1 Yohana 2:28-29, 1 Yohana 3:1-10 NEN

1 Yohana 2:28-29

Watoto Wa Mungu

2:28 Kol 3:4; 1Yn 3:2; Efe 3:12; 1The 2:19Sasa basi, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake wakati wa kuja kwake.

2:29 1Yn 3:7; Mdo 22:14; Yn 1:13Kama mkijua kuwa yeye ni mwenye haki, mwajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.

Read More of 1 Yohana 2

1 Yohana 3:1-10

3:1 Yn 3:16; 15:21Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 3:2 Rum 8:29; 2Pet 1:4; Za 17:15Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. 3:3 2Kor 7:1; 2Pet 3:13, 14Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.

3:4 1Yn 5:17; Mt 7:23; Rum 4:15Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi. 3:5 2Kor 5:21; 1Yn 1:2; Isa 53:5, 6, 11; 1Tim 1:15; Ebr 1:3; 9:26; 1Pet 2:24Lakini mwajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi, wala ndani yake hamna dhambi. 3:6 1Yn 5:18; 3Yn 1; 1Yn 2:4Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua.

3:7 1Yn 2:1; 2:26; 2:29Watoto wapendwa, mtu yeyote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki. 3:8 Yn 1:13; Za 119:3; 1Pet 1:23Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili aziangamize kazi za ibilisi. 3:9 Yn 1:13; 1Yn 3:6; Za 119:3; 1Yn 5:18; 1Pet 1:23Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. 3:10 1Yn 3:1, 2; Yn 1:12; 1Yn 3:8; 4:8; 2:9Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na pia watoto wa ibilisi. Yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Read More of 1 Yohana 3