1 Samweli 14:24-52, 1 Samweli 15:1-35 NEN

1 Samweli 14:24-52

Yonathani Ala Asali

14:24 Yos 6:26; Law 27:29; Hes 21:2; Kum 27:15-26; Amu 11:30; 21:1-5; Mit 11:9Basi watu wa Israeli walikuwa katika dhiki siku ile, kwa sababu Sauli alikuwa amewafunga watu kwa kiapo, akisema, “Alaaniwe mtu yeyote ambaye atakula chakula kabla ya jioni, kabla sijalipiza kisasi juu ya adui zangu!” Kwa hiyo hakuna mtu yeyote katika jeshi aliyeonja chakula.

14:25 Kum 9:28; Mt 3:5; Kut 3:8; Hes 13:27Jeshi lote liliingia mwituni, na huko kulikuwepo na asali ardhini. Walipoingia mwituni, wakaona asali ikitiririka, hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyetia mkono wake kinywani, kwa sababu waliogopa kiapo. 14:27 Za 19:10; Mit 16:24; 24:13Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kuwa baba yake alikuwa amewafunga watu kwa kiapo, hivyo akainyoosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya katika sega la asali. Akainua mkono wake na kuutia kinywani mwake, nayo macho yake yakawa maangavu. Kisha mmoja wa askari wake akamwambia, “Baba yako alilifunga jeshi kwa kiapo kikali, akisema, ‘Alaaniwe mtu yeyote alaye chakula leo!’ Ndiyo sababu watu wanalegea.”

14:29 Yos 7:25; 1Fal 18:18Yonathani akasema, “Baba yangu ameitaabisha nchi. Ona jinsi nilivyopata nguvu mpya nilipoonja asali hii kidogo. Ingekuwa bora zaidi mara ngapi kama watu wangalikula leo baadhi ya nyara walizoteka kutoka kwa adui zao. Je, mauaji ya Wafilisti yasingekuwa makubwa zaidi?”

14:31 Yos 10:12Siku ile baada ya Waisraeli kuwaua Wafilisti kutoka Mikmashi mpaka Aiyaloni, walikuwa wamechoka. 14:32 1Sam 15:19; Es 9:10; Mwa 9:4; Law 3:17; Kum 12:16Watu wakarukia zile nyara, wakichukua kondoo, ngʼombe na ndama, wakawachinja hapo juu ya nchi na kuwala, pamoja na damu. 14:33 Mwa 9:4Kisha mtu mmoja akamwambia Sauli, “Tazama, watu wanatenda dhambi dhidi ya Bwana kwa kula nyama yenye damu.”

Akasema, “Mmevunja uaminifu. Livingirisheni jiwe kubwa hapa mara moja.” 14:34 Law 19:26Kisha Sauli akasema, “Nendeni miongoni mwa watu, mwaambie, ‘Kila mmoja wenu aniletee ngʼombe wake na kondoo, mwachinjie hapa na mle. Msitende dhambi dhidi ya Bwana kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ”

Hivyo kila mmoja akaleta ngʼombe wake jioni ile na kumchinja hapo. 14:35 1Sam 7:17; Amu 21:4; 2Sam 24:25Ndipo Sauli akamjengea Bwana madhabahu, na ndiyo ilivyokuwa mara yake ya kwanza kujenga madhabahu.

14:36 Mwa 25:22; Amu 18:5; Mal 2:7; Yak 4:8Sauli akasema, “Tuteremke tufuatie Wafilisti usiku na kuwateka nyara mpaka mapambazuko, nasi tusiache hata mmoja wao hai.”

Wakajibu, “Fanya lolote lile uonalo jema zaidi kwako.”

Lakini kuhani akasema, “Tuulize kwa Mungu mahali hapa.”

14:37 1Sam 28:6, 15; 2Sam 22:42; Za 18:41Basi Sauli akamuuliza Mungu, akisema, “Je, niteremke kuwafuatia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwa Israeli?” Lakini Mungu hakumjibu siku ile.

14:38 Yos 7:11; 1Sam 10:19Kwa hiyo Sauli akasema, “Njooni hapa, ninyi nyote ambao ni viongozi wa jeshi, na tutafute ni dhambi gani imefanywa leo. 14:39 Hes 14:21; 2Sam 12:5; Ay 19:25; Za 18:46; 42:2; Yos 7:15Kwa hakika kama Bwana aiokoaye Israeli aishivyo, hata kama itakuwa juu ya mwana wangu Yonathani, ni lazima afe.” Lakini hakuna mtu yeyote aliyesema neno.

Kisha Sauli akawaambia Waisraeli wote, “Ninyi simameni huko; mimi na mwanangu Yonathani tutasimama hapa.”

Watu wakajibu, “Fanya lile unaloona jema zaidi kwako.”

14:41 Mdo 1:24; Mit 16:33; Yos 7:16; 1Sam 10:20-21Kisha Sauli akamwomba Bwana, Mungu wa Israeli, akisema, “Nipe jibu lililo sawa.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama. 14:42 Yon 1:7Sauli akasema, “Pigeni kura kati yangu na mwanangu Yonathani.” Kura ikamwangukia Yonathani.

14:43 Yos 7:19Basi Sauli akamwambia Yonathani, “Niambie ni nini ulichokifanya.”

Hivyo Yonathani akamwambia, “Nilionja tu asali kidogo kwa ncha ya fimbo yangu. Je, sasa ni lazima nife?”

14:44 Rut 1:17Sauli akasema, “Mungu na anishughulikie kwa ukali zaidi kama wewe Yonathani hutakufa.”

14:45 1Fal 1:52; Mt 10:30; 2Sam 14:11; Lk 21:18; Isa 13:3; 2Kor 6:1Lakini watu wakamwambia Sauli, “Je, Yonathani atakufa, yeye ambaye ameleta wokovu huu mkubwa Israeli? Hasha! Hakika kama Bwana aishivyo, hakuna hata unywele wa kichwa chake utakaoanguka juu ya ardhi, kwa kuwa alifanya jambo hili leo kwa msaada wa Mungu.” Basi watu wakamwokoa Yonathani, wala hakuuawa.

Kisha Sauli akaacha kuwafuata Wafilisti, nao wakajiondoa na kurudi katika nchi yao.

14:47 Mwa 19:37-38; 2Sam 12:31; 8:3; 10:6; 23:36Baada ya Sauli kujitwalia utawala katika Israeli, alipigana dhidi ya adui zake kila upande: Moabu, Waamoni, Edomu, wafalme wa Soba, na Wafilisti. Popote alipogeukia, aliwashinda. 14:48 Mwa 36:12; Hes 13:29; Amu 3:13; 1Sam 15:2, 7; 27:8; 28:18; 30:13; 2Sam 1:13; 1Nya 4:43Akapigana kishujaa na kuwashinda Waamaleki, akiikomboa Israeli kutoka mikono ya wale waliokuwa wamewateka nyara.

Jamaa Ya Sauli

14:49 1Sam 31:2; 1Nya 8:33; Mwa 29:26; 1Sam 18:17-20Wana wa Sauli walikuwa Yonathani, Ishvi na Malki-Shua. Jina la binti yake mkubwa lilikuwa Merabu, naye mdogo aliitwa Mikali. 14:50 2Sam 2:8; 3:6; 1Fal 2:5; 1Sam 10:14Jina la mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu binti wa Ahimaasi. Jina la jemadari wa jeshi la Sauli aliitwa Abneri mwana wa Neri, naye Neri alikuwa babaye mdogo Sauli. 14:51 1Sam 9:1Babaye Sauli yaani, Kishi na Neri baba yake Abneri walikuwa wana wa Abieli.

14:52 1Sam 8:11Siku zote za utawala wa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wowote Sauli alimwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.

Read More of 1 Samweli 14

1 Samweli 15:1-35

Bwana Anamkataa Sauli Asiwe Mfalme

15:1 1Sam 9:16Samweli akamwambia Sauli, “Mimi ndiye ambaye Bwana alinituma nikutie mafuta uwe mfalme juu ya watu wake Israeli, basi sasa sikiliza ujumbe kutoka kwa Bwana. 15:2 Mwa 14:7; 1Sam 14:48; 2Sam 1; 8; Kut 17:8-14; Kum 25:17Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipanda kutoka Misri. 15:3 Mwa 14:23; Yos 6:17; 1Sam 22:17; 22:19; 27:9; 28:8; Es 3:13; 9:5; Law 27:28; Kut 20:5; Isa 14:21; Mwa 3:17; Yos 7:24Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ngʼombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”

15:4 Yos 15:24Ndipo Sauli akawaita watu na kuwapanga huko Telaimu, askari wa miguu 200,000 pamoja na watu 10,000 kutoka Yuda. Sauli akaenda katika mji wa Amaleki na kuwavizia bondeni. 15:6 Mwa 15:19; Hes 24:22; Amu 1:16; 1Sam 30:29; Mwa 18:25; 19:12; Mdo 2:40; Ufu 18:4; Kut 18:10; Hes 10:29Kisha akawaambia Wakeni, “Ondokeni, waacheni Waamaleki ili nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao, kwa kuwa ninyi mliwatendea mema Waisraeli wote wakati walipanda kutoka Misri.” Basi Wakeni wakaondoka, wakawaacha Waamaleki.

15:7 1Sam 14:48; Mwa 16:7; 25:17-18; Kut 15:22Ndipo Sauli akawashambulia Waamaleki toka Havila mpaka Shuri, hadi mashariki ya Misri. 15:8 Kut 17:8-16; Hes 24:7; Yos 8:23; 1Fal 20:34; Es 3:1; 1Sam 30:1Akamchukua Agagi, mfalme wa Waamaleki akiwa hai, nao watu wake wote akawaangamiza kabisa kwa upanga. 15:9 Mit 15:27; 1Tim 6:10Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ngʼombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

Kisha neno la Bwana likamjia Samweli kusema: 15:11 Mwa 6:6; Kut 32:14; Yos 22:16; Ay 21:14; 34:27; Za 28:5; Isa 5:12; 53:6; Yer 48:10; Eze 18:24; 1Sam 8:6; Yos 22:16; 1Fal 9:6; Za 36:3; Sef 1:6; Mt 24:13“Ninasikitika kwamba nimemfanya Sauli kuwa mfalme, kwa sababu ameacha kunifuata mimi na hakutimiza maagizo yangu.” Samweli akafadhaika, naye akamlilia Bwana usiku ule wote.

15:12 Yos 15:55; Hes 32:42Asubuhi na mapema Samweli akaamka kwenda kukutana na Sauli, lakini akaambiwa, “Sauli amekwenda Karmeli. Huko amesimamisha mnara kwa heshima yake mwenyewe naye ameendelea na kuteremkia Gilgali.”

15:13 Mwa 14:19; Amu 17:2; Rut 3:2; Lk 8:11Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, “Bwana akubariki! Nimetimiza yale Bwana aliniagiza.”

Lakini Samweli akasema, “Nini basi huu mlio wa kondoo masikioni mwangu? Huu mlio wa ngʼombe ninaousikia ni kitu gani?”

15:15 Mwa 3:12; Mit 28:13Sauli akajibu, “Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ngʼombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote.”

Samweli akamwambia Sauli, “Ngoja! Nami nitakuambia lile Bwana aliloniambia usiku huu.”

Sauli akajibu, “Niambie.”

15:17 Kut 3:11; 1Sam 9:21Samweli akamwambia, “Ingawa zamani ulijiona mdogo machoni pako mwenyewe, Je, hukuwa kiongozi wa kabila za Israeli? Bwana alikutia mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli. Naye akakutuma kwa kazi maalum, akisema, ‘Nenda ukaangamize kabisa wale watu waovu, wale Waamaleki, upigane nao vita mpaka utakapowaangamiza kabisa.’ 15:19 Mwa 14:23; 1Sam 14:32Kwa nini hukumtii Bwana? Kwa nini ulivamia nyara na kufanya uovu machoni pa Bwana?”

15:20 1Sam 28:18Sauli akasema, “Lakini nilimtii Bwana. Nilikamilisha ile kazi ambayo Bwana alinituma. Niliwaangamiza Waamaleki kabisa na kumleta Agagi mfalme wao. Askari walichukua kondoo na ngʼombe kutoka kwenye nyara, zile ambazo ni nzuri sana zimewekwa wakfu kwa Mungu, ili zitolewe dhabihu kwa Bwana Mungu wako huko Gilgali.”

15:22 Za 40:6-8; 51:16; Mit 21:3; Isa 1:11-15; Yer 7:22; Hos 6:6; Amo 5:25; Mik 6:6-8; Mk 12:33; Mt 12:7; Ebr 10:6; Kut 19:5; Mhu 5:1; Yer 7:23; Hos 6:6; Mt 5:24; 9:13Lakini Samweli akajibu:

“Je, Bwana anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

kama vile kuitii sauti ya Bwana?

Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu,

nako kusikia ni bora

kuliko mafuta ya kondoo dume.

15:23 Kum 18:10; 1Sam 13:13Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

Kwa sababu umelikataa neno la Bwana,

naye amekukataa wewe

kuendelea kuwa mfalme.”

15:24 Kut 9:27; Hes 22:24; Za 51:4; 1Sam 13:13; Mit 29:25; Isa 51:12-13; Yer 42:11; 2Sam 12:13; Mt 27:4; Ay 31:34; Mit 29:25; Ufu 21:8Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya Bwana na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka. 15:25 Kut 10:17Sasa ninakusihi usamehe dhambi yangu, nawe urudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu Bwana.”

15:26 Hes 15:31; 1Sam 13:14; 1Fal 14:10Lakini Samweli akamwambia, “Sitarudi pamoja nawe. Umelikataa neno la Bwana, naye Bwana amekukataa wewe, usiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli!”

15:27 1Sam 28:14; 1Fal 11:11; 14:8; 2Fal 17:21Samweli alipogeuka ili aondoke, Sauli akangʼangʼania pindo la joho lake, nalo likararuka. 15:28 1Sam 28:17; 13:14; 2Sam 6:21; 7:15; 1Fal 11:31Samweli akamwambia, “Bwana ameurarua ufalme wa Israeli kutoka kwako leo, naye ameutia kwa mmoja wa majirani zako, aliye bora kuliko wewe. 15:29 Tit 1:2; Hes 23:19; Ebr 7:21; 1Nya 29:11; Eze 24:14Yeye aliye Utukufu wa Israeli hasemi uongo wala hana kigeugeu; kwa kuwa yeye si mwanadamu, hata abadili nia yake.”

15:30 Hes 22:34; Isa 29:13; Yn 12:43; 12:41-43; Rum 2:28-29Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli; rudi pamoja nami, ili nipate kumwabudu Bwana Mungu wako.” Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabudu Bwana.

Ndipo Samweli akasema, “Niletee Agagi mfalme wa Waamaleki.”

Agagi akaja kwake kwa ujasiri, akifikiri, “Hakika uchungu wa mauti umepita.”

15:33 Es 9:7-10; Yer 18:21; Mwa 9:6; Kut 17:11; Amu 1:7; Yak 2:13; 1Fal 18:40Lakini Samweli akasema,

“Kama upanga wako ulivyofanya wanawake

kufiwa na watoto wao,

ndivyo mama yako atakavyokuwa

hana mtoto miongoni mwa wanawake.”

Naye Samweli akamuua Agagi mbele za Bwana huko Gilgali.

15:34 1Sam 7:17; Amu 19:14; 1Sam 10:5; 11:4Kisha Samweli akaenda Rama, lakini Sauli akapanda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. 15:35 1Sam 19:24; 16:1; Mwa 6:6Hadi siku Samweli alipofariki hakwenda kumwona Sauli tena, ingawa Samweli alimwombolezea. Naye Bwana alihuzunika kwamba alimfanya Sauli kuwa mfalme juu ya Israeli.

Read More of 1 Samweli 15