1 Yohana 2:12-27 NEN

1 Yohana 2:12-27

2:12 1Yn 2:9; 3:23Nawaandikia ninyi, watoto wadogo,

kwa sababu dhambi zenu

zimesamehewa kwa ajili ya Jina lake.

2:13 Mt 5:37; Yn 1:1; 16:33; 1Yn 2:14; 2:13Nawaandikia ninyi, akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana

kwa sababu mmemshinda yule mwovu.

Nawaandikia ninyi watoto wadogo,

kwa sababu mmemjua Baba.

2:14 Efe 6:10; Yn 5:38; 1Yn 1:10Nawaandikia ninyi akina baba,

kwa sababu mmemjua

yeye aliye tangu mwanzo.

Nawaandikia ninyi vijana,

kwa sababu mna nguvu,

na neno la Mungu linakaa ndani yenu,

nanyi mmemshinda yule mwovu.

Msiupende Ulimwengu

2:15 Rum 12:2; Yak 4:4Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake. 2:16 Efe 2:8; Mit 27:20Kwa maana kila kitu kilichomo ulimwenguni, yaani tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima, havitokani na Baba bali hutokana na ulimwengu. 2:17 Ebr 12:27; Mt 12:50; 1Kor 7:31; Yak 1:10; 4:14; 1Pet 1:24Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

Onyo Dhidi Ya Wapinga Kristo

2:18 1Yn 4:1; 2Yn 7Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho. 2:19 Mk 1:24; Yer 31:34Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.

2:20 1Yn 2:27; 2Kor 1:21; Mk 1:24; Yer 31:34; Mt 13:11; Yn 14:26Lakini ninyi mmetiwa mafuta na yeye Aliye Mtakatifu, nanyi nyote mnaijua kweli. 2:21 2Pet 1:12; Yud 5Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli. 2:22 1Yn 4:13; 2Yn 7Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. 2:23 Yn 14:7; 2Yn 9Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba. Yeyote anayemkubali Mwana anaye na Baba pia.

2:24 2Yn 9Hakikisheni kwamba lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu. Kama lile mlilosikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 2:25 Mt 25:46; Yn 17:3; 1Yn 1:2; 5:11Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele.

2:26 1Yn 3:7; 2Yn 7Nawaandikia mambo haya kuhusu wale watu ambao wanajaribu kuwapotosha. 2:27 1Yn 2:20; Yer 31:33, 34; Ebr 8:10, 11; Yn 14:26; 16:13Nanyi, upako mlioupata kutoka kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake.

Read More of 1 Yohana 2