1 Nyakati 4:9-43, 1 Nyakati 5:1-26 NEN

1 Nyakati 4:9-43

4:9 Mwa 34:19; Za 112:6; Mit 10:7; Mwa 3:16Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” 4:10 Mwa 12:8; 1Nya 16:8; Ay 12:4; 22:27; Isa 12:4; 1Fal 3:7-13; Mt 7:7-11; Za 21:4; 65:2Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni. Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka.

4:13 Yos 15:17Wana wa Kenazi walikuwa:

Othnieli na Seraya.

Wana wa Othnieli walikuwa:

Hathathi na Meonathai. 4:14 Neh 11:35Meonathai akamzaa Ofra.

Seraya akamzaa Yoabu,

baba wa Ge-Harashimu.4:14 Maana yake Bonde la Mafundi. Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi.

Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu:

Iru, Ela na Naamu.

Naye mwana wa Ela alikuwa:

Kenazi.

Wana wa Yahaleleli walikuwa:

Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.

4:17 Kut 15:20Wana wa Ezra walikuwa:

Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa. 4:18 Yos 15:34Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.

4:19 Yos 15:44; Kum 3:14Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa:

baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.

Wana wa Shimoni walikuwa:

Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni.

Wazao wa Ishi walikuwa:

Zohethi na Ben-Zohethi.

4:21 Mwa 38:5Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa:

Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea, 4:22 2Sam 8:2Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.) Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme.

Simeoni

4:24 Mwa 21:14; Yos 15:26Wazao wa Simeoni walikuwa:

Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.

Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.

Wazao wa Mishma walikuwa:

Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.

Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda. Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali, 4:29 Yos 15:29Bilha, Esemu, Toladi, Bethueli, Horma, Siklagi, 4:31 Yos 15:35Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi. 4:32 Hes 34:11; Yos 15:42Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani; jumla miji mitano: pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baali. Haya yalikuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao.

Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia, Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli. Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya, Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.

Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana, 4:39 Yos 15:58wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. 4:40 Amu 18:7-10; Mwa 9:22; 10:6; Za 78:51Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.

4:41 2Nya 20:1; 26:7; 2Fal 18:8Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao. 4:42 Mwa 14:6Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri. 4:43 1Sam 15:8; 2Sam 8:12Wakawaua Waamaleki waliobaki, waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo.

Read More of 1 Nyakati 4

1 Nyakati 5:1-26

Wana Wa Reubeni

5:1 Mwa 29:32; 35:22; 49:4; 48:16; 49:26; 48:5; 1Nya 26:10Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa. 5:2 Mwa 49:10; 49:12; Za 60:7; Mt 2:6; Mwa 25:31; Hes 2:3; 7:12; Za 108:8; 78:68-71; Yer 23:5-6; Mik 5:2Na ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yosefu.) 5:3 Kut 6:19; Hes 26:5-11; 26:5; Mwa 46:9Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa:

Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.

Wazao wa Yoeli walikuwa:

Shemaya mwanawe, Gogu mwanawe;

Shimei mwanawe, Mika mwanawe,

Reaya mwanawe, Baali mwanawe,

5:6 2Fal 16:10; 2Nya 28:20; 2Fal 15:29na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni.

5:7 Mit 17; Yos 13:17Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo:

Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria, 5:8 Hes 32:34; Amu 11:26; Yos 13:17Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni. 5:9 Hes 32:26; Yos 22:9; Wim 4:1; Mik 7:14Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.

5:10 Mwa 25:12Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi.

Wana Wa Gadi

5:11 Mwa 30:11; Yos 13:24-28; Kum 3:10; Yos 13:11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.

Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.

Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba:

Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi.

Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi.

Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao.

5:16 Mit 18:21; 1Nya 27:31; Isa 35:2; 65:10Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea.

5:17 2Fal 15:32; 14:23Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

5:18 Hes 1:3Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo. 5:19 Mwa 28:15; 1Nya 1:31; Mwa 25:15Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu. 5:20 Za 46:5; 54:4; 20:7-9; 2Nya 6:34; Isa 26:3; Dan 6:23; Za 9:10; Yer 17:7-8Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea. Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000, 5:22 Kum 20:4; 2Nya 32:8; 1Nya 5:10; 2Fal 15:29na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho.

Nusu Ya Kabila La Manase

5:23 Kum 3:8, 9; Wim 4:8Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.

Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao. 5:25 2Fal 17:7; 2Nya 12:2; Kut 34; 15; Law 18:3; Yer 5:7; Kum 32:15Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao. 5:26 Isa 37:7; 2Fal 15:19; 15:29; 17:6; 18:11Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

Read More of 1 Nyakati 5