1 Nyakati 22:1-19, 1 Nyakati 23:1-32 NEN

1 Nyakati 22:1-19

22:1 Kum 12:5; Mwa 28:17; 1Nya 21:18-28; 2Nya 3:1; Kum 12:5; 2Sam 24:18Ndipo Daudi akasema, “Nyumba ya Bwana Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”

Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu

22:2 Kum 20:11; 1Fal 9:21; 5:17-18; Ezr 3:7Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. 22:3 1Fal 7:47Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika. 22:4 1Fal 5:6Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi.

22:5 1Fal 3:7; 1Nya 29:1Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya Bwana inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.

22:6 Mdo 7:47Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya Bwana, Mungu wa Israeli. 22:7 1Nya 17:2; 2Sam 7:2; 1Fal 8:17; Kum 12:5-11; Mdo 7:48Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu. 22:8 1Fal 5:3; 1Nya 28:3Lakini neno hili la Bwana likanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. 22:9 Yos 14:15; 2Sam 12:24; 1Fal 4:20; 5:4; 1Nya 28:5Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake. 22:10 1Nya 17:12; 2Sam 7:13-14; 2Nya 6:15; 1Fal 5:5; 1Nya 28:6; Za 89:26-27; Ebr 1:5Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’

22:11 1Sam 18:12; Rum 8:31“Sasa, mwanangu, Bwana awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya Bwana Mungu wako, kama alivyosema utafanya. 22:12 1Fal 3:11; 2Nya 1:10; Kum 4:6Bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya Bwana Mungu wako. 22:13 1Nya 28:7; Kum 31:6-7; Yos 1:6-9; 1Fal 6:12-13; 9:4-5; Isa 3:10; 1Nya 28:20Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Bwana alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.

22:14 1Nya 29:2-5, 19“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,00022:14 Talanta 100,000 za dhahabu ni sawa na tani 3,750. za dhahabu, talanta 1,000,00022:14 Talanta 1,000,000 za fedha ni sawa na tani 37,500. za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”

22:17 1Nya 28:1-6Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe. 22:18 1Fal 8:6; Kum 12:10; Yos 22:4Akawaambia, “Je, Bwana Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya Bwana na watu wake. 22:19 2Nya 20:3; 1Fal 8:6; 2Nya 5:7; 6:11Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta Bwana Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya Bwana Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la Bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la Bwana.”

Read More of 1 Nyakati 22

1 Nyakati 23:1-32

Jamaa Za Walawi Na Utendaji Wao

23:1 1Fal 1:30-33; 1Nya 28:5; 29:28; 29:22-25Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 23:3 Hes 8:24; 4:3-49Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. 23:4 Ezr 3:8; 2Nya 19:8; Kum 16:18; Eze 44:24; Kum 16:18; 1Nya 26:29Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, 23:5 1Nya 15:16; Za 92:3; Neh 12:45; Amo 6:5; 2Nya 29:25-26na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

23:6 2Nya 23:18; 29:25; 8:14; Kut 6:16; Hes 26:57; 2Nya 35:10; 31:2; Ezr 6:18Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Wagershoni

Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:

Ladani na Shimei.

Wana wa Ladani walikuwa watatu:

Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.

Wana wa Shimei walikuwa watatu:

Shelomothi,23:9 Yaani Shelomithi; maana yake ni Mpenda amani. Hazieli na Harani.

Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.

Nao wana wa Shimei walikuwa wanne:

Yahathi, Zina,23:10 Tafsiri zingine zinamwita Ziza. Yeushi na Beria.

Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

Wakohathi

23:12 Mwa 46:11; Kut 6:18-20; 1Nya 6:2Wana wa Kohathi walikuwa wanne:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

23:13 Kut 30:7-10; 28:1; Kum 21:5; Hes 6:23; 16:40; Ebr 5:4; Hes 16:40; 1Sam 2:28Wana wa Amramu walikuwa:

Aroni na Mose.

Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele. 23:14 Kum 33:1Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.

23:15 Kut 18:4; 2:22Wana wa Mose walikuwa:

Gershomu na Eliezeri.

23:16 1Nya 26:24-28Wazao wa Gershomu:

Shebueli alikuwa wa kwanza.

Wazao wa Eliezeri:

Rehabia alikuwa wa kwanza.

Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

Wana wa Ishari:

Shelomithi alikuwa wa kwanza.

23:19 1Nya 24:23; 26:31Wana wa Hebroni walikuwa:

Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.

Wana wa Uzieli walikuwa:

Mika wa kwanza na Ishia wa pili.

Wamerari

23:21 1Nya 6:19; 24:26Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Wana wa Mahli walikuwa:

Eleazari na Kishi.

23:22 Hes 36:6Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

23:23 1Nya 24:30Wana wa Mushi:

Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.

23:24 Hes 4:3; 10:17-21Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana. Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.” Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

23:28 Neh 13:9; Mal 3:3Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu. 23:29 Kut 25:30; Law 2:4-7; 6:20-23; 19:35-36; 1Nya 9:29-32Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa. 23:30 1Nya 9:33; Ufu 5:8-14; 2Nya 31:2; 1Nya 6:31-33; Za 135:1-3; Ufu 14:3Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni 23:31 2Fal 4:23; Law 23:4; Kol 2:16; Hes 10:10; Za 81:3; Isa 1:13-14na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

23:32 Hes 1:53; 1Nya 6:48; Hes 3:6-8; 2Nya 31:2; Eze 44:14Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana.

Read More of 1 Nyakati 23