1 Wakorintho 14:1-19 NEN

1 Wakorintho 14:1-19

Karama Za Unabii Na Lugha

14:1 1Kor 16:14; 12:31; Efe 4:11Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii. 14:2 Mk 16:17; 1Kor 13:2Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho. 14:3 Rum 14:19; 1Kor 14:31; 14:4, 5, 12Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji. 14:4 Mk 16:17; 1Kor 13:2Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa. 14:5 Hes 11:29; 1Kor 1:3Ningependa kila mmoja wenu anene kwa lugha lakini ningependa zaidi nyote mtoe unabii. Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa atafsiri, ili kanisa lipate kujengwa.

14:6 Efe 1:17; 2Kor 8:7; Rum 6:17Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho? Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, kama vile filimbi au kinubi, mtu atajuaje ni wimbo gani unaoimbwa kusipokuwa na tofauti ya upigaji? 14:8 Hes 10:9; Yer 4:19Tena kama tarumbeta haitoi sauti inayoeleweka, ni nani atakayejiandaa kwa ajili ya vita? Vivyo hivyo na ninyi, kama mkinena maneno yasiyoeleweka katika akili, mtu atajuaje mnalosema? Kwa maana mtakuwa mnasema hewani tu. Bila shaka ziko sauti nyingi ulimwenguni, wala hakuna isiyo na maana. 14:11 Mwa 11:7Basi kama sielewi maana ya hiyo sauti, nitakuwa mgeni kwa yule msemaji, naye atakuwa mgeni kwangu. 14:12 1Kor 12:1Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani kuwa na karama za rohoni, jitahidini kuzidi sana katika karama kwa ajili ya kulijenga kanisa.

14:13 1Kor 14:2Kwa sababu hii, yeye anenaye kwa lugha na aombe kwamba apate kutafsiri kile anachonena. 14:14 1Kor 14:2Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu inaomba, lakini akili yangu haina matunda. 14:15 Efe 5:19; Kol 3:16Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, na pia nitaomba kwa akili yangu. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. 14:16 Kum 27:15-26; 1Nya 16:36; Neh 8:6; Za 106:48; Ufu 5:14; 7:12; Mt 14:19; 1Kor 11:24Ikiwa unabariki kwa roho, mtu mwingine atakayejikuta miongoni mwa hao wasiojua, atawezaje kusema “Amen” katika kushukuru kwako, wakati haelewi unachosema? 14:17 1Kor 14:3Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, sawa, lakini huyo mtu mwingine hajengeki.

Namshukuru Mungu kwamba mimi nanena kwa lugha kuliko ninyi nyote. 14:19 1Kor 14:6Lakini ndani ya kanisa ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno 10,000 kwa lugha.

Read More of 1 Wakorintho 14