1 Samweli 13:1-23, 1 Samweli 14:1-23 NEN

1 Samweli 13:1-23

Samweli Amkemea Sauli

Sauli alikuwa na miaka thelathini, alipokuwa mfalme, akatawala Israeli miaka arobaini na miwili.

13:2 Neh 11:31; Isa 10:28; Amu 19:14; 1Sam 10:26Sauli alichagua watu 3,000 kutoka Israeli; miongoni mwa hao watu 2,000 walikuwa pamoja naye huko Mikmashi na katika nchi ya vilima ya Betheli, nao watu 1,000 walikuwa pamoja na Yonathani huko Gibea ya Benyamini. Watu waliosalia aliwarudisha nyumbani mwao.

13:3 1Sam 10:5; Yos 18:24; Law 25:6; Amu 3:27Yonathani akashambulia ngome ya Wafilisti huko Geba, nao Wafilisti wakapata habari hizo. Kisha Sauli akaamuru tarumbeta ipigwe nchi yote na kusema, “Waebrania na wasikie!” 13:4 Mwa 34:30Hivyo Israeli wote wakasikia habari kwamba: “Sauli ameshambulia ngome ya Wafilisti, nao sasa Israeli wamekuwa harufu mbaya kwa Wafilisti.” Basi watu waliitwa kuungana na Sauli huko Gilgali.

13:5 1Sam 17:1; Yos 11:4; Ufu 20:8; Yos 7:2Wafilisti wakakusanyika ili kupigana na Israeli, wakiwa na magari ya vita 3,000, waendesha magari ya vita 6,000 na askari wa miguu wengi kama mchanga wa ufuoni mwa bahari. Walipanda na kupiga kambi huko Mikmashi, mashariki ya Beth-Aveni. 13:6 1Sam 14:11, 22; Amu 6:2; Eze 33:27Watu wa Israeli walipoona kuwa hali yao ni ya hatari na kuwa jeshi lao limesongwa sana, wakajificha katika mapango na katika vichaka, katikati ya miamba, kwenye mashimo na kwenye mahandaki. 13:7 Hes 32:33; Mwa 35:5; Kut 19:16Hata baadhi ya Waebrania wakavuka Yordani mpaka nchi ya Gadi na Gileadi.

Sauli akabaki huko Gilgali, navyo vikosi vyote vilivyokuwa pamoja naye vilikuwa vikitetemeka kwa hofu. 13:8 1Sam 10:8Akangoja kwa siku saba, muda uliowekwa na Samweli; lakini Samweli hakuja Gilgali, nao watu wa Sauli wakaanza kutawanyika. 13:9 Kum 12:5-14; 2Sam 24:25; 1Fal 3:4; 2Nya 26:16; Mit 15:8; 21:3, 27; Ebr 5:4Basi akasema, “Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani.” Naye Sauli akatoa sadaka ya kuteketezwa. 13:10 1Sam 15:13; 25:14; Rut 2:4Mara alipomaliza kutoa hiyo sadaka, Samweli akatokea, naye Sauli akaondoka kwenda kumlaki.

Samweli akamuuliza, “Umefanya nini?”

Sauli akajibu, “Nilipoona kwamba watu wanatawanyika, na kwamba hukuja wakati uliopangwa na kwamba Wafilisti walikuwa wakikusanyika huko Mikmashi, 13:12 Yos 10:43; Kum 4:29; Za 119:58; Yer 26:19nikawaza, ‘Sasa Wafilisti watateremka dhidi yangu huko Gilgali nami sijaomba kibali kwa Bwana.’ Hivyo nikalazimika kutoa sadaka ya kuteketezwa.”

13:13 2Nya 16:9; Yos 22:16; 1Sam 15:23, 24; 2Sam 7:15; 1Nya 10:13; Za 72:5; 1Fal 18:18; Ay 34:18; Mit 19:3; Mt 14:3, 4; Law 17:1; Hes 18:7Samweli akasema, “Umetenda kwa upumbavu. Hukuyashika maagizo ya Bwana Mungu wako aliyokupa. Kama ungelitii, angeudumisha ufalme wako juu ya Israeli kwa wakati wote. 13:14 1Sam 15:28; 18:8; 24:20; 1Nya 10:14; Mdo 7:46; 13:12; 2Sam 6:21; 1Sam 25:10; 2Sam 5:2; Za 18:43; Isa 16:5; 55:4; Yer 30:9; Eze 34:23-24; 37:24; Dan 9:25; Hos 3:5; Mik 5:2; 1Sam 15:26; 16; 1; 2Sam 12:6; 1Fal 13:21Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Bwana amemtafuta mtu aupendezaye moyo wake, na amemchagua awe kiongozi wa watu wake, kwa sababu hukuyatii maagizo ya Bwana.”

13:15 1Sam 14:2Kisha Samweli akaondoka Gilgali, akapanda Gibea ya Benyamini, naye Sauli akawahesabu watu aliokuwa nao. Jumla yao walikuwa watu 600.

Israeli Bila Silaha

13:16 Yos 18:24Sauli, mwanawe Yonathani na watu waliokuwa pamoja nao walikuwa wakiishi huko Gibea ya Benyamini, wakati Wafilisti wakiwa wamepiga kambi huko Mikmashi. 13:17 1Sam 14:15; Yos 18:23Makundi ya wavamiaji walikuja kutoka kambi ya Wafilisti katika vikosi vitatu. Kikosi kimoja kilielekea Ofra karibu na Shuali, 13:18 Yos 10:10; Neh 11:34; Yos 18:13-14; 1Nya 6:68; 2Nya 8:5kikosi kingine kilielekea Beth-Horoni, nacho kikosi cha tatu kilielekea kwenye nchi ya mpakani ielekeayo Bonde la Seboimu linalotazamana na jangwa.

13:19 Mwa 4:22; Hes 25:7; Yer 24:1; 2Fal 24:14Hapakuwa na mhunzi ambaye angeweza kupatikana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walikuwa wamesema, “Waebrania wasije wakatengeneza panga au mikuki!” Hivyo Waisraeli wote huteremka kwa Wafilisti ili kunoa majembe ya plau, majembe ya mkono, mashoka na miundu. Bei ilikuwa fedha theluthi mbili za shekeli13:21 Theluthi mbili za shekeli za fedha ni sawa na gramu 8. kunoa majembe ya plau na majembe ya mkono, na theluthi moja ya shekeli13:21 Theluthi moja ya shekeli ya fedha ni sawa na gramu 4. kwa nyuma, mashoka na michokoo.

13:22 1Nya 9:39; Hes 25:7; 1Sam 14:6; 17:47; Zek 4:6; Amu 5:8Kwa hiyo siku ya vita hakuna askari yeyote aliyekuwa kambini na Sauli na Yonathani ambaye alikuwa na upanga wala mkuki mkononi mwake; Sauli tu na mwanawe Yonathani ndio waliokuwa navyo.

Yonathani Awashambulia Wafilisti

13:23 1Sam 14:4Basi kikosi cha Wafilisti kilikuwa kimetoka kuelekea njia iendayo Mikmashi.

Read More of 1 Samweli 13

1 Samweli 14:1-23

Siku moja Yonathani mwana wa Sauli akamwambia kijana mbeba silaha wake, akasema, “Njoo, tuwavukie Wafilisti kwenye doria upande ule mwingine.” Lakini hakumwambia baba yake.

14:2 Amu 4:5; 1Sam 13:15; Kut 28:33; Isa 10:28Sauli alikuwa akikaa kwenye viunga vya Gibea chini ya mkomamanga huko Migroni. Alikuwa pamoja na watu kama 600, 14:3 Mwa 35:18; 1Sam 22:11; 1:3; Za 78:60; 1Sam 4:21; 2:28; 4:21; Kut 28:30; 1Sam 2:28; 22:18miongoni mwao alikuwepo Ahiya, ambaye alikuwa amevaa kisibau. Alikuwa mwana wa Ikabodi, nduguye Ahitubu mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa Bwana huko Shilo. Hakuna yeyote aliyekuwa na habari kwamba Yonathani alikuwa ameondoka.

14:4 1Sam 13:23Kila upande wa njia ambayo Yonathani alikusudia kupita ili kuvuka kufikia doria ya Wafilisti kulikuwepo na jabali; moja lilikuwa linaitwa Bosesi, na jingine Sene. 14:5 Yos 18:24Jabali moja lilisimama kaskazini kuelekea Mikmashi na jingine upande wa kusini kuelekea Geba.

14:6 Amu 14:3; 1Sam 17:26; 31:4; Yer 9:26; Eze 28:10; 1Sam 13:22; 1Fal 19:12; Mt 19:26; Ebr 11:34; Amu 7:4; Za 33:16; 1Sam 17:46-47Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda Bwana atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia Bwana kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”

Mbeba silaha wake akamwambia, “Fanya yale yote uliyo nayo katika moyo wako. Songa mbele; moyo wangu na roho yangu viko pamoja nawe.”

Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone. Kama wakituambia, ‘Subirini hapo mpaka tuje kwenu,’ tutakaa pale tulipo na hatutakwea kwao. 14:10 Mwa 24:1, 14; Yos 2:24; Amu 6:36-37; 1Sam 10:7; 2Sam 5:24; Isa 7:11-14Lakini kama watasema, ‘Pandeni mje kwetu,’ tutakwea, kwa sababu hiyo itakuwa ishara yetu kwamba Bwana amewatia mikononi mwetu.”

14:11 Mwa 14:13; 1Sam 13:6Basi wote wawili wakajionyesha kwa doria ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, “Tazama! Waebrania wanatambaa toka mashimoni walimokuwa wamejificha.” 14:12 Amu 8:16; 1Sam 17:46; 2Sam 5:24; 1Sam 17:43-44Watu wa kwenye doria wakawapigia kelele Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njooni, pandeni kwetu nasi tutawakomesha.”

Basi Yonathani akamwambia mbeba silaha wake, “Panda nyuma yangu; Bwana amewatia mikononi mwa Israeli.”

Yonathani akapanda juu, akitumia mikono yake na miguu, pamoja na mbeba silaha wake papo hapo nyuma yake. Wafilisti wakaanguka mbele ya Yonathani, naye mbeba silaha wake akamfuata akiwaua nyuma yake. Katika hilo shambulio la kwanza, Yonathani na mbeba silaha wake waliua kama watu ishirini kwenye eneo kama la nusu eka.

Israeli Wawafukuza Wafilisti

14:15 Mwa 35:5; Kut 14:24; 19:16; 2Fal 7:5-7; 1Sam 13:17; Amu 7:21; Ay 18:11; Za 48:5-6Kisha fadhaa ikawapata jeshi lote, wale waliokuwa kambini na shambani, wale waliokuwa katika doria na makundi ya washambuliaji, nayo nchi ilitetemeka. Ilikuwa ni hofu ya ghafula iliyotumwa na Mungu.

14:16 2Sam 18:24; 2Fal 9:17; Isa 52:8; Eze 33:2Wapelelezi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona jeshi likitokomea pande zote. Ndipo Sauli akawaambia watu wale waliokuwa pamoja naye, “Kagueni jeshi mkaone ni nani ameondoka katikati yetu.” Walipokagua, akawa ni Yonathani na mbeba silaha wake ambao hawakuwepo.

14:18 1Sam 30:7; Amu 18:5Sauli akamwambia Ahiya, “Leta Sanduku la Mungu.” (Wakati huo lilikuwa kwa Waisraeli.) 14:19 Hes 27:21; Yos 9:14; Za 106:13Wakati Sauli alipokuwa akisema na kuhani, makelele katika kambi ya Wafilisti yakaongezeka zaidi na zaidi. Hivyo Sauli akamwambia kuhani, “Rudisha mkono wako.”

14:20 Amu 7:22; Eze 38:21; Zek 14:13; 2Nya 20:23Kisha Sauli na watu wake wote wakakusanyika na kwenda vitani. Wakawakuta Wafilisti wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, wakitiana panga kila mmoja na wenzake. 14:21 1Sam 29:4Wale Waebrania ambao walishakuwa pamoja na Wafilisti, na waliokuwa wamepanda pamoja nao katika kambi zao, wakaenda upande wa Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani. 14:22 1Sam 13:6; Isa 9:19-21Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika nchi ya milima ya Efraimu waliposikia kuwa Wafilisti wamekimbia, wakajiunga vitani na kuwafuata kwa bidii. 14:23 Kut 14:30; Yos 7; 2; 1Sam 13:5; Za 44:6-7; Isa 63:9; Za 17:7Hivyo Bwana akawaokoa Waisraeli siku ile, navyo vita vilienea hadi kupita Beth-Aveni.

Read More of 1 Samweli 14