1 Wakorintho 9:19-27, 1 Wakorintho 10:1-13 NEN

1 Wakorintho 9:19-27

9:19 2Kor 4:5; Gal 5:13; Mt 18:15; 1Pet 3:1Ingawa mimi ni huru, wala si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya kuwa mtumwa wa kila mtu, ili niweze kuwavuta wengi kadri iwezekanavyo. 9:20 Mdo 16:3; 21:20-26; Rum 11:14; 2:12Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa watu wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama aliye chini ya sheria (ingawa mimi siko chini ya sheria), ili niweze kuwapata wale walio chini ya sheria. 9:21 Rum 2:12-14; Gal 6:2Kwa watu wasio na sheria nilikuwa kama asiye na sheria (ingawa siko huru mbali na sheria ya Mungu, bali niko chini ya sheria ya Kristo), ili niweze kuwapata wale wasio na sheria. 9:22 Rum 14:1; 1Kor 2:3; 10:33; Rum 11:14Kwa walio dhaifu nilikuwa dhaifu, ili niweze kuwapata walio dhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote niweze kuwaokoa baadhi yao. Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nipate kushiriki baraka zake.

9:24 Flp 3:14; Kol 2:18; Gal 2:2; 5:7; Flp 2:16; 2Tim 4:7; Ebr 12:1Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa jinsi ambavyo mtapata tuzo.

9:25 2Tim 2:5; 4:8; Yak 1:12; 1Pet 5:4; Ufu 2:10; 3:11Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji isiyodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji idumuyo milele. 9:26 1Tim 6:12; 2Kor 2:5; 1Kor 9:24Kwa hiyo mimi sikimbii kama mtu akimbiaye bila lengo, sipigani kama mtu anayepiga hewa, 9:27 Rum 8:12; 8:13; Kol 3:5; Rum 6:18-19; Yer 6:30; 2Kor 13:5, 6; Lk 10:7la, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha ili nikiisha kuwahubiria wengine, mimi nisiwe mtu wa kukataliwa.

Read More of 1 Wakorintho 9

1 Wakorintho 10:1-13

Onyo Kutoka Historia Ya Waisraeli

10:1 Rum 11:25; Kut 13:21; Za 105:39; Kut 14:22-29; Za 66:6Ndugu zangu, sitaki mkose kufahamu ukweli huu kwamba baba zetu walikuwa wote chini ya wingu na kwamba wote walipita katikati ya bahari. 10:2 Rum 6:3Wote wakabatizwa kuwa wa Mose ndani ya lile wingu na ndani ya ile bahari. 10:3 Yn 6:31; Kut 16:15, 35; Neh 9:15, 20; Za 78:24Wote walikula chakula kile kile cha roho, 10:4 Kut 17:6; Hes 20:11; Za 78:15na wote wakanywa kile kile kinywaji cha roho, kwa maana walikunywa kutoka ule mwamba wa roho uliofuatana nao, nao ule mwamba ulikuwa Kristo. 10:5 Hes 14:29; Ebr 3:17; Yud 5Lakini Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo miili yao ilitapakaa jangwani.

10:6 1Kor 9:11; Hes 11:4, 34Basi mambo haya yalitokea kama mifano ili kutuzuia tusiweke mioyo yetu katika mambo maovu kama wao walivyofanya. 10:7 Kut 32:4-19; 1Kor 9:14; Kut 32:6Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyokuwa, kama ilivyoandikwa, “Watu waliketi chini kula na kunywa, kisha wakainuka kucheza na kufanya sherehe za kipagani.” 10:8 Hes 25:1-9Wala tusifanye uzinzi kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu 23,000 kwa siku moja. 10:9 Kut 17:2; Za 78:18; 95:9; 106:14; Hes 21:5-6Wala tusimjaribu Kristo, kama baadhi yao walivyofanya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10:10 Hes 16:41; 17:5, 10; 16:49; Kut 12:23; 1Nya 21:15; Ebr 11:28Msinungʼunike kama baadhi yao walivyofanya, wakaangamizwa na mharabu.

10:11 Rum 4:24; 13:11; 1Kor 10:6; 1Pet 4:7Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. 10:12 Rum 11:20; 2Kor 1:24Hivyo, yeye ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. 10:13 1Kor 1:9; 2Pet 2:9Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kutokea ili mweze kustahimili.

Read More of 1 Wakorintho 10