sauli akamwambia Daudi, “Nenda, naye Bwana na awe pamoja nawe.”

Read More of 1 Samweli 17