1 Wakorintho 14:20-40 NEN

1 Wakorintho 14:20-40

14:20 1Kor 3:11; Efe 4:14; Ebr 5:12-13; 1Pet 2:2; Yer 4:22; Mt 10:16; Rum 16:19Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima. 14:21 Yn 10:34; Kum 28:49; Isa 28:11-12Katika Sheria imeandikwa kwamba:

“Kupitia kwa watu wenye lugha ngʼeni

na kupitia midomo ya wageni,

nitasema na watu hawa,

lakini hata hivyo hawatanisikiliza,”

asema Bwana.

14:22 1Kor 14:1Basi kunena kwa lugha ni ishara, si kwa watu waaminio, bali kwa wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio. 14:23 Mdo 2:13Kwa hiyo kama kanisa lote likikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioelewa wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu? 14:24 Mdo 4:13Lakini kama mtu asiyeamini au asiyeelewa akiingia wakati kila mtu anatoa unabii, ataaminishwa na watu wote kuwa yeye ni mwenye dhambi na kuhukumiwa na wote, 14:25 Rum 2:16; Zek 8:23; Isa 45:14nazo siri za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akikiri, “Kweli Mungu yuko katikati yenu!”

Kumwabudu Mungu Kwa Utaratibu

14:26 Kum 7:1; 1Kor 12:7-10; Efe 5:19; Rum 14:19Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kanisa. Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu si zaidi, mmoja baada ya mwingine na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.

14:29 1Kor 13:2; 12:10Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo. 14:30 1The 5:19, 20Kama mtu yeyote aliyeketi karibu, akipata ufunuo, basi yule wa kwanza na anyamaze. Kwa maana wote mnaweza kutoa unabii, mmoja baada ya mwingine, ili kila mtu apate kufundishwa na kutiwa moyo. 14:32 1Yn 4:1Roho za manabii huwatii manabii. 14:33 Rum 15:33; 1Kor 7:17; 10:32; Mdo 9:13Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani.

Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu, 14:34 1Kor 11:5, 13; Efe 5:22; 1Tim 2:11-12wanawake wanapaswa kuwa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria isemavyo. 14:35 1Tim 2:11-12; Mwa 3:16Kama wakitaka kuuliza kuhusu jambo lolote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani.

14:36 Ebr 4:12Je, neno la Mungu lilianzia kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia? 14:37 Mdo 11:27; 1Kor 13:2; 2Kor 10:7; 1Kor 2:15; 1Yn 4:6Kama mtu yeyote akidhani kwamba yeye ni nabii, au ana karama za rohoni, basi na akubali kwamba haya ninayoandika ni maagizo kutoka kwa Bwana. Kama mtu akipuuza jambo hili yeye mwenyewe atapuuzwa.

14:39 1Kor 12:31; Efe 4:11Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha. 14:40 Kol 2:5Lakini kila kitu kitendeke kwa heshima na kwa utaratibu.

Read More of 1 Wakorintho 14