1 Yohana 3:11-24, 1 Yohana 4:1-6 NEN

1 Yohana 3:11-24

Mpendane Ninyi Kwa Ninyi

3:11 1Yn 1:5; Yn 15:12Hili ndilo neno mlilolisikia tangu mwanzo: Kwamba imetupasa tupendane sisi kwa sisi. 3:12 Mwa 4:8; Mt 5:37; Za 38:20; Mit 29:10Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamuua ndugu yake. Basi kwa nini alimuua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki. 3:13 Yn 15:18, 19; 17:14Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama ulimwengu ukiwachukia. 3:14 Yn 5:24; 1Yn 2:9Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini. 3:15 Mt 5:21, 22; Gal 5:20, 21; Yn 3:16Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.

3:16 Yn 10:11; 15:13; Flp 2:17; 1The 2:8Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu. 3:17 Yak 2:15, 16; 1Yn 4:20Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? 3:18 1Yn 2:1; Eze 33:1; Rum 12:9Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli. 3:19 Yn 18:37; 1Yn 1:8Basi hivi ndivyo tutakavyoweza kujua ya kuwa sisi tu wa kweli na hivyo twaithibitisha mioyo yetu mbele za Mungu 3:20 1Kor 4:4kila mara mioyo yetu inapotuhukumu. Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, naye anajua kila kitu.

3:21 Efe 3:12; 1Kor 10:14; 1Yn 5:14Wapendwa, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri mbele za Mungu, 3:22 Mt 7:7; Ebr 13:21lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza. 3:23 Yn 6:23; 13:34Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru. 3:24 1Yn 4:15; 1The 4:8Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupa.

Read More of 1 Yohana 3

1 Yohana 4:1-6

Zijaribuni Hizo Roho

4:1 Mt 7:15; 1Kor 10:14; Yer 29:9; 1Kor 12:10; 2The 2:2; 1Yn 2:18Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. 4:2 Yn 1:4; 1Yn 2:23; 1Kor 12:3Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. 4:3 1Yn 2:22; 2Yn 7; 1Yn 2:18Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.

4:4 Rum 8:31; 2Fal 6:16Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu. 4:5 Yn 17:14, 16Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza. 4:6 Yn 8:47; 14:17Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.

Read More of 1 Yohana 4