1 Wakorintho 15:1-34 NEN

1 Wakorintho 15:1-34

Kufufuka Kwa Kristo

15:1 Isa 40:9; Rum 2:16; 1Kor 3:6Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. 15:2 Rum 1:16; 11:22Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

15:3 Gal 1:12; 1Kor 11:2; Isa 53:5; Yn 1:29; Gal 1:4; 1Pet 2:24; Mt 26:24; Lk 24:27; Mdo 17:2; 26:22; 23Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, 15:4 Mt 27:59-61; Mdo 2:24; Mt 16:21; Yn 2:21-22ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko, 15:5 Lk 24:34-43; Mk 16:14na kwamba alimtokea Kefa,15:5 Yaani Petro. kisha akawatokea wale kumi na wawili. 15:6 Mt 9:24Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala. 15:7 Mdo 15:13; Lk 24:33-37; Mdo 1:3-4Ndipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote. 15:8 Mdo 9:3-6; 1Kor 9:1; Gal 1:16Mwisho wa wote, akanitokea mimi pia, ambaye ni kama aliyezaliwa si kwa wakati wake.

15:9 2Kor 12:11; Efe 3:8; 1Tim 1:15; Mdo 8:3; 1Kor 10:32Kwa maana mimi ndiye mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 15:10 Rum 3:24; 12:3; 2Kor 11:23; Kol 1:29; Flp 2:13Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. 15:11 Gal 2:6Hivyo basi, kama ilikuwa mimi au wao, hili ndilo tunalohubiri, na hili ndilo mliloamini.

Ufufuo Wa Wafu

15:12 Yn 11:24; Mdo 17:32; 23:8; 2Tim 2:18Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo hakufufuliwa. 15:14 1The 4:14Tena ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. 15:15 Mdo 2:24; 4:10, 33; 13:30Zaidi ya hayo, twaonekana kuwa mashahidi wa uongo kuhusu Mungu, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu kwamba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, lakini hilo haliwezi kuwa kweli kama wafu hawafufuliwi. 15:16 1Kor 6:14Kwa kuwa kama wafu hawafufuliwi, basi hata Kristo hajafufuka. 15:17 Rum 4:25Tena kama Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni batili; nanyi bado mko katika dhambi zenu. 15:18 Mt 9:24Hivyo basi, wote waliolala katika Kristo wamepotea. 15:19 1Kor 4:9Ikiwa tumaini letu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wote.

15:20 1Pet 1:3; Mdo 26:23; Ufu 1:5; Mt 9:24Lakini kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala. 15:21 Rum 5:12Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 15:22 Rum 5:14-18; 1Kor 6:14Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai. 15:23 1The 2:19; 1Kor 3:23Lakini kila mmoja kwa wakati wake: Kristo, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja. 15:24 Dan 2:44; 7:14; 2Pet 1:11; Rum 8:38Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. 15:25 Isa 9:7; 52:7; Mt 22:44Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. 15:26 2Tim 1:10; Ufu 20:14; 21:4Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti. 15:27 Za 8:6; Mt 22:44; 28:18Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa. 15:28 Flp 3:21; 1Kor 3:23Atakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.

Basi kama hakuna ufufuo, watafanyaje wale wabatizwao kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa ajili yao? 15:30 2Kor 11:26Nasi kwa upande wetu kwa nini tunajihatarisha kila saa? 15:31 Rum 8:36Kama majivuno yangu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu ni kweli, ndugu zangu, ninakufa kila siku. 15:32 2Kor 1:8; Mdo 18:19; Isa 22:13; Lk 12:19Kama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi,

“Tuleni na kunywa,

kwa kuwa kesho tutakufa.”

15:33 1Kor 6:9; Mit 22:24-25Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 15:34 Gal 4:8; 1Kor 4:8; 4:14Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, wala msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.

Read More of 1 Wakorintho 15