1 Wakorintho 16:5-24 NEN

1 Wakorintho 16:5-24

Mahitaji Binafsi

16:5 1Kor 4:19; Mdo 16:9Baada ya kupitia Makedonia nitakuja kwenu, maana ninakusudia kupitia Makedonia. 16:6 Rum 15:24; Tit 3:13Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo. 16:7 Mdo 18:21Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu; natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana akipenda. 16:8 Mdo 18:19; 2:1Lakini nitakaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste, 16:9 Mdo 14:27; 2Kor 2:12; Kol 4:3; Ufu 3:8; Mdo 19:9kwa maana mlango mkubwa umefunguliwa kwangu kufanya kazi yenye matunda, nako huko kuna adui wengi wanaonipinga.

16:10 Mdo 16:1; 19:22; Rum 16:21; Flp 2:20, 22; 1The 3:2Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, hakikisheni kwamba hana hofu yoyote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo. 16:11 1Tim 4:12; 2Kor 1:16; 3Yn 6; Mdo 19:9Basi asiwepo mtu atakayekataa kumpokea. Msafirisheni kwa amani ili aweze kunijia tena. Namtarajia pamoja na ndugu.

16:12 Mdo 18:24; 1Kor 1:12Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kabisa kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi.

Maneno Ya Mwisho

16:13 1Kor 1:8; 2Kor 1:21; Gal 5:1; Flp 1:27; 1The 3:8; Tit 1:9; Efe 6:10Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, kuweni mashujaa kuweni hodari. 16:14 1Kor 14:1Fanyeni kila kitu katika upendo.

16:15 1Kor 1:6; Rum 16:5; Mdo 18; 12; 24; 17; 9:13Ninyi mnajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefana ndio waliokuwa wa kwanza kuamini katika Akaya, nao wamejitoa kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu. Ndugu nawasihi, 16:16 1The 5:12; Ebr 13:17mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii. 16:17 2Kor 11:9; Flp 2:30Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. 16:18 Rum 15:32; Flp 1:7; 2:29Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa.

Salamu Za Mwisho

16:19 Mdo 2:9; 18:2; Rum 16:5Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila,16:19 Prisila kwa Kiyunani ni Priska, hivyo tafsiri nyingine zimemuita Priska. pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu sana katika Bwana. 16:20 Rum 16:16; 2Kor 13:12; 1Pet 5:14Ndugu wote walioko hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.

16:21 Gal 6:11; Kol 4:18; 2The 3:17Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe.

16:22 Efe 6:24; Rum 9:3; Ufu 22:20Kama mtu yeyote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo.16:22 Kwa Kiaramu ni Marana tha.

16:23 Rum 16:20Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.

Upendo wangu uwe nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amen.

Read More of 1 Wakorintho 16