1 Nyakati 16:37-43, 1 Nyakati 17:1-27, 1 Nyakati 18:1-17 NEN

1 Nyakati 16:37-43

Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku. 16:38 1Nya 13:13; 26:4-10Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.

16:39 1Sam 2:35; 1Nya 21:29; 2Sam 8:17; Yos 9:3; 1Fal 3:4Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni 16:40 Kut 29:38; Hes 28:1-8ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli. 16:41 1Nya 15:19; 2Nya 5:13; Yak 5:11; Ezr 3:11; Neh 9:17; Za 25:10; 33:5; Yer 33:11; Yoe 2:13; Lk 3:36Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.” 16:42 2Nya 7:6Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.

16:43 2Sam 6:19-20; Mwa 18:19; Yos 24:15Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

Read More of 1 Nyakati 16

1 Nyakati 17:1-27

Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi

(2 Samweli 7:1-17)

17:1 Mdo 7:46; 1Nya 15:1Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la Bwana liko ndani ya hema.”

17:2 1Nya 22:7; 2Nya 6:7Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.” Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema:

17:4 1Nya 28:3“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo. 17:5 2Sam 6:21; Kut 40:2; 1Fal 8:4, 16Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine. Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’ 

17:7 2Sam 6:21“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 17:9 2Nya 15:2; Isa 49:17; Yer 31:12; Eze 34:14Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 17:10 Amu 2:16na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote.

“ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba Bwana atakujengea nyumba: Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake. 17:12 1Fal 5:5; 2Nya 7:18; 13:5Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. 17:13 2Kor 6:18; 2Sam 7:14-15; Ebr 1:5; Lk 1:32; 1Nya 28:6; 22:10Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 17:14 1Fal 2:12; 2Nya 9:8; Za 132:11; Yer 33:17; Za 2:6; 89:36; Isa 9:7; Eze 37:25; Dan 2:44; 7:14-27; Mt 21:1-11; Lk 1:33; Ebr 1:8Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ”

Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

Maombi Ya Daudi

(2 Samweli 7:18-29)

17:16 2Sam 7:18; 2Fal 19:14; Ay 7:14-17; Mwa 32:10; Za 144:3Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:

“Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee Bwana Mungu.

17:18 Za 139:1; Yn 21:17“Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako, 17:19 2Sam 7:16-17, 25; 2Fal 20:6; Mt 11:26; Efe 1:11Ee Bwana Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana.

17:20 Kut 8:10; Kum 3:24; Isa 44:6; Kut 15:11; Kum 33:26; 1Sam 2:2; 2Sam 7:22; Za 86:8“Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe. 17:21 Kut 6:6Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 17:22 Kut 19:5-6Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana Mungu, umekuwa Mungu wao.

17:23 1Fal 8:25“Sasa basi, Bwana ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi, 17:24 2Nya 6:33; Yn 12:28; Za 21:13; 72:19; Mt 6:9, 13ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.

“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya. 17:26 Kut 34:6; Ebr 6:18Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 17:27 Za 16:11; 21:6; Rum 11:29; Mwa 27:33; Za 72:17Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, Ee Bwana, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.”

Read More of 1 Nyakati 17

1 Nyakati 18:1-17

Ushindi Wa Daudi

(2 Samweli 8:1-18)

Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Gathi pamoja na vijiji vinavyouzunguka kutoka utawala wa Wafilisti.

18:2 Hes 24:17; 21:29Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.

18:3 1Nya 19:6; Mwa 2:14; 15:18; Kum 11:24; 2Sam 8:3Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alikwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati. 18:4 Mwa 49:6; 2Sam 8:4Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.

18:5 2Fal 16:9; 1Nya 19:6Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. 18:6 1Nya 17:8; Mit 21:31; Za 91:14; 121:8Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru. Bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.

Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu. 18:8 1Fal 7:23; 2Nya 4:12-16Kutoka miji ya Tibhathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.

Tou mfalme wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri mfalme wa Soba, 18:10 2Sam 8:10akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Mfalme Hadadezeri, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu, fedha na shaba.

18:11 Hes 24:18-20Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki.

18:12 1Fal 11:15; 2Sam 7:13; 2Fal 14:7; 2Nya 25:11Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi. 18:13 Mwa 27:29; Hes 24:18; 1Sam 10:3; 13:3; 14:1Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. Bwana akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.

Maafisa Wa Daudi

18:14 1Nya 29:26; 11:1-6Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote. 18:15 2Sam 5:6-8Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu; 18:16 2Sam 8:17; 1Nya 6:8; 24; 6Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Shausha alikuwa mwandishi; 18:17 1Sam 30:14; 2Sam 8:18naye Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa maafisa wakuu katika utumishi wa mfalme.

Read More of 1 Nyakati 18