1 Samweli 10:9-27, 1 Samweli 11:1-15, 1 Samweli 12:1-25 NEN

1 Samweli 10:9-27

Sauli Afanywa Mfalme

10:9 Kum 13:2Ikawa Sauli alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu aliubadilisha moyo wa Sauli, na ishara hizi zote zikatimizwa siku ile. 10:10 Hes 11:25; 1Sam 11:6; 19:20; Mt 7:21-23Walipofika Gibea, akakutana na kundi la manabii. Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akajiunga nao katika kutoa unabii kwao. 10:11 Mt 13:54; Yn 7:15; 1Sam 19:24; 2Fal 9:11; Yer 29:26; Hos 9:7Ikawa wale wote waliomfahamu hapo mwanzo walipomwona akitoa unabii pamoja na manabii, wakaulizana, “Ni nini hiki kilichomtokea mwana wa Kishi? Je, Sauli naye pia yumo miongoni mwa manabii?”

10:12 Isa 54:13; Yn 3:8Mtu mmoja ambaye aliishi huko akajibu, “Je, naye baba yao ni nani?” Basi ikawa mithali, kusema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?” 10:13 1Sam 19:23Baada ya Sauli kumaliza kutoa unabii, alikwenda mahali pa juu.

10:14 1Sam 14:50; 9:3Basi babaye mdogo akamuuliza Sauli na mtumishi wake, “Je, mlikuwa wapi?”

Akajibu, “Tulikuwa tukiwatafuta punda. Lakini tulipoona hawapatikani, tulikwenda kwa Samweli.”

Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.”

10:16 1Sam 9:3, 20Sauli akajibu, “Alituhakikishia kwamba punda wamepatikana.” Lakini hakumwambia babaye mdogo kila kitu Samweli alichomwambia kuhusu ufalme.

10:17 1Sam 7:5; Amu 20:1; 1Sam 11:15Samweli akawaita watu wa Israeli kuja kwa Bwana huko Mispa, 10:18 Kut 1:14; Hes 10:9; Amu 6:8-9; Kum 4:34; Neh 9:9-12naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowaonea.’ 10:19 Hes 11:20; Kum 33:5; Za 7:10; 18:48; 68:20; 145:19; 1Sam 8:5; Kum 17:14; Yos 7:14Lakini sasa mmemkataa Mungu wenu, ambaye anawaokoa toka katika maafa yenu yote na taabu zenu zote. Nanyi mmesema, ‘Hapana, tuteulie mfalme atutawale.’ Sasa basi, jihudhurisheni wenyewe mbele za Bwana kwa kabila zenu na kwa koo zenu.”

10:20 Yos 7:14; Mdo 1:24Samweli alipoyasogeza makabila yote ya Israeli, kabila la Benyamini likachaguliwa. 10:21 Es 3:7; Mit 16:33Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana. 10:22 Mwa 25:22; Amu 18:5Wakazidi kuuliza kwa Bwana, “Je, huyo mtu amekwisha kufika hapa?”

Naye Bwana akasema, “Ndiyo, amejificha katikati ya mizigo.”

10:23 1Sam 9:2Wakakimbia na kumleta kutoka huko, naye aliposimama katikati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wengine wote. 10:24 Kum 17:15; 2Sam 21:6; 1Sam 9:2; 1Fal 1:25, 34, 39; 2Fal 11:12Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye Bwana amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.”

Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.”

10:25 1Sam 8:9; Kum 17:14-20; 1Sam 8:11-18; 2Fal 11:12; 1Sam 11:14Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za Bwana. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake.

10:26 Amu 19:14; 20:44Sauli pia akaenda nyumbani kwake huko Gibea, akisindikizwa na watu hodari ambao Mungu alikuwa amegusa mioyo yao. 10:27 Kum 13:13; 1Sam 20:7; 1Fal 10:25; 2Nya 32:23; 17:5; Za 68:29; Mdo 7:35, 51, 52; 2Sam 8:2; 1Fal 4:21; 10:25; Za 72:10; Mt 2:11Lakini baadhi ya watu wakorofi walisema, “Huyu mtu atawezaje kutuokoa?” Wakamdharau na wala hawakumletea zawadi. Lakini Sauli akanyamaza kimya.

Read More of 1 Samweli 10

1 Samweli 11:1-15

Sauli Aukomboa Mji Wa Yabeshi

11:1 Mwa 19:38; 1Sam 12:12; 31:11; 2Sam 10:2; 17:27; 2:4-5; 21:12; Kut 23:32; Yer 37:1; Eze 17:13; 1Nya 19:1; Amu 21:8Nahashi yule Mwamoni, akakwea kuuzunguka kwa jeshi mji wa Yabeshi-Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia, “Fanya mkataba na sisi, na tutakuwa chini yako.”

11:2 Mwa 34:15; Hes 16:14; 1Sam 17:26; 2Sam 17:26Lakini Nahashi yule Mwamoni akajibu, “Nitafanya mkataba na ninyi tu kwa sharti kwamba nitangʼoa jicho la kulia la kila mmoja wenu, na hivyo kuleta aibu juu ya Israeli yote.”

11:3 1Sam 8:4; Amu 2:16Viongozi wa Yabeshi wakamwambia, “Tupe siku saba ili tuweze kutuma wajumbe katika Israeli yote, kama hakuna hata mmoja anayekuja kutuokoa, tutajisalimisha kwako.”

11:4 1Sam 10:5; 15:34; Mwa 27:38; Hes 25:6; Amu 2:4; 21:2; 2Sam 21:6; Rum 12:15Wajumbe walipofika Gibea ya Sauli na kutoa taarifa juu ya masharti haya kwa watu, wote walilia kwa sauti kubwa. Wakati huo huo Sauli alikuwa anarudi kutoka mashambani, akiwa nyuma ya maksai wake, naye akauliza, “Watu wana nini? Mbona wanalia?” Ndipo wakamweleza jinsi watu wa Yabeshi walivyokuwa wamesema.

11:6 Amu 3:10; 6:34; 13:25; 1Sam 10:10; 16:13Sauli aliposikia maneno yao, Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akawaka hasira. 11:7 1Sam 6:14; Amu 19:29; 21:5; 20:1; Mwa 35:5; 1Nya 14:14; 17:10; Mit 14:26Akachukua jozi ya maksai na kuwakata vipande vipande, naye kuvituma hivyo vipande kupitia wajumbe katika Israeli yote, wakitangaza, “Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa maksai wa kila mmoja ambaye hatamfuata Sauli na Samweli.” Kisha hofu ya Bwana ikawaangukia watu, nao wakatoka kama mtu mmoja. 11:8 Amu 20:2; 1:4; 2Sam 24:9Sauli alipowakusanya huko Bezeki, watu wa Israeli walikuwa 300,000 na watu wa Yuda 30,000.

Wakawaambia wale wajumbe waliokuwa wamekuja, “Waambieni watu wa Yabeshi-Gileadi, ‘Kesho kabla jua halijawa kali, mtaokolewa.’ ” Wajumbe walipokwenda na kutoa taarifa hii kwa watu wa Yabeshi, wakafurahi. Wakawaambia Waamoni, “Kesho tutajisalimisha kwenu, nanyi mtaweza kututendea chochote mnachoona chema kwenu.”

11:11 Amu 7:16; Mwa 19:38Kesho yake Sauli alitenganisha watu wake katika vikosi vitatu; wakati wa zamu ya mwisho ya usiku wakaingia katika kambi ya Waamoni na kuwachinja mpaka mchana. Wale walionusurika wakasambaa, kiasi kwamba hawakusalia watu wawili pamoja.

Sauli Athibitishwa Kuwa Mfalme

11:12 Kum 13:13; Lk 19:27Kisha watu wakamwambia Samweli, “Ni nani yule aliyeuliza, ‘Je, Sauli atatawala juu yetu?’ Tuletee hawa watu, nasi tutawaua.”

11:13 2Sam 19:22; 1Sam 19:5; 1Nya 11:14; Kut 14:13; Za 44:4-8; Ebr 2:3Lakini Sauli akasema, “Hakuna hata mmoja atakayeuawa leo, kwa kuwa siku hii Bwana ameokoa Israeli.”

11:14 Yos 10:43; 1Sam 10:8; 10:25Ndipo Samweli akawaambia watu, “Njooni, twendeni Gilgali na huko tuthibitishe ufalme.” 11:15 Yos 5:9; 2Sam 19:15; 1Sam 12:1Kwa hiyo watu wote wakaenda Gilgali na kumthibitisha Sauli kuwa mfalme mbele za Bwana. Huko wakatoa dhabihu za sadaka za amani mbele za Bwana, naye Sauli na Waisraeli wote wakafanya karamu kubwa.

Read More of 1 Samweli 11

1 Samweli 12:1-25

Hotuba Ya Samweli Ya Kuaga

12:1 1Sam 8:7; 11:15; 10:25Samweli akawaambia Israeli wote, “Nimesikiliza kila kitu mlichoniambia nami nimewawekea mfalme juu yenu. 12:2 1Sam 8:5; 8:3; Hes 27:17Sasa mnaye mfalme kama kiongozi wenu. Lakini kwa habari yangu mimi ni mzee na nina mvi, nao wanangu wapo hapa pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu mpaka siku hii ya leo. 12:3 1Sam 9:16; 24:6; 26:9-11; 2Sam 1; 14; 19:21; Za 105:15; Hes 16:15; Kut 18:21; 20:17; 1Sam 8; 3; Mdo 20:33; Law 25:14; Kum 16:19Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele za Bwana na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, mimi nitawarudishia.”

Wakajibu, “Hujatudanganya wala kutuonea. Hujapokea chochote kutoka kwenye mkono wa mtu awaye yote.”

12:5 Mwa 31:50; Mdo 23:9; 24:20; Kut 22:4; Yn 18:38; 2Kor 1:12; Za 17:3Samweli akawaambia, “Bwana ni shahidi juu yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta chochote mkononi mwangu.”

Wakasema, “Yeye ni shahidi.”

12:6 Kut 6:26; 3:10; Mik 6:4; Neh 9:9-14; 2Kor 1:12; Za 17:3Kisha Samweli akawaambia watu, “Bwana ndiye alimchagua Mose na Aroni, na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri. 12:7 Yos 24:1; Isa 1:18; 3:14; Yer 2:9; 25:31; Eze 17:20; 20:35; Mik 6:1-5; Amu 5; 11Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu nitakabiliana nanyi kwa ushahidi mbele za Bwana wa matendo yote ya haki yaliyofanywa na Bwana kwenu na kwa baba zenu.

12:8 Mwa 46:6; Kut 2:23; 3:10; 4:16“Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia Bwana kwa ajili ya msaada, naye Bwana akawatuma Mose na Aroni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa.

12:9 Kum 32:18; 32:30; Amu 3:7; 4:2; 10:7; 3:12; 13:1; Yos 11:1“Lakini wakamsahau Bwana Mungu wao, hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori na katika mikono ya Wafilisti na mfalme wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao. 12:10 Amu 3:9; 2:13; 10:10, 15; 1Sam 8:8; 7:3Wakamlilia Bwana na kusema, ‘Tumetenda dhambi; tumemwacha Bwana na kutumikia Mabaali na Maashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia.’ 12:11 Amu 6:32; 4:6; 11:1; 1Sam 7:15Ndipo Bwana akawatuma Yerub-Baali,12:11 Yerub-Baali pia aliitwa Gideoni. Baraka, Yefta na Samweli, naye akawaokoa kutoka mikononi mwa adui zenu kila upande, ili ninyi mpate kukaa salama.

12:12 1Sam 11:1; 8:5; 25:30; 1Nya 5:2; 2Sam 5:2; Amu 8:3-23“Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawa Bwana Mungu wenu alikuwa mfalme wenu. 12:13 1Sam 8:5; 9:20; 10:24; Hos 13:11Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni, Bwana amemweka mfalme juu yenu. 12:14 Yos 24:14; Yer 4:17; Mao 1:18; Kum 6:13; 10:12; 13:4; Yos 24:14; Za 81:13; Mhu 8:12; Isa 3:10Kama mkimcha Bwana na kumtumikia na kumtii nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayetawala juu yenu mkimfuata Bwana, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu! 12:15 Law 26:16; Yos 24:20; Isa 1:20; Yer 4:17; 26:4Lakini kama hamkumtii Bwana, nanyi kama mkiasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu.

12:16 Kut 14:13-14“Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo Bwana anakwenda kulifanya mbele ya macho yenu! 12:17 Mwa 30:14; 7:12; 1Sam 6:13; 2:10; 1Fal 18:42; Yak 5:18; Kut 9:23; 9:18; Ay 37:13; Mit 26:1; 1Sam 8:6-7; 7:9-10Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba Bwana ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya Bwana mlipoomba mfalme.”

12:18 Za 99:8; Mwa 3:10; Kut 14:31Kisha Samweli akamwomba Bwana, na siku ile ile Bwana akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana Bwana na Samweli.

12:19 Kut 8:8; 1Sam 7:8; Yer 37:3; Yak 5:18; 1Yn 5:16Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe Bwana Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”

12:20 Kum 32:30Samweli akajibu, “Msiogope, mmefanya uovu huu wote; hata hivyo msimwache Bwana, bali mtumikieni Bwana kwa moyo wenu wote. 12:21 Isa 40:20; 41:24-29; 44:9; Yer 2:5, 11; 14:22; 16:19; Yn 2:8; Hab 2:8; Mdo 14:15; Kum 11:16Msigeukie sanamu zisizofaa. Haziwezi kuwatendea jema, wala haziwezi kuwaokoa kwa sababu hazina maana. 12:22 Za 25:11; 106:8; Isa 48:9-11; Yer 14:7; Dan 9:19; Yos 7:9; 2Sam 7:23; Yn 17:12; Law 26:11; Kum 31:6; 7:7; 1Pet 2:6; 1Fal 6:13Kwa ajili ya jina lake kuu Bwana hatawakataa watu wake, kwa sababu ilimpendeza Bwana kuwafanya kuwa wake mwenyewe. 12:23 Hes 11:2; 1Sam 1:20; 7:2; Rum 1:10; 1Fal 8:36; Za 25:4; 34:11; 86:11; 94:12; Mit 4:11; Kol 1:9Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya Bwana kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka. 12:24 Kum 6:2; Mhu 12:13; Kum 6:5; Yos 24:14; Ay 34:27; Isa 5:12; 22:11; 26:10; Kum 10:21Lakini hakikisheni mnamcha Bwana na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote; tafakarini mambo makubwa aliyoyatenda kwa ajili yenu. 12:25 1Sam 31:1-5; Kum 28:36; Yos 24:20; 1Fal 14:10Hata hivyo mkiendelea kufanya uovu, ninyi na mfalme wenu mtafutiliwa mbali!”

Read More of 1 Samweli 12