1 Nyakati 2:18-55, 1 Nyakati 3:1-24, 1 Nyakati 4:1-8 NEN

1 Nyakati 2:18-55

Kalebu Mwana Wa Hesroni

Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni. 2:19 1Nya 2:42, 50Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri. 2:20 Kut 32:2; 35:30; 2Nya 1:5Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.

2:21 Hes 21:1Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi. 2:23 Hes 32:41; 32:42; Yos 13:30; Kum 3:14(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.

2:24 1Nya 4:5; 2Nya 11:6; 20:20; 2Sam 14:2; Neh 3:5; Yer 6:1Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.

Yerameeli Mwana Wa Hesroni

Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:

Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.

Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:

Maasi, Yamini na Ekeri.

Wana wa Onamu walikuwa:

Shamai na Yada.

Wana wa Shamai walikuwa:

Nadabu na Abishuri.

Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.

Wana wa Nadabu walikuwa

Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.

Apaimu akamzaa:

Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani.

Sheshani akamzaa Alai.

Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:

Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.

Wana wa Yonathani walikuwa:

Pelethi na Zaza.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.

Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.

Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.

2:36 1Nya 11:41Atai akamzaa Nathani,

Nathani akamzaa Zabadi,

Zabadi akamzaa Eflali,

Eflali akamzaa Obedi,

Obedi akamzaa Yehu,

Yehu akamzaa Azaria,

Azaria akamzaa Helesi,

Helesi akamzaa Eleasa,

Eleasa akamzaa Sismai,

Sismai akamzaa Shalumu,

Shalumu akamzaa Yekamia,

naye Yekamia akamzaa Elishama.

Koo Za Kalebu

Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:

Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.

Hebroni alikuwa na wana wanne:

Kora, Tapua, Rekemu na Shema. Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai. 2:45 Yos 15:55; 15:58Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.

Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.

Wana wa Yadai walikuwa:

Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.

Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana. 2:49 Yos 15:31; 15:16Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa. 2:50 1Nya 4:4; 2:19Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.

Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:

Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.

Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:

Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi, 2:53 2Sam 23:38pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.

2:54 Ezr 2:22; Neh 12:28Wazao wa Salma walikuwa:

Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori, 2:55 Mwa 15:19; Amu 1:16; Yos 19:35; 2Fal 10:15, 23; Yer 35:2-19; Amu 4:11; Hes 24:21-22pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

Read More of 1 Nyakati 2

1 Nyakati 3:1-24

Wana Wa Daudi

3:1 1Nya 14:3; 14:3; 28:5; Yos 15:56; 1Sam 25:42; 27:3Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:

Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli;

wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;

3:2 1Fal 2:22wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;

wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;

3:3 2Sam 3:5wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali;

wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.

3:4 2Sam 5:4; 1Nya 29:27; 1Sam 2:11; 5:5; 1Fal 2:11Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.

Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu, 3:5 2Sam 11:3; 12:24; 1Nya 14:4nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:

mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua,3:5 Sawa na Shimea; maana yake ni Mashuhuri, Maarufu. Shobabu, Nathani na Solomoni. Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti, Noga, Nefegi, Yafia, 3:8 2Sam 5:14Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa. 3:9 2Sam 13:1; 1Nya 14:4; 2Sam 14:27Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.

Wafalme Wa Yuda

3:10 1Fal 14:21-31; 15:1-8; 2Nya 12:16; 13:1; 17:1–21:3Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu,

mwanawe huyo alikuwa Abiya,

mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati,

mwanawe huyo alikuwa Asa,

3:11 2Fal 8:16-24; 2Nya 21:1; 22:1-10; 2Fal 11:1-12mwanawe huyo alikuwa Yehoramu,

mwanawe huyo alikuwa Ahazia,

mwanawe huyo alikuwa Yoashi,

3:12 2Fal 14:1-22; 2Nya 25:1-28; 27:1; Isa 1:1; 3:13; 2Nya 28:1; Isa 1:1; 2Fal 21:1-18; 2Nya 33:1mwanawe huyo alikuwa Amazia,

mwanawe huyo alikuwa Azaria,

mwanawe huyo alikuwa Yothamu,

mwanawe huyo alikuwa Ahazi,

mwanawe huyo alikuwa Hezekia,

mwanawe huyo alikuwa Manase,

mwanawe huyo alikuwa Amoni

na mwanawe huyo alikuwa Yosia.

3:15 2Fal 23:34; Yer 37:1; 2Fal 25:3Wana wa Yosia walikuwa:

Yohanani mzaliwa wake wa kwanza,

Yehoyakimu mwanawe wa pili,

wa tatu Sedekia,

wa nne Shalumu.

3:16 2Fal 24:6, 8; Mt 1:11; 2Fal 24:18Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:

Yekonia mwanawe,

na Sedekia.

Ukoo Wa Kifalme Baada Ya Uhamisho

3:17 Ezr 3:2Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:

Shealtieli mwanawe, 3:18 Ezr 1:8; 5:14; Yer 22:30Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.

3:19 Hag 2:2; Zek 4:6; Ezr 3:2Wana wa Pedaya walikuwa:

Zerubabeli na Shimei.

Wana wa Zerubabeli walikuwa:

Meshulamu na Hanania.

Shelomithi alikuwa dada yao.

Pia walikuwepo wengine watano:

Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.

Wazao wa Hanania walikuwa:

Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.

3:22 Ezr 8:2-3Wazao wa Shekania:

Shemaya na wanawe:

Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.

Wana wa Nearia walikuwa:

Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.

Wana wa Elioenai walikuwa:

Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.

Read More of 1 Nyakati 3

1 Nyakati 4:1-8

Koo Nyingine Za Yuda

4:1 Mwa 46:12; 1Nya 2:3; Hes 26:21; Mwa 38:29; Rut 4:18Wana wa Yuda walikuwa:

Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.

Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi.

Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu:

Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. 4:4 1Nya 2:50; Rut 1:19Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha.

Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.

4:5 1Nya 2:24Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.

Wana wa Hela walikuwa:

Serethi, Sohari, Ethnani, na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.

Read More of 1 Nyakati 4