1 Nyakati 7:1-40, 1 Nyakati 8:1-40 NEN

1 Nyakati 7:1-40

Wana Wa Isakari

7:1 Mwa 30:18; Hes 26:23; Mwa 46:13Wana wa Isakari walikuwa:

Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.

7:2 2Sam 24:1-2; 1Nya 21:1-5; 27:1Wana wa Tola walikuwa:

Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.

7:3 1Nya 5:24Mwana wa Uzi alikuwa:

Izrahia.

Wana wa Izrahia walikuwa:

Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.

Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.

Wana Wa Benyamini

7:6 Mwa 46:21; Hes 26:38Wana watatu wa Benyamini walikuwa:

Bela, Bekeri na Yediaeli.

Wana wa Bela walikuwa:

Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.

Wana wa Bekeri walikuwa:

Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. 7:9 Kum 10:8Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.

Mwana wa Yediaeli alikuwa:

Bilhani.

Wana wa Bilhani walikuwa:

Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.

7:12 Hes 26:38-39Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.

Wana Wa Naftali

7:13 Mwa 30:8; 46:24Wana wa Naftali walikuwa:

Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.

Wana Wa Manase

7:14 Mwa 41:51; Yos 17:1; Hes 26:30Wana wa Manase walikuwa:

Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. 7:15 Hes 26:33; 36:1-12; 27:1-11Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu. Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.

7:17 Hes 26:30; 1Sam 12:11Mwana wa Ulamu alikuwa:

Bedani.

Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. 7:18 Yos 17:2Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.

Wana wa Shemida walikuwa:

Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.

Wana Wa Efraimu

7:20 Mwa 41:52; Hes 26:35; Mwa 48:14-20; Kum 33:13, 17; Za 60:7; 108:8Wana wa Efraimu walikuwa:

Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,

Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,

Eleada akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Zabadi,

na Zabadi akamzaa Shuthela.

Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 7:22 Mwa 37:34-35; Yos 7:6; 2Sam 3:31; Ay 2:11; Za 69:11; Yoe 2:13; Yn 1:19Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 7:23 Mwa 35:18; 1Sam 4:21; 1Nya 4:9Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 7:24 Yos 10:10; 16:3, 5; 16:3; 1Sam 13:18; 2Nya 8:5Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.

Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,

Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,

Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi,

Amihudi akamzaa Elishama, 7:27 Hes 13:8, 16Elishama akamzaa Nuni,

Nuni akamzaa Yoshua.

7:28 Yos 10:33; 16:7Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. 7:29 Yos 17:11; 11:2; 1Fal 9:15; Amu 1:22-29Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.

Wana Wa Asheri

7:30 Mwa 40:17; Hes 26:44; Mwa 49:20; Kum 33:24Wana wa Asheri walikuwa:

Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.

Wana wa Beria walikuwa:

Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.

Wana wa Yafleti walikuwa:

Pasaki, Bimhali na Ashvathi.

Hawa walikuwa wana wa Yafleti.

Wana wa Shemeri walikuwa:

Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.

Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:

Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

Wana wa Sofa walikuwa:

Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani7:37 Kwa jina lingine Yetheri. na Beera.

Wana wa Yetheri walikuwa:

Yefune, Pispa na Ara.

Wana wa Ula walikuwa:

Ara, Hanieli na Risia.

7:40 Kum 2:14Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.

Read More of 1 Nyakati 7

1 Nyakati 8:1-40

Ukoo Wa Sauli Mbenyamini

8:1 Mwa 46:21; 1Nya 7:6; Hes 26:38Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,

Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,

Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.

8:3 Mwa 46:21Wana wa Bela walikuwa:

Adari, Gera, Abihudi, 8:4 2Sam 23:9Abishua, Naamani, Ahoa, Gera, Shefufani na Huramu.

8:6 Amu 3:12-30; 1Nya 2:52; Neh 6:2Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:

Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.

Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara. Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.

8:12 Ezr 2:33; Neh 7:37Wana wa Elpaali walikuwa:

Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka), 8:13 Yos 10:12; Yn 11:22; Yos 19:42na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.

Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, Zebadia, Aradi, Ederi, Mikaeli, Ishpa, na Yoha.

Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.

Yakimu, Zikri, Zabdi, Elienai, Silethai, Elieli, Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.

Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, Abdoni, Zikri, Hanani, Hanania, Elamu, Anthothiya, Ifdeya na Penueli.

Shamsherai, Sheharia, Athalia, Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.

Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

8:29 Yos 9:3; 1Nya 9:35Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.

Mke wake aliitwa Maaka. Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 8:31 1Nya 9:37Gedori, Ahio, Zekeri, na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.

8:33 1Sam 28:19; 9:1; 14:49; 2Sam 2:8; Mdo 13:21Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.

8:34 2Sam 9:12; 4:4; 21:7-14Yonathani akamzaa:

Merib-Baali,8:34 Merib-Baali maana yake ni Baali na Ashindane naye (Amu 6:32); ni jina lingine la mwana wa Yonathani, Mefiboshethi ambalo nalo maana yake ni Mtu wa Aibu (ona 2Sam 4:4). naye Merib-Baali akamzaa Mika.

Wana wa Mika walikuwa:

Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.

Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.

Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:

Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.

Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:

Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 8:40 Hes 26:38; 1Nya 12:2; 2Nya 11:1; 13:3; Neh 4:13; Wim 3:7-8; Efe 6:11-20Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.

Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.

Read More of 1 Nyakati 8