1 Nyakati 24:1-31, 1 Nyakati 25:1-31, 1 Nyakati 26:1-19 NEN

1 Nyakati 24:1-31

Migawanyo Ya Makuhani

24:1 2Nya 5:11; Ezr 6:18; Kut 6:23; Hes 3:2-4; 26:60Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 24:2 Law 10:1-2; Hes 3:4; 26:61Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. 24:3 2Sam 8:17Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. 24:5 1Nya 26:13; Mdo 1:26; Yos 18:10; Mit 16:33; 18:18Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

24:6 1Nya 18:16; Neh 8:4; 1Fal 4:3Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

24:7 Ezr 2:36; Neh 7:39; 12:6Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,

ya pili Yedaya,

24:8 Ezr 10:21; Neh 12:4-6ya tatu Harimu,

ya nne Seorimu,

ya tano Malkiya,

ya sita Miyamini,

24:10 Neh 12:4, 17; Lk 1:5ya saba Hakosi,

ya nane Abiya,

ya tisa Yeshua,

ya kumi Shekania,

ya kumi na moja Eliashibu,

ya kumi na mbili Yakimu,

ya kumi na tatu Hupa,

ya kumi na nne Yeshebeabu,

24:14 Ezr 2:37; Yer 20:1ya kumi na tano Bilga,

ya kumi na sita Imeri,

24:15 Neh 10:20ya kumi na saba Heziri,

ya kumi na nane Hapisesi,

ya kumi na tisa Pethahia,

ya ishirini Yehezkeli,

ya ishirini na moja Yakini,

ya ishirini na mbili Gamuli,

ya ishirini na tatu Delaya,

ya ishirini na nne Maazia.

24:19 1Nya 9:25; Hes 4:49; 2Fal 5:7; Lk 1:18-23Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

Walawi Waliobaki

24:20 1Nya 23:6-17Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:

Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;

kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.

Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:

Ishia alikuwa wa kwanza.

Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,

kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.

24:23 1Nya 23:19; 15:9Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;

kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.

24:25 1Nya 22:9Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;

na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.

24:26 1Nya 6:19; 23:21; Hes 3:20; Kut 6:19Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.

Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.

Wana wa Merari:

kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.

24:28 1Nya 23:22Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.

Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:

alikuwa Yerameeli.

24:30 1Nya 23:23Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.

Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

Read More of 1 Nyakati 24

1 Nyakati 25:1-31

Waimbaji

25:1 1Nya 6:31-39; 16:41-42; Neh 11:17; 1Sam 10:5; Ezr 3:10; 2Nya 5:12; 1Nya 12:28; 23:2; 15:17; Kut 15:20; Hes 11:25; Za 150:3-5; 1Kor 14:1; Ufu 15:2-4Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:

Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:

Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.

25:3 Mwa 4:21; Za 33:2Wana wa Yeduthuni walikuwa sita:

Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.

Wana wa Hemani walikuwa:

Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi. 25:5 1Sam 9:9; 2Sam 24:11; Amo 7:12; 1Pet 4:11; Isa 3:18; 1Nya 21:9; 26:28; Mwa 33:5; 1Sam 1:17; 1Nya 28:5; Za 127:3; 128:3Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

25:6 1Nya 15:16-19; 2Nya 23:18; 29:25Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. 25:7 Efe 5:19; Kol 3:16; Yak 5:13Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288. 25:8 2Nya 23:13; 1Nya 26:13Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.

25:9 1Nya 6:36-39; 25:31; Ufu 5:8; 1Nya 9:33Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, wanawe na jamaa zake, 12Ya pili ikamwangukia Gedalia, yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12Ya tatu ikamwangukia Zakuri, wanawe na jamaa zake, 12ya nne ikamwangukia Isri,25:11 Isri jina lingine ni Seri. wanawe na jamaa zake, 12ya tano ikamwangukia Nethania, wanawe na jamaa zake, 12ya sita ikamwangukia Bukia, wanawe na jamaa zake, 12ya saba ikamwangukia Yesarela,25:14 Yesarela jina lingine ni Asarela. wanawe na jamaa zake, 12ya nane ikamwangukia Yeshaya, wanawe na jamaa zake, 12ya tisa ikamwangukia Matania, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi ikamwangukia Shimei, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na moja ikamwangukia Azareli,25:18 Azareli jina lingine ni Uzieli. wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, wanawe na jamaa zake, 12Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, wanawe na jamaa zake, 12ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini ikamwangukia Eliatha, wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, wanawe na jamaa zake, 12ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, wanawe na jamaa zake, 1225:31 Ufu 4:4; 5:8; 11:6ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, wanawe na jamaa zake, 12.

Read More of 1 Nyakati 25

1 Nyakati 26:1-19

Mabawabu

26:1 1Nya 9:17; Hes 26:9-11; 2Nya 23:19; Hes 16:1-2; 1Nya 15:18; Yud 11; 1Nya 6:39Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu:

Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu.

26:2 1Nya 9:21Meshelemia alikuwa na wana wafuatao:

Zekaria mzaliwa wa kwanza,

Yediaeli wa pili,

Zebadia wa tatu,

Yathnieli wa nne,

Elamu wa tano

Yehohanani wa sita

na Eliehoenai wa saba.

Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:

Shemaya mzaliwa wa kwanza,

Yehozabadi wa pili,

Yoa wa tatu,

Sakari wa nne,

Nethaneli wa tano,

26:5 Mwa 33; 5; 2Sam 5:10; 1Nya 13:13-14; Za 127:3Amieli wa sita,

Isakari wa saba,

na Peulethai wa nane.

(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)

Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.

Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.

26:10 Kum 21:16-17; 1Nya 16:38; 5:1; Mwa 4:7; 49:3Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu.

Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 26:13 1Nya 24:5; 25:8; Mit 18:18; Yos 18:10; Yn 1:7; Mdo 1:26; 10:34; Gal 3:28; Kol 3:11Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.

26:14 1Nya 9:18-21Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.26:14 Shelemia jina lingine ni Meshelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 26:15 1Nya 13:13; 2Nya 25:24Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 26:16 1Fal 10:5; 1Nya 24:31; Neh 12:24; 2Nya 9:4; 1Nya 25:8Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.

Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.

26:19 Neh 7:1; Eze 44:11Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.

Read More of 1 Nyakati 26