1 Wakorintho 10:14-33, 1 Wakorintho 11:1 NEN

1 Wakorintho 10:14-33

Karamu Za Sanamu Na Meza Ya Bwana

10:14 Ebr 6:9; 1Pet 2:11; 1Yn 2:9; 5:21; Yud 3Kwa hiyo wapenzi wangu, zikimbieni ibada za sanamu. Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 10:16 Mt 14:19; 26:26-28; 1Kor 11:25Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 10:17 Rum 12:5; 1Kor 12:27Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja.

10:18 Law 7:6, 14, 15Waangalieni watu wa Israeli: Je, wale wote walao dhabihu si ni wale watendao kazi madhabahuni? 10:19 1Kor 8:4; Rum 12:5; 1Kor 12:27Je, nina maana kwamba kafara iliyotolewa kwa sanamu ni kitu chenye maana yoyote? Au kwamba sanamu ni kitu chenye maana yoyote? 10:20 Kum 32:17; Law 17:7; Za 107:37; Ufu 9:20La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani. 10:21 2Kor 6:15-16; Kum 32:38; Mal 1:7, 12Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani pia. 10:22 Kum 32:16, 21; 1Fal 14:22; Za 78:58; Yer 44:8; Mhu 6:10; Isa 45:9Je, tunataka kuamsha wivu wa Bwana? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?

Fanyeni Yote Kwa Utukufu Wa Mungu

10:23 1Kor 6:12“Vitu vyote ni halali,” lakini si vitu vyote vilivyo na faida. “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote vinavyojenga. 10:24 Rum 15:1-2; 1Kor 13:5; Flp 2:4, 21Mtu yeyote asitafute yaliyo yake mwenyewe, bali kila mtu atafute yale yanayowafaa wengine.

10:25 Mdo 10:15; 1Kor 8:7Kuleni chochote kinachouzwa sokoni, bila kuuliza swali lolote kwa ajili ya dhamiri. 10:26 Za 24:1; Kut 9:29; 19:5; Ay 41:11; Za 50:12; 1Tim 4:4Kwa maana, “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.”

10:27 Lk 10:7Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 10:28 1Kor 8:7, 10-12; Kum 10:14Lakini kama mtu yeyote akikuambia, “Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri. Nina maana dhamiri ya huyo aliyekuambia, wala si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 10:30 Rum 14:6; 1Tim 4:3, 4Kama nikila kwa shukrani, kwa nini nashutumiwa kwa kile ambacho kwa hicho ninamshukuru Mungu?

10:31 Zek 14:21; Kol 3:17; 1Pet 4:11Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 10:32 Mt 5:29; Mdo 24:16; 2Kor 6:3; 1Kor 11:16-22; 15:9; 1Tim 3:5Msiwe kikwazo kwa mtu yeyote, wawe Wayahudi au Wayunani, au kwa kanisa la Mungu, 10:33 Rum 15:2; 1Kor 9:22; Rum 11:14kama hata mimi ninavyojaribu kumpendeza kila mtu kwa kila namna. Kwa maana sitafuti mema kwa ajili yangu mwenyewe bali kwa ajili ya wengi, ili waweze kuokolewa.

Read More of 1 Wakorintho 10

1 Wakorintho 11:1

11:1 1Kor 4:16; Rum 15:13; 1Pet 2:12Igeni mfano wangu, kama ninavyouiga mfano wa Kristo.

Read More of 1 Wakorintho 11