1 Nyakati 28:1-21, 1 Nyakati 29:1-30 NEN

1 Nyakati 28:1-21

Maandalizi Ya Daudi Ya Kujenga Hekalu

28:1 1Nya 11:10; 29:6; Kut 18:25; 1Nya 27:16; Yos 23:2; 24:1; 1Nya 23:2; Kum 1:15Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari.

28:2 1Sam 10:7; 1Nya 17:2; Za 132:7; Isa 60:13; Ebr 2:11; Kum 17:20; 1Nya 11:1-3; Za 22:22; 2Sam 7:2; 1Fal 8:17; 2Nya 6:7-8Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano la Bwana kwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga. 28:3 2Sam 7:5; 1Nya 22:8; 1Fal 5:3; 1Nya 17:4Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’

28:4 1Nya 17:23-27; 2Nya 6:6; 1Sam 16:1-13; Mwa 49:10; Hes 24:17-19“Hata hivyo, Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote. 28:5 1Nya 3:1; 2Sam 12:24; 1Nya 22:9; 14:4-7Miongoni mwa wanangu wote, naye Bwana amenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme wa Bwana juu ya Israeli. 28:6 2Sam 7:13; 1Nya 22:9-10Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. 28:7 1Nya 22:13; 1Fal 9:4; 11:11Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’

28:8 Kum 6:1; 4:1; 17:14-20“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la Bwana naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za Bwana Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.

28:9 1Nya 29:19; 2Nya 6:30; Za 40:16; Yer 29:13; Kum 4:31; Yos 24:20; Za 9:10; Yer 9:24; Yn 17:3; 2Fal 20:3; Za 101:2; 1Sam 16:7; 1Fal 8:39; 1Nya 29:17; Ufu 2:23; 2Nya 15:2; Mt 7:7; Yak 4:8-10“Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Bwana huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele. 28:10 1Nya 22:16; Mit 4:23Angalia basi, kwa maana Bwana amekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.”

28:11 Kut 25:9; Ebr 8:9; 1Fal 6:2Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho. 28:12 1Nya 12:18; 26:12-20Akampa vielelezo vya yote Roho alikuwa ameviweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu la Bwana na vyumba vyote vilivyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu la Bwana. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu. Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali. 28:15 Kut 25:31Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara; 28:16 Kut 25:23; 1Fal 7:48; 2Nya 4:8uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha; 28:17 Kut 27:3uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha; 28:18 Kut 30:1-10; 25:22; Eze 10:2; Za 68:17; 1Fal 6:23; Za 18:10na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano la Bwana.

28:19 1Fal 6:38; Kut 25:9; 25:40; 26:30Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwa Bwana ulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.”

28:20 2Nya 29:11; Hag 2:4; Kum 4:31; Yos 24:20; 1Fal 6:14; Ebr 13:5; Kum 31:7; Yos 1:5-7; 1Nya 22:13; 1Kor 16:13Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana Bwana aliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la Bwana itakapokamilika. 28:21 1Nya 25:1; Kut 35:25–36:5Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”

Read More of 1 Nyakati 28

1 Nyakati 29:1-30

Matoleo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Hekalu

29:1 1Fal 3:7; 2Nya 13:7; Mit 4:3; 1Nya 22:5Ndipo Mfalme Daudi akaliambia kusanyiko lote: “Mwanangu Solomoni, yeye ambaye Mungu amemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu. Kazi hii ni kubwa, kwa sababu Hekalu hili la fahari si kwa ajili ya mwanadamu bali ni kwa ajili ya Bwana. 29:2 Ezr 6:5; Ufu 21:18; Hag 2:8; Isa 54:11; 1Nya 22:2-5; Kut 28:9Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno. 29:3 2Nya 24:10; Za 28:9; 2Nya 35:8; Za 26:8; 27:4; Mit 3:9Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu: 29:4 Mwa 10:29; 1Nya 22:14; Ay 22:24; 1Fal 9:28; 2Nya 8:18talanta 3,00029:4 Talanta 3,000 za dhahabu sawa na tani 110. za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,00029:4 Talanta 7,000 za fedha ni sawa na tani 260. za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu, kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?”

29:6 1Nya 28:1; Kut 36:2; Ezr 7:15Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,00029:7 Talanta 5,000 za dhahabu ni sawa na tani 190. na darkoni 10,00029:7 Darkoni 10,000 za dhahabu ni sawa na kilo 84. za dhahabu, talanta 10,00029:7 Talanta 10,000 za fedha ni sawa na tani 375. za fedha, talanta 18,00029:7 Talanta 18,000 za shaba ni sawa na tani 675. za shaba na talanta 100,00029:7 Talanta 100,000 za chuma ni sawa na tani 3,750. za chuma. 29:8 Kut 35:27; 1Nya 26:21Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 29:9 1Fal 8:61; 2Kor 9:7Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.

Maombi Ya Daudi

29:10 1Fal 8:15-16; 2Nya 6:4; Za 72:18; Eze 3:12Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:

“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,

Mungu wa Israeli baba yetu,

tangu milele hata milele.

29:11 Za 24:8; 89:11; Mt 6:13; Ufu 5:12-13; Dan 4:34-35; 1Tim 1:17Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,

na utukufu na enzi na uzuri,

kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

ni chako wewe.

Ee Bwana, ufalme ni wako;

umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

29:12 Ezr 7:27; Mhu 5:19; 2Nya 20:6; Rum 11:36; Kum 8:18; 1Sam 2:7-8; Za 75:6; Mit 10:22; Yak 1:17Utajiri na heshima vyatoka kwako;

wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.

Mikononi mwako kuna nguvu na uweza

ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru

na kulisifu Jina lako tukufu.

“Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako. 29:15 Mwa 47:9; 23:4; Ebr 11:13; Mhu 6:12; Za 102:11; Ay 14:2; Za 39:12; 1Pet 2:11; Za 90:9; 144:4Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini. Ee Bwana Mungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako. 29:17 Mit 17:3; Yer 11:20; Za 15:1-5; Mit 11:20; Ebr 4:13; Kum 8:2; 1Sam 16:7; 1Nya 28:9; Za 7:9; Yer 17:10; Mit 16:2Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe. 29:18 Za 10:17; Yer 10:23Ee Bwana, Mungu wa baba zetu Abrahamu, Isaki na Israeli, weka shauku hii ndani ya mioyo ya watu wako daima na uifanye mioyo yao iwe na uaminifu kwako. 29:19 1Fal 8:61; Isa 38:3; 1Nya 22:14; Za 72:1Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.”

Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini Bwana Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za Bwana na mfalme.

Solomoni Akubalika Kuwa Mfalme

Siku ya pili yake wakamtolea Bwana dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli. 29:22 1Nya 12:40; 1Sam 2:35; 1Fal 1:33-39Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile.

Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani. 29:23 1Fal 2:12; 1Nya 17:14Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi cha Bwana kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii. 29:24 Mwa 24:2; 47:29; Eze 17:18; 2Nya 30:8Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni.

29:25 1Fal 10:7; 3:13; Mhu 2:9; 2Nya 1:12; Dan 5:18-19; Ebr 2:9Bwana akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.

Muhtasari Wa Utawala Wa Daudi

29:26 1Nya 18:14Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote. 29:27 2Sam 5:4-5; 1Fal 2:11Alitawala Israeli kwa miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.

29:28 Mwa 15:15; Mdo 13:36; 1Nya 23:1; Mwa 25:8; Hes 23:10; Ay 5:26Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

29:29 1Sam 9:9; 22:5; 2Sam 7:2; Ay 5:26Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi, 29:30 Dan 2:21pamoja na habari zote za utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, na Israeli, na falme za nchi nyingine zote.

Read More of 1 Nyakati 29