1 Nyakati 26:20-32, 1 Nyakati 27:1-34 NEN

1 Nyakati 26:20-32

Watunza Hazina Na Maafisa Wengine

26:20 2Nya 24:5; 1Nya 28:12; 22:14-16; Kum 12:6; 1Fal 7:51; 14:26; 1Nya 9:26-29; Mal 3:10; 2Nya 31:11-12Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

26:21 1Nya 6:17; 23:8; 29:8Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la Bwana.

26:23 Hes 3:27; Kut 6:18; 1Nya 23:12Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli:

26:24 1Nya 23:16-18; 24:20Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 26:25 1Nya 23:18; 24:22Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. 26:26 2Sam 8:11Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 26:27 Hes 31:50; Yos 6:19, 24; 1Nya 22:14-16; 2Nya 15:11, 18; 2Fal 12:14; 22:4-5; Neh 10:32Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana. 26:28 1Sam 9:9Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake.

26:29 Kum 17:8-13; Neh 11:16; 2Nya 19:8-11; 1Nya 23:4Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli.

26:30 1Nya 27:17Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za Bwana na utumishi wa mfalme. 26:31 1Nya 23:19; 2Sam 5:4; Isa 16:9; Yer 48:32; 1Fal 2:11; 1Nya 29:27; Yos 21:39Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 26:32 2Nya 19:11Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.

Read More of 1 Nyakati 26

1 Nyakati 27:1-34

Vikosi Vya Jeshi

Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.

27:2 2Sam 23:8; 1Nya 11:11Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake. 27:3 Mwa 38:29Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.

27:4 2Sam 23:9-20Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:5 1Fal 4:5Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. 27:6 2Sam 23:20-23Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.

27:7 2Sam 2:18; 1Nya 11:26-28; 2Sam 23:24Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:9 2Sam 23:26; 1Nya 11:28Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:11 2Sam 21; 18; 1Nya 11:29Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:12 2Sam 23:27; 1Nya 11:30-31Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:13 2Sam 23:28; 1Nya 11:36Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:14 2Sam 23:30; 1Nya 11:31Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

27:15 2Sam 23:29; Yos 15:17; Amu 3:9Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

Maafisa Wa Makabila

Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa:

Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;

kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;

27:17 1Nya 26:30; 2Sam 8:17; 1Nya 12:28kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;

kwa Aroni: Sadoki;

27:18 1Sam 16:6kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;

kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;

kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;

kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;

kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;

kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;

kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;

kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;

kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.

Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.

27:23 2Sam 24:1; 1Nya 21:2-5; Mwa 12:2; 15:5; Kut 32:13; Ebr 11:12Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 27:24 2Sam 24:15; 1Nya 21:7Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.

Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme

Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.

Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.

Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.

27:27 Wim 8:11Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.

Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.

27:28 1Fal 10:27; 2Nya 1:15Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.

Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.

Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni.

Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni.

Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.

Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.

27:31 1Nya 5:10Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.

Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi.

27:32 2Sam 21:21Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.

27:33 2Sam 15:12, 37Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.

Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. 27:34 1Sam 22:20; 2Sam 2:13; 1Nya 11:6Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.

Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.

Read More of 1 Nyakati 27