1 Wakorintho 2:6-16 NEN

1 Wakorintho 2:6-16

Hekima Ya Kweli Itokayo Kwa Mungu

2:6 Efe 4:13; Flp 3:15; Kol 4:12; Ebr 5:14; 6:1; Yak 1:4; 1Kor 1:20; Za 146:4Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. 2:7 Rum 16:25; Efe 3:5, 9; Kol 1:26; 2Tim 1:9Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. 2:8 1Kor 1:20; Za 24:7; Mdo 7:2; Yak 2:1Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu. 2:9 Isa 64:4; 65:17Lakini ni kama ilivyoandikwa:

“Hakuna jicho limepata kuona,

wala sikio limepata kusikia,

wala hayakuingia moyoni wowote,

yale Mungu amewaandalia

wale wampendao”:

2:10 Mt 13:11; 2Kor 12:1-7; Gal 1:12; 2:2; Efe 3:3-5; Yn 14:26Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa Roho wake.

Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu. 2:11 Yer 17:9; Mit 20:27Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 2:12 Rum 8:15; 1Kor 1:20-27; Yak 2:5Basi hatukupokea roho ya dunia bali Roho atokaye kwa Mungu, ili tuweze kuelewa kile kipawa ambacho Mungu ametupatia bure. 2:13 1Kor 1:17Haya ndiyo tusemayo, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua kweli za kiroho kwa maneno ya kiroho. 2:14 Yn 14:17; 1Kor 3:1Mtu ambaye hana Roho hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni. 2:15 1Kor 3:1; Gal 6:1Mtu wa kiroho hubainisha mambo yote, lakini yeye mwenyewe habainishwi na mtu yeyote.

2:16 Isa 40:13; Rum 11:34; Yn 15:15“Kwa maana ni nani aliyefahamu mawazo ya Bwana

ili apate kumfundisha?”

Lakini sisi tunayo mawazo ya Kristo.

Read More of 1 Wakorintho 2