1 Wakorintho 7:1-16 NEN

1 Wakorintho 7:1-16

Kuhusu Ndoa

7:1 1Kor 7:8, 26Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke. Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. 7:3 Kut 21:10; 1Pet 3:7Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe. Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe. 7:5 Kut 19:15; 1Sam 21:4-5; Mt 4:10; 1The 3:5Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi. 7:6 2Kor 8:8Nasema haya kama ushauri na si amri. 7:7 1Kor 9:5; Mt 19:11-12; Rum 12:6; 1Kor 12:4-11Laiti watu wangekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa kipawa chake kutoka kwa Mungu, mmoja ana kipawa cha namna hii na mwingine ana cha namna ile.

7:8 1Kor 7:1, 26Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe. 7:9 1Tim 5:14Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa.

7:10 Mal 2:14-16; Lk 16:18Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi ila ni Bwana): Mke asitengane na mumewe. 7:11 Rum 7:2-3Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.

7:12 2Kor 11:17Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache. Naye mwanamke aaminiye kama ameolewa na mwanaume asiyeamini na huyo mume anakubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimwache. 7:14 Mk 2:15Kwa maana huyo mume asiyeamini anatakaswa kupitia mkewe, naye mke asiyeamini anatakaswa kupitia mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wenu wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu. 7:15 Rum 14:19; 1Kor 14:19; 14:33Lakini kama yule asiyeamini akijitenga, basi afanye hivyo. Katika hali kama hiyo mwanamke au mwanaume aaminiye hafungwi, kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. 7:16 Rum 11:16; 1Pet 3:1Wewe mke, unajuaje kama utamwokoa mumeo? Au wewe mume unajuaje kama utamwokoa mkeo?

Read More of 1 Wakorintho 7