1 Wafalme 3:16-28, 1 Wafalme 4:1-34, 1 Wafalme 5:1-18 NEN

1 Wafalme 3:16-28

Utawala Wa Hekima

Basi wanawake wawili makahaba walikuja kwa mfalme na kusimama mbele yake. Mmojawapo akasema, “Bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunaishi kwenye nyumba moja. Nilikuwa nimezaa alipokuwa pamoja nami. Siku ya tatu baada ya mtoto wangu kuzaliwa, mwanamke huyu pia naye akazaa mtoto. Tulikuwa peke yetu, hapakuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba isipokuwa sisi wawili.

“Wakati wa usiku mwana wa huyu mwanamke akafa kwa sababu alimlalia. Hivyo akaondoka katikati ya usiku na kumchukua mwanangu kutoka ubavuni pangu wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa nimelala. Akamweka kifuani mwake na kumweka mwanawe aliyekufa kifuani mwangu. Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”

Huyo mwanamke mwingine akasema, “Hapana! Mwana aliye hai ndiye wangu, aliyekufa ni wako.”

Lakini yule wa kwanza akasisitiza, “Hapana! Mwana aliyekufa ni wako, aliye hai ni wangu.” Hivi ndivyo walivyobishana mbele ya mfalme.

Mfalme akasema, “Huyu anasema, ‘Mwanangu ndiye aliye hai, na aliyekufa ndiye mwanao,’ maadamu yule anasema, ‘Hapana! Aliyekufa ni wako, na aliye hai ni wangu.’ ”

Kisha mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Basi wakamletea mfalme upanga. Ndipo mfalme akatoa amri: “Mkate mtoto aliye hai vipande viwili; mpe huyu nusu na mwingine nusu.”

Mwanamke ambaye mwanawe alikuwa hai akajawa na huruma kwa ajili ya mwanawe na kumwambia mfalme, “Tafadhali, bwana wangu, mpe yeye mtoto aliye hai! Usimuue!”

Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Mkate vipande viwili. Asiwe wangu au wake!”

Kisha mfalme akatoa uamuzi wake: “Mpeni mama wa kwanza mtoto aliye hai. Msimuue; ndiye mama yake.”

Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.

Read More of 1 Wafalme 3

1 Wafalme 4:1-34

Maafisa Wa Solomoni Na Watawala

Basi Mfalme Solomoni akatawala Israeli yote. 4:2 Es 8:17; 2Fal 17:24, 41; 19:37Hawa ndio waliokuwa maafisa wake wakuu:

Kuhani: Azaria mwana wa Sadoki;

4:3 Yn 4:9; 2Nya 36:22-23; Ezr 1:1-4; 6:3; Isa 44:28; Neh 2:20; Mdo 8:21Elihorefu na Ahiya, wana wa Shisha: waandishi;

Yehoshafati mwana wa Ahiludi: karani;

4:4 Ezr 3:3; Yer 38:4; Isa 35:3-4Benaya mwana wa Yehoyada: jemadari mkuu wa jeshi;

Sadoki na Abiathari: makuhani;

Azaria mwana wa Nathani: kiongozi wa maafisa wa wilaya;

Zabudi mwana wa Nathani: kuhani na mshauri binafsi wa mfalme;

4:6 Es 3:13; 9:5; Dan 9:1Ahishari: msimamizi wa jumba la kifalme;

Adoniramu mwana wa Abda: msimamizi wa kazi za kulazimisha.

4:7 Ezr 7:1; Isa 36:11; Neh 2:1Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka. 4:8 Za 112:6; Zek 1:14; Rum 8:28Majina yao ni haya:

Ben-Huri: katika nchi ya vilima ya Efraimu;

4:9 Ezr 5:6; 2Fal 17:30, 31Ben-Dekeri: katika Makasi, Shaalbimu, Beth-Shemeshi na Elon-Bethhanani;

4:10 Neh 4:2; Ezr 7:12Ben-Hesedi: katika Arubothi (Soko na nchi yote ya Heferi zilikuwa zake);

Ben-Abinadabu: katika Nafoth-Dori (alimwoa Tafathi binti Solomoni);

4:12 Amo 7:10; Lk 23:2; Mdo 24:5Baana mwana wa Ahiludi: katika Taanaki na Megido, na katika Beth-Shani yote karibu na Sarethani chini ya Yezreeli, kuanzia Beth-Shani hadi Abel-Mehola kupita hadi Yokmeamu;

4:13 Ezr 7:24; Neh 5:4; Mt 9:9Ben-Geberi: katika Ramoth-Gileadi (makao ya Yairi mwana wa Manase katika Gileadi ilikuwa miji yake, pamoja na wilaya ya Argobu katika Bashani na miji yake mikubwa sitini yenye kuzungukwa na kuta zenye makomeo ya shaba);

Ahinadabu mwana wa Ido: katika Mahanaimu;

4:15 Ezr 5:17; Es 3:8; Mdo 17:6-7Ahimaasi: katika Naftali (alikuwa amemwoa Basemathi binti Solomoni);

Baana mwana wa Hushai: katika Asheri na katika Bealothi;

Yehoshafati mwana wa Parua: katika Isakari;

Shimei mwana wa Ela: katika Benyamini;

4:19 2Fal 18:7Geberi mwana wa Uri: katika Gileadi (nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani). Naye alikuwa ndiye mtawala pekee katika eneo hilo.

Mahitaji Ya Solomoni Ya Kila Siku

4:20 Mwa 15:18-21; Kut 23:31; Za 72:8; 1Nya 18:3Watu wa Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani; walikula, wakanywa na kufurahi. Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.

4:22 Dan 6:2Mahitaji ya Solomoni ya kila siku yalikuwa kori thelathini4:22 Kori 30 ni sawa na madebe 360. za unga laini, kori sitini4:22 Kori 60 ni sawa na madebe 720. za unga wa kawaida. 4:23 Mit 4:16Ngʼombe kumi wa zizini, ngʼombe ishirini wa malisho, kondoo na mbuzi mia moja, pamoja na ayala, paa, kulungu na kuku wazuri sana. 4:24 Dan 9:25; Ay 20:5Kwa kuwa Solomoni alitawala falme zote magharibi ya mto, kuanzia Tifsa hadi Gaza, naye akawa na amani pande zote. Wakati wa maisha ya Solomoni Yuda na Israeli, kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba, wakaishi salama kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake.

Solomoni alikuwa na mabanda 4,0004:26 Waandishi wengine wanasema 40,000 (angalia 2Nya 9:25). ya magari ya vita, na farasi 12,000.

Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua. Pia walileta sehemu walizopangiwa za shayiri na majani kwa ajili ya farasi wavutao magari na farasi wengine mahali palipostahili.

Hekima Ya Solomoni

Mungu akampa Solomoni hekima na akili kubwa, pia ufahamu mpana usiopimika kama mchanga ulioko pwani ya bahari. Hekima ya Solomoni ilikuwa kubwa kuliko hekima ya watu wote wa Mashariki na kubwa kuliko hekima yote ya Misri. Alikuwa na hekima kuliko kila mwandishi, akiwemo Ethani Mwezrahi: kuliko Hemani, Kalkoli na Darda, wana wa Maholi. Umaarufu wake ukaenea kwa mataifa yote yaliyomzunguka. Akanena mithali 3,000 na nyimbo zake zilikuwa 1,005. Akaelezea maisha ya mimea kuanzia mwerezi wa Lebanoni hadi hisopo iotayo ukutani. Pia akafundisha kuhusu wanyama na ndege, wanyama wenye damu baridi, wakiwemo samaki. Watu wa mataifa yote wakaja kusikiliza hekima ya Solomoni, waliotumwa na wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamesikia juu ya hekima yake.

Read More of 1 Wafalme 4

1 Wafalme 5:1-18

Maandalio Ya Ujenzi Wa Hekalu

(2 Nyakati 2:1-18)

5:1 Ezr 6:14; Hag 1:14; Zek 8:9Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Solomoni ametiwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Solomoni, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi. 5:2 1Nya 3:19; Ezr 6:14; Mhu 12:11; Zek 4:6-10; Hag 1:2-15; 2:2-5Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu:

5:3 Ezr 6:6“Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wake, hadi Bwana alipowaweka adui zake chini ya miguu yake. Lakini sasa Bwana Mungu wangu amenipa utulivu kila upande hakuna adui wala maafa. 5:5 2Fal 25:28; 1Pet 3:12; 2Nya 16:9; Ezr 7:6, 28; Za 33:18; Isa 41:10Kwa hiyo, ninakusudia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia baba yangu Daudi, wakati aliposema, ‘Mwanao nitakayemweka kwenye kiti cha ufalme mahali pako, ndiye atajenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

5:6 Ezr 4:9“Hivyo toa amri ili mierezi ya Lebanoni ikatwe kwa ajili yangu. Watu wangu watafanya kazi na watu wako, nami nitawalipa watu wako kwa ujira wowote utakaoupanga. Unajua kwamba hatuna mtu yeyote mwenye ustadi katika kukata miti kama Wasidoni.”

Hiramu aliposikia ujumbe wa Solomoni, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Bwana leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima kutawala juu ya taifa hili kubwa.”

Hiramu akatuma neno kwa Solomoni:

“Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mierezi na misunobari. 5:9 Ezr 4:12Watu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga mafungu mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.”

Kwa njia hii Hiramu akampa Solomoni miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji, 5:11 1Fal 6:1; Yos 24:15; Za 119:46; Yn 1:9; Mt 10:32; Lk 12:8; Mdo 27:23; 2Nya 3:1, 2naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,0005:11 Kori 20,000 ni sawa na madebe 240,000. za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000.5:11 Bathi 20,000 ni sawa na madebe 200. Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. 5:12 2Nya 34:24-25; 36:16, 17; Yer 39:1; 2Fal 24:2Bwana akampa Solomoni hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Solomoni, na wote wawili wakafanya mkataba.

5:13 Ezr 1:1Mfalme Solomoni akakusanya wafanyakazi 30,000 kutoka Israeli yote. 5:14 Ezr 6:5; Dan 5:2; 1Nya 3:18; Hag 1:4Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu 10,000 kwa mwezi, hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja na miezi miwili nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa. Solomoni alikuwa na wachukuzi wa mizigo 70,000 na wachonga mawe 80,000 huko vilimani, 5:16 Ezr 3:10; 6:15; 4:15; 6:1-2pamoja na wasimamizi 3,300 ambao walisimamia kazi hiyo na kuwaongoza wafanyakazi. 5:17 Ezr 6:1, 2; Mit 25:2Kwa amri ya mfalme walitoa kwenye machimbo ya mawe, mawe makubwa, yaliyo bora kwa kujengea msingi wa nyumba yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu. Mafundi wa Solomoni, wa Hiramu na watu wa Gebali5:18 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.

Read More of 1 Wafalme 5