1 Wafalme 6:1-38, 1 Wafalme 7:1-22 NEN

1 Wafalme 6:1-38

Solomoni Ajenga Hekalu

(2 Nyakati 3)

6:1 Ezr 4:15; 5:17Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Bwana.

Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini,6:2 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27. upana wa dhiraa ishirini6:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. na kimo cha dhiraa thelathini6:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. kwenda juu. 6:3 Ezr 3:10; Hag 2:3Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu. 6:4 1Fal 6:36; Ezr 7:20; Isa 60:6; Za 68:29Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu. 6:5 1Nya 29:2; Yer 27:18-22; Ezr 5:14Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu. 6:6 Ezr 5:3Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano,6:6 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba.6:6 Dhiraa saba ni sawa na mita 3.15. Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu.

Katika kujenga Hekalu, yalitumika tu mawe yaliyochongwa huko machimboni, wala hakuna nyundo, patasi au chombo kingine chochote cha chuma kilichosikika sauti yake katika eneo la ujenzi wa Hekalu wakati lilipokuwa likijengwa.

6:8 1Sam 9:10Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu, ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutokea hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu. Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha, akiliweka paa za boriti na mbao za mierezi. 6:10 Ezr 7:23; Yer 29:7; Law 1:9; Mwa 8:21; 1Tim 2:1-2Mfalme Solomoni akajenga vyumba vya pembeni kuzunguka Hekalu lote. Kimo cha kila kimoja kilikuwa dhiraa tano. Navyo vilikuwa vimeunganishwa na Hekalu kwa boriti za mierezi.

6:11 Kum 21:22-23; Es 2:23; Ezr 7:26; Dan 2:5Neno la Bwana likamjia Solomoni kusema: 6:12 Kut 20:24; Kum 12:11; 1Fal 9:3; 2Nya 7:16; Za 132:13“Kwa habari ya Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, kwa kupitia wewe nitatimiza ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako. 6:13 Ay 5:12; Ezr 4:9; Za 9:16; 1Kor 3:19Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.”

6:14 Ezr 5:1; 7:1; Neh 2:1; Ezr 4:24Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha. 6:15 Zek 4:9Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari. 6:16 1Fal 8:63; 2Nya 7:15; Yn 10:22Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu. 6:17 2Sam 6:13; 1Nya 16:1-3; 2Nya 29:21; Hes 7:2-3; Ezr 8:25Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini.6:17 Dhiraa 40 ni sawa na mita 18. 6:18 1Nya 24:1; 23:6; Hes 3:6-9; 8:9-11Hekalu ndani ilikuwa ya mierezi iliyonakshiwa mifano ya maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana.

6:19 Kut 12:11; Hes 28:16Ndani ya Hekalu akatengeneza sehemu takatifu ya ndani, kwa ajili ya kuweka Sanduku la Agano la Bwana. 6:20 2Nya 30:15-17; 35:11; Kut 12:25; 2Nya 29:34Sehemu takatifu ya ndani ilikuwa na upana, urefu na kimo cha dhiraa ishirini ndani kwa ndani. Akaifunika ndani kwa dhahabu safi, pia akaifunika madhabahu ya mierezi vivyo hivyo. 6:21 Kut 12:48; Za 93:5Solomoni akaifunika sehemu ya ndani ya Hekalu kwa dhahabu safi, naye akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande moja hadi ule mwingine mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, ambako palifunikwa kwa dhahabu. 6:22 Kut 12:17; Mit 21:1; Ezr 1:1Basi akafunika sehemu yote ya ndani kwa dhahabu. Pia akafunika madhabahu yale yaliyokuwa ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kwa dhahabu.

Katika Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza makerubi wawili kwa mzeituni, kila moja likiwa na dhiraa kumi6:23 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. kwenda juu. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na bawa jingine dhiraa tano, hivyo urefu kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa jingine ulikuwa dhiraa kumi. Kerubi wa pili alikuwa na urefu wa dhiraa kumi pia, hivyo makerubi hao wawili walifanana kwa vipimo na kwa umbo. Kimo cha kila kerubi kilikuwa dhiraa kumi. Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba. Akafunika wale makerubi kwa dhahabu.

Juu ya kuta zote zilizozunguka Hekalu, za vyumba vya ndani na vya nje, zilipambwa kwa nakshi zilizokatwa za makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua. Pia alifunika sakafu zote za vyumba vya ndani na vya nje vya Hekalu kwa dhahabu.

Kwa ingilio la Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza milango ya mbao za mzeituni, zikiwa na miimo na vizingiti vyenye umbo la pembe tano. Juu ya milango miwili ya mbao za mzeituni alinakshi makerubi, miti ya mitende pamoja na maua yaliyochanua na kufunika makerubi na miti ya mitende kwa dhahabu iliyofuliwa. Kwa njia iyo hiyo akatengeneza miimo yenye pande nne ya miti ya mizeituni, kwa ajili ya ingilio la ukumbi mkubwa. Kulikuwa na milango miwili iliyoweza kukunjuka iliyotengenezwa kwa mbao za msunobari na kila mmoja ulikuwa na bawaba ambazo zingeuwezesha kujikunja kila kipande juu ya kingine. Akanakshi makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua juu yake na kufunika kwa dhahabu iliyonyooshwa vizuri juu ya michoro.

Tena akajenga ua wa ndani safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa.

Msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa tano. Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Solomoni. Alilijenga kwa miaka saba.

Read More of 1 Wafalme 6

1 Wafalme 7:1-22

Solomoni Ajenga Jumba Lake La Kifalme

7:1 Ezr 4:7; Neh 2:1; 1Nya 6:14Ilimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 7:2 1Fal 2:35; Neh 11:11Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,7:2 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,7:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa. Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu. Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. Milango yote ilikuwa na miimo ya mstatili, ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana.

7:6 Neh 12:36; Ezr 5:5; Isa 41:20; Mwa 32:28; Neh 1:10-11Akajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini7:6 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoningʼinia.

7:7 Ezr 8:1; 2:43Akajenga ukumbi wa kiti cha enzi, Ukumbi wa Hukumu, mahali ambapo angelitolea hukumu, akaufunika kwa mierezi kutoka sakafuni hadi darini. Kwenye jumba la kifalme ambamo angeliishi, aliiweka nyuma zaidi, ikiwa na mjengo wa aina moja na hiyo nyingine. Pia Solomoni akajenga jumba la kifalme linalofanana na huo ukumbi mkubwa kwa ajili ya binti Farao, aliyekuwa amemwoa.

7:9 Neh 2:8Ujenzi huu wote, kuanzia nje mpaka kwenye ua mkuu na kuanzia kwenye msingi hadi upenuni, ulifanywa kwa mawe ya ubora wa hali ya juu yaliyokuwa yamechongwa kwa vipimo na kusawazishwa kwa msumeno nyuso zake za ndani na za nje. 7:10 Kum 33:10; Neh 8:1-8; 2Tim 4:2; 1Sam 7:3; 2Nya 12:14; Za 10:18; 119:45; Mal 2:7Misingi iliwekwa kwa mawe makubwa yaliyo bora, yenye urefu wa dhiraa kumi7:10 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. na mengine yenye urefu wa dhiraa nane7:10 Dhiraa nane ni sawa na mita 3.6. Sehemu za juu kulikuwepo na mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo na boriti za mierezi. 7:12 Dan 2:37; Ezr 4:10Ule ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Bwana na baraza yake.

Samani Za Hekalu

(2 Nyakati 4)

Mfalme Solomoni akatuma watu Tiro kumleta Hiramu, 7:14 Es 1:14ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Solomoni na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.

7:15 Kum 12:5; 1Nya 29:6; 2Nya 6:2; Za 135:21Hiramu akasubu nguzo mbili za shaba, kila moja ikiwa na urefu wa dhiraa kumi na nane,7:15 Dhiraa 18 ni sawa na mita 8.1. kila nguzo ikiwa na mzingo wa dhiraa kumi na mbili7:15 Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4. kwa mstari. 7:16 Kut 3:22; Ezr 8:25; Zek 6:10; 1Nya 29:6Pia alitengeneza mataji mawili ya shaba ya kusubu ili kuyaweka juu ya hizo nguzo; kila taji lilikuwa na kimo cha dhiraa tano7:16 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. kwenda juu. 7:17 2Fal 3:5; Hes 15:5-12Wavu wa mikufu iliyosokotewa kwenye zile taji juu ya zile nguzo, saba kwa kila taji. Akatengeneza makomamanga katika safu mbili kuzunguka kila wavu kuremba mataji yaliyo juu ya nguzo. Alifanya hivyo kwa kila nguzo. 7:19 Ezr 5:14; Yer 27:22Mataji yaliyokuwa juu ya nguzo kwenye baraza, yalikuwa katika umbo la yungiyungi, kimo chake ni dhiraa nne7:19 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. 7:20 Ezr 6:4; 1Kor 4:1-2Juu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga 200 katika safu kuzunguka pande zote. 7:21 Ezr 4:16-20; 5:3-6Hiramu akasimamisha nguzo kwenye baraza ya Hekalu. Nguzo ya upande wa kusini akaiita Yakini,7:21 Yakini maana yake Mungu atafanya imara. na ile ya upande wa kaskazini Boazi.7:21 Boazi maana yake Ndani ya Mungu kuna nguvu. Mataji yaliyokuwa juu yalikuwa na umbo la yungiyungi. Hivyo kazi ya nguzo ikakamilika.

Read More of 1 Wafalme 7