1 Nyakati 12:23-40, 1 Nyakati 13:1-14, 1 Nyakati 14:1-17 NEN

1 Nyakati 12:23-40

Wengine Waungana Na Daudi Huko Hebroni

12:23 2Sam 2:3-4; 1Nya 10:14; 1Sam 16:1; 1Nya 11:10Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama Bwana alivyokuwa amesema:

watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita.

Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100.

Watu wa Lawi walikuwa 4,600, pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700, 12:28 2Sam 8:17; 1Nya 27:17; 1Fal 1:8; 2:25; 1Nya 6:8; Eze 44:15na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake.

12:29 2Sam 3:19; 2:8-9Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo.

Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao.

Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000.

12:32 Es 1:13Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.

Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000.

Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki.

Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita.

Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita.

Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000.

12:38 2Sam 5:1-3Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme. 12:39 2Sam 3:20; Isa 25:6-8Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao. 12:40 2Sam 16:1; 17:29; 1Sam 25:18; 1Nya 29:22Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.

Read More of 1 Nyakati 12

1 Nyakati 13:1-14

Kurudishwa Kwa Sanduku La Mungu

(2 Samweli 6:1-11)

13:1 1Nya 12:14; Za 132:1; Mit 15:22Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia. 13:2 1Nya 10:7; Isa 37:4Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya Bwana Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi. 13:3 1Sam 7:1-2; 2Nya 1:5; 1Sam 23:2-4Sisi na tulirudishe Sanduku la Mungu wetu kwetu kwa maana hatukujali wakati wa utawala wa Sauli.” Kusanyiko lote likakubaliana kufanya hivyo, kwa sababu ilionekana vyema kwa watu wote.

13:5 1Nya 11:1; 15:3; Yos 13:3; Hes 13:21; 1Sam 6:21; 7:2Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu. 13:6 Yos 15:9; 2Sam 6:2; Kut 25:22; 2Fal 19:15; 1Sam 4:4Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu Bwana, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko.

13:7 Hes 4:15; 1Sam 7:1Wakalisafirisha Sanduku la Mungu kwa gari jipya la kukokotwa na maksai kutoka nyumba ya Abinadabu, Uza na Ahio wakiliongoza gari hilo. 13:8 2Sam 6:5; Za 92:3Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.

13:9 2Sam 6:6Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Kidoni, Uza akaunyoosha mkono wake ili kulizuia Sanduku, kwa sababu maksai walijikwaa. 13:10 1Nya 15:13, 15; Law 10:2; Hes 4:15Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.

13:11 1Nya 15:13; Za 7:11Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, mahali pale pakaitwa Peres-Uza13:11 Maana yake ni Gadhabu dhidi ya Uza. hadi leo.

Siku ile Daudi akamwogopa Mungu naye akauliza. “Nitawezaje kulichukua Sanduku la Mungu kwangu?” 13:13 1Nya 15:18, 24; 16:38; 26:4-5, 15Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani kwa Obed-Edomu, Mgiti. 13:14 2Sam 6:11; 1Nya 26:4-5; Mwa 30:27; 39:5; 1Nya 26:5; Za 37:22; Mit 3:9; 10:22; Mal 3:10Sanduku la Mungu likabaki pamoja na jamaa ya Obed-Edomu, nyumbani kwake kwa miezi mitatu, naye Bwana akaibariki nyumba yake pamoja na kila kitu alichokuwa nacho.

Read More of 1 Nyakati 13

1 Nyakati 14:1-17

Nyumba Ya Daudi Na Jamaa Yake

(2 Samweli 5:11-16)

14:1 1Fal 5:6; Hag 1:8; 2Sam 5:11Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme. 14:2 Hes 24:7; Kum 26:19Naye Daudi akatambua kwamba Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.

14:3 1Nya 3:1; Kum 17:14-17Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi. 14:4 2Sam 5:14; 1Nya 3:5Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, Ibihari, Elishua, Elpeleti, Noga, Nefegi, Yafia, Elishama, Beeliada na Elifeleti.

Daudi Awashinda Wafilisti

(2 Samweli 5:17-25)

14:8 1Nya 11:1; 2Sam 5:17; Za 2:1-5Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao. 14:9 Yos 15:8; 1Nya 11:15Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai, Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”

14:11 Za 94:16; Isa 28:21Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu,14:11 Maana yake ni Bwana Afurikae. akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 14:12 Kut 32:20; Yos 7:15Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.

14:13 2Sam 5:22Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 14:14 Yos 8:6-7; 2Sam 5:23hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.” 14:16 Yos 9:3; 10:33; 2Sam 5:25Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.

14:17 Yos 6:27; 2Nya 26:8; Kum 2:25; Za 2:1-12Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.

Read More of 1 Nyakati 14