1 Wakorintho 7:17-35 NEN

1 Wakorintho 7:17-35

Kuishi Kama Alivyoagiza Bwana

7:17 Rum 12:3; 1Kor 4:17; 14:33; 2Kor 8:18; 11:28Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, yale Mungu aliyomwitia. Hii ni sheria ninayoiweka kwa makanisa yote. 7:18 Mdo 15:1-2; 15:19, 24; 28; Gal 5:2Je, mtu alikuwa tayari ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe. 7:19 Rum 2:25-27; Gal 5:6; 6:15; Kol 3:11Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu. 7:20 1Kor 7:24Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali aliyoitwa nayo. Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote. 7:22 Yn 8:32-36; Rum 6:22Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana akiwa mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana, kama vile yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo. 7:23 1Kor 6:20; 1Pet 1:18, 19; Law 25:42Mlinunuliwa kwa gharama; msiwe watumwa wa wanadamu. Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika wito wake alioitiwa na Mungu.

Wajane Na Wasioolewa

7:25 2Kor 8:8; 4:1; 1Tim 1:13-16Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana. 7:26 1Kor 7:1, 8Kwa sababu ya shida iliyoko kwa sasa, naona ni vyema mkibaki kama mlivyo. Je, umeolewa? Basi usitake talaka. Je, hujaoa? Usitafute mke. 7:28 1Kor 7:36Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo.

7:29 Rum 13:11-12Lakini ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa wale waliooa waishi kama wasio na wake; nao wanaoomboleza, kama ambao hawaombolezi; wenye furaha kama wasiokuwa nayo; wale wanaonunua, kama vile vitu walivyonunua si mali yao; 7:31 Ebr 12:27nao wale wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama ambao hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inapita.

7:32 1Tim 5:5Ningetaka msiwe na masumbufu. Mwanaume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza Bwana. 7:33 Lk 14:20; Efe 5:29Lakini mwanaume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mkewe, 7:34 Lk 2:37na mawazo yake yamegawanyika. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana: lengo lake ni awe mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe. 7:35 Za 86:11Ninasema haya kwa faida yenu wenyewe, sio ili kuwawekea vizuizi bali mpate kuishi kwa jinsi ilivyo vyema bila kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana.

Read More of 1 Wakorintho 7