1 Wakorintho 12:27-31, 1 Wakorintho 13:1-13 NEN

1 Wakorintho 12:27-31

12:27 Efe 1:23; 4:12; Kol 1:18, 24; Rum 12:5Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili. 12:28 1Kor 10:32; Efe 4:11; Mk 16:17; Rum 12:6-8Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha. Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza? 12:30 1Kor 12:10Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri? 12:31 1Kor 14:1, 39Basi tamanini sana karama zilizo kuu.

Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.

Read More of 1 Wakorintho 12

1 Wakorintho 13:1-13

Karama Ya Upendo

13:1 Mk 16:17; 1Kor 13:8Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo. 13:2 Efe 4:11; Mdo 11:27; 1Kor 14:2; 2Kor 8:7; 1Kor 12:9; Mt 17:20; 21:21Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 13:3 Lk 19:8; Mdo 2:45; Dan 3:28Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.

13:4 1The 5:14; 1Kor 5:2Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. 13:5 1Kor 10:24; Mt 5:22; Ay 14:16-17; Mit 10:12; 7:19; 1Pet 4:8Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya. 13:6 2The 2:12; 2Yn 4; 1:3-4Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli. 13:7 1Kor 13:8, 13; Mit 10:12; 1Kor 9:12; Rum 15:1Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

13:8 1Kor 13:2; 1Pet 4:8Upendo haushindwi kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; zikiwepo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatapita. 13:9 1Kor 8:2Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu. 13:10 Flp 3:12Lakini ukamilifu ukija, yale yasiyo kamili hutoweka. 13:11 Za 131:2Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, niliwaza kama mtoto, nilifikiri kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. 13:12 Ay 26:14; 36:26; Mwa 32:30; Ay 19:26; 1Yn 3:2; 1Kor 8:2; 8:3; Gal 4:9Kwa maana sasa tunaona taswira kama kwa kioo, lakini wakati huo tutaona wazi. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile mimi ninavyofahamika kikamilifu.

13:13 Rum 5:2-5; Gal 5:5-6; Efe 4:25; Kol 1:4-5; 1The 1:3; Ebr 6:10-12; Mt 22:37-40; 1Kor 16:14; Gal 5:6; 1Yn 4:7-12, 16Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.

Read More of 1 Wakorintho 13