1 Wakorintho 15:50-58, 1 Wakorintho 16:1-4 NEN

1 Wakorintho 15:50-58

15:50 Efe 6:12; Ebr 2:14; Mt 25:34Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika. 15:51 1Kor 13:2; 14:2; Mt 9:24; 2Kor 5:4; Flp 3:21Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 15:52 Mt 24:31; Yn 5:25ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 15:53 2Kor 5:2-4Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa. 15:54 Isa 25:8; Ebr 2:14; Ufu 20:14Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

15:55 Hos 13:14; Isa 25:8“Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako?

Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

15:56 Rum 5:12; 14:15Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. 15:57 2Kor 2:14; Rum 8:37; Ebr 2:14-15Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

15:58 1Kor 16:10; Isa 65:23Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.

Read More of 1 Wakorintho 15

1 Wakorintho 16:1-4

Changizo Kwa Ajili Ya Watakatifu

16:1 Mdo 24:17; 9:13; 16:6Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. 16:2 Mdo 20:7; 2Kor 9:4-5Siku ya kwanza ya kila juma, kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake na fedha hizo aziweke akiba, ili nitakapokuja pasiwe na lazima ya kufanya mchango. 16:3 2Kor 3:1; 8:18-19Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu. 16:4 2Kor 8:4, 19Kama ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami.

Read More of 1 Wakorintho 16