1 Wafalme 9:10-28, 1 Wafalme 10:1-29, 1 Wafalme 11:1-13 NEN

1 Wafalme 9:10-28

Shughuli Nyingine Za Solomoni

(2 Nyakati 8)

9:10 Kum 11:8; Isa 1:19-20Miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Solomoni alijenga majengo haya mawili, yaani Hekalu la Bwana na jumba la kifalme, 9:11 Law 18:25-28; Kum 18:9; 1Fal 14:24Mfalme Solomoni akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji. 9:12 Kut 34:15; Kum 7:3; Mit 13:22; Kut 23:32-33; Amu 2:2; 2Pet 2:20; 2Kor 6:14Lakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Solomoni alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. 9:13 Ay 15:5; Za 103:10Hiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?”

Naye akaiita nchi ya Kabul,9:13 Kabul maana yake isiyofaa kitu. jina lililoko hadi leo. 9:14 Kum 9:8-14; Neh 13:27; Yn 5:14Basi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 1209:14 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu.

9:15 Neh 9:33; Za 51:4; Rum 3:19; Isa 24:16; 1Fal 8:47; Dan 9:14; Za 130:3Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Solomoni, alivyowafanyiza watu ili kulijenga hekalu la Bwana, na jumba lake la kifalme, na Milo,9:15 Milo maana yake Boma la Ngome, pia 9:24. ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri. (Farao mfalme wa Misri alikuwa ameushambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Solomoni, kama zawadi ya arusi. Solomoni akaujenga tena Gezeri.) Akajenga Beth-Horoni ya Chini, akajenga Baalathi na Tamari kwenye jangwa katika eneo la nchi yake, vilevile miji ya ghala na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake: chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika eneo yote aliyotawala.

Watu wote waliosalia kutoka kwa Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi (mataifa haya hayakuwa Waisraeli), yaani, wazao wao waliobakia katika nchi, ambao Waisraeli hawangeweza kuwaangamiza kabisa: hawa Solomoni akawalazimisha kuwa watumwa katika shokoa, kama ilivyo hadi leo. Lakini Solomoni hakumfanya yeyote wa Waisraeli kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa wapiganaji wake, maafisa wake wa serikali, maafisa wake, wakuu wake, majemadari wa jeshi wa magari yake ya vita na wapanda farasi. Pia walikuwa maafisa wakuu wasimamizi wa miradi ya Solomoni: maafisa 550 waliwasimamia watu waliofanya kazi.

Baada ya binti Farao kuja kutoka Mji wa Daudi na kuingia jumba la kifalme ambalo Solomoni alikuwa amemjengea, akajenga Milo.

Solomoni akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejengea kwa ajili ya Bwana, akifukiza uvumba mbele za Bwana pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za hekalu.

Mfalme Solomoni pia akatengeneza pia meli huko Esion-Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika Edomu, kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu.9:26 Yaani Bahari Nyekundu au Bahari ya Mafunjo. Naye Hiramu akawatuma watu wake; mabaharia walioijua bahari, kuhudumu katika hizo meli pamoja na watu wa Solomoni. Wakasafiri kwa bahari mpaka Ofiri na kurudi na talanta 4209:28 Talanta 420 za dhahabu ni sawa na tani 14. za dhahabu, ambazo walimkabidhi Mfalme Solomoni.

Read More of 1 Wafalme 9

1 Wafalme 10:1-29

Malkia Wa Sheba Amtembelea Solomoni

(2 Nyakati 9:1-12)

10:1 2Nya 20:9; Dan 9:20Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni na uhusiano wake na jina la Bwana, akaja kumjaribu kwa maswali magumu. 10:2 Ezr 9:2; Kut 34:13; Neh 13:27; Kum 30:8-10Alifika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana: pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani; alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. 10:3 2Fal 11:17; 2Nya 34:31; Kut 34:16; Kum 7:2-3; Ezr 9:4; Za 119:53, 120; Isa 66:2Solomoni akamjibu maswali yake yote, hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea. 10:4 1Nya 28:10; Isa 35:3-4Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, 10:5 Neh 5:12; 13:25chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika hekalu la Bwana, alipatwa na mshangao.

10:6 Kum 9:18; Yn 3:7; Za 102:4Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli. Lakini sikuamini mambo haya hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana ile taarifa niliyoisikia. 10:8 Law 27:28; Yos 6:19Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako! 10:9 1Sam 12:18; Ezr 1:5Ahimidiwe Bwana Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe na kukuweka juu ya kiti cha ufalme cha Israeli. Kwa sababu ya upendo wake Bwana wa milele ajili ya Israeli, amekufanya mfalme, ili kudumisha haki na uadilifu.”

Naye akampa mfalme talanta 12010:10 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5. za dhahabu, kiasi kikubwa sana cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa tena vikolezi vingi hivyo kuletwa kama vile malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.

10:11 Kum 24:1; Mit 28:13; Mal 2:10-16; Yer 3:13; Isa 1:16-17; Rum 12:2(Meli za Hiramu zilileta dhahabu kutoka Ofiri; tena kutoka huko zilileta shehena kubwa ya miti ya msandali na vito vya thamani. 10:12 Yos 6:5Mfalme akatumia miti ya msandali kuwa nguzo ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa au kuonekana humo tangu siku ile.)

Mfalme Solomoni akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, kando na vile mfalme alivyokuwa amempa kwa ukarimu wake wa kifalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.

Fahari Ya Solomoni

(2 Nyakati 9:13-28)

10:14 Kum 16:18; Hes 25:4; 2Nya 30:8; 2Fal 23:26; 2Nya 28:11-13; 29:10; 30:8; Za 78:38; Isa 12:1Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,10:14 Talanta 666 za dhahabu ni sawa na tani 25. 10:15 Neh 11:16mbali na mapato kutoka kwa wafanyabiashara na wachuuzi, na kutoka kwa wafalme wote wa Kiarabu na watawala wa nchi.

Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa; kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 60010:16 Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 3.5. Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu10:17 Mane tatu za dhahabu ni sawa na kilo 1.7. za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.

10:18 Ezr 5:2; 2:2; Amu 3:6; Zek 6:1Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi. 10:19 2Fal 10:15; Law 5:15; 6:4-6; 1Nya 29:24; 2Nya 30:8; Gal 2:9; Mit 22:26Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na egemeo la nyuma lilikuwa la mviringo kwa juu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. 10:20 1Nya 24:14Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote. 10:21 1Nya 24:8Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo siku za Solomoni. 10:22 1Nya 9:12Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara10:22 Au: za Tarshishi (ona pia 1Fal 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 2:16; 60:9). baharini zilizokuwa zikiandamana na meli za Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo.

10:23 Neh 8:7; 9:4Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia. 10:24 Neh 3:1; 12:10Dunia yote ikatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake. 10:25 Ezr 3:2; 8:3; Neh 7:13Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja alileta zawadi: vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.

10:26 Kum 17:16Solomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. 10:27 Ay 27:16; 1Nya 27:28Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue.10:28 Yaani Kilikia ilioko Syria. Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue. 10:29 Hes 13:29Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha10:29 Shekeli 600 za fedha ni sawa na kilo 7. na farasi kwa shekeli 150.10:29 Shekeli 150 za fedha ni sawa na kilo 1.7. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.10:29 Waaramu hapa ina maana ya Washamu.

Read More of 1 Wafalme 10

1 Wafalme 11:1-13

Wakeze Solomoni

11:1 Kut 34:16; 1Fal 12:21, 31Hata hivyo, Mfalme Solomoni akawapenda wanawake wengi wa kigeni zaidi, mbali na binti Farao: wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti. 11:2 Kut 34:16; 1Fal 16:31Walitoka katika mataifa ambayo Bwana aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Solomoni akakaza kuwapenda. 11:3 Mwa 22:24; Mit 31:3Alikuwa na wake 700 mabinti wa uzao wa kifalme, na masuria 300, nao wake zake wakampotosha. 11:4 Kut 34:16; 1Nya 29:19Kadiri Solomoni alivyozidi kuzeeka, wake zake wakaugeuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukujitolea kikamilifu kwa Bwana Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake. 11:5 Amu 2:13Solomoni akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki11:5 Moleki au Milkomu ni mungu aliyekuwa akiabudiwa na Waamoni; alikuwa chukizo kwa sababu watoto walitolewa kafara kwake. mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni. 11:6 Kum 4:25Kwa hiyo Solomoni akafanya uovu machoni pa Bwana; hakumfuata Bwana kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake.

11:7 2Fal 23:13; Hes 21:29; Mdo 7:43Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Solomoni akajenga mahali pa juu kwa ajili ya Kemoshi chukizo la Wamoabu, na kwa Moleki mungu chukizo la Waamoni. Akafanya hivyo kwa wake zake wote wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa dhabihu kwa miungu yao.

11:9 1Fal 3:5Bwana akamkasirikia Solomoni kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye alikuwa amemtokea mara mbili. 11:10 1Fal 9:6; 6:12Ingawa alikuwa amemkataza Solomoni kufuata miungu mingine, Solomoni hakutii amri ya Bwana. Kwa hiyo Bwana akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa hii ndiyo hali yako na hukushika Agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako na kumpa mmoja wa walio chini yako. Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. 11:13 2Sam 7:15; Kum 12:11Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua.”

Read More of 1 Wafalme 11