1 Wakorintho 9:1-18 NEN

1 Wakorintho 9:1-18

Haki Za Mtume

9:1 1Kor 1:1; 2Kor 12:12; 1Kor 15:8; 3:6; 4:15Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? 9:2 2Kor 3:2-3; 1Kor 12:12Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni mhuri wa utume wangu katika Bwana.

Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu. 9:4 Mdo 18:3; Lk 10:8; 1Kor 9:14Je, hatuna haki ya kula na kunywa? 9:5 1Kor 7:7-8; Mt 12:46; 1Kor 1:12Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini, kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa?9:5 Yaani Petro. 9:6 Mdo 4:36; 2The 3:8, 9Au ni mimi na Barnaba tu inatubidi kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?

9:7 2Tim 2:3-4; Kum 20:6; Mit 27:18; 1Kor 3:6-8Ni askari yupi aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye shamba la mizabibu na asile matunda yake? Ni nani achungaye kundi na asipate maziwa yake. Je, nasema mambo haya katika mtazamo wa kibinadamu tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? 9:9 Kum 25:4; 1Tim 5:18; Kum 22:1-4; Mit 12:10Kwa maana imeandikwa katika Sheria ya Mose: “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka.” Je, Mungu hapa anahusika na ngʼombe? 9:10 Rum 4:23-24; Mit 11:25; 2Tim 2:6Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Hakika yameandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu mtu anapolima na mpuraji akapura nafaka, wote wanapaswa kufanya hivyo wakiwa na tumaini la kushiriki mavuno. 9:11 Rum 15:27; Gal 6:6Je, ikiwa sisi tulipanda mbegu ya kiroho miongoni mwenu, itakuwa ni jambo kubwa iwapo tutavuna vitu vya mwili kutoka kwenu? 9:12 Mdo 18:3; 2Kor 6:3; 11:7-12Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi?

Lakini sisi hatukutumia haki hii. Kinyume chake, tunavumilia kila kitu ili tusije tukazuia Injili ya Kristo. 9:13 Law 6:16-26; Kum 18:1Je, hamjui kwamba, watu wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni, nao wale wahudumiao madhabahuni hushiriki kile kitolewacho madhabahuni? 9:14 1Tim 5:18; Mt 10:10; Lk 10:7; Gal 6:6; 1Tim 5:17Vivyo hivyo, Bwana ameamuru kwamba wale wanaohubiri Injili wapate riziki yao kutokana na Injili.

9:15 Mdo 18:3; 2Kor 11:9-10Lakini sijatumia hata mojawapo ya haki hizi. Nami siandiki haya nikitumaini kwamba mtanifanyia mambo hayo. Heri nife kuliko mtu yeyote kuninyima huku kujisifu kwangu. 9:16 Rum 1:14; Mdo 9:15; 26:15-18Lakini ninapohubiri Injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili! 9:17 1Kor 3:8-14; 4:1; Gal 2:7; Kol 1:25Nikihubiri kwa hiari, ninayo thawabu. Lakini kama si kwa hiari, basi ninachofanya ni kutekeleza tu uwakili niliowekewa. 9:18 2Kor 11:7; 12:13; 1Kor 10:33; 2Kor 4:5; 1Kor 7:31Basi je, thawabu yangu ni nini? Thawabu yangu ni hii: Ya kwamba katika kuhubiri Injili niitoe bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.

Read More of 1 Wakorintho 9