1 Nyakati 11:1-47, 1 Nyakati 12:1-22 NEN

1 Nyakati 11:1-47

Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Israeli

(2 Samweli 5:1-10)

11:1 1Nya 9:1; Mwa 13:18; 23:19; 2Sam 5:1; 1Nya 12:23Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako. 11:2 1Sam 18:5, 16; Za 78:71; Mt 2:6; 1Nya 5:2Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Bwana Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

11:3 1Sam 16:1-13; 2Sam 5:3; Rum 8:31Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na Bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli.

Daudi Ateka Yerusalemu

11:4 Yos 3:10; Amu 1:21; 2Sam 5:6; Mwa 10:16; 15:21; Kut 3:17; Amu 19:10Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

11:6 2Sam 2:13; 8:16Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

11:7 2Sam 5:7Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi. 11:8 2Sam 5:9; 2Nya 32:5Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu. 11:9 2Sam 3:1; Es 9:4Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

Mashujaa Wa Daudi

(2 Samweli 23:8-39)

11:10 1Nya 11:1; 12:23; 2Sam 23:8; 1Sam 16:1, 12Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi. 11:11 2Sam 17:10Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi:

Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.

Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. 11:13 1Sam 17:1Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti. 11:14 Kut 14:30; 1Sam 17:10; Mit 21:31Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

11:15 1Nya 14:9Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 11:16 2Sam 5:17Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!” 11:18 Kum 12:16Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa.

Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

11:20 1Sam 26:6Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. 11:21 2Sam 23:24; 1Nya 27:7Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

11:22 Yos 15:21; 1Sam 17:36; 2Sam 1:23; 23:20; 1Nya 12:8Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 11:23 1Sam 26:6Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano.11:23 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao. Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

11:26 1Nya 2:18; 2Sam 23:24; 1Nya 27:7Wale watu mashujaa walikuwa:

Asaheli nduguye Yoabu,

Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,

11:27 1Nya 27:8Shamothi Mharori,

Helesi Mpeloni,

11:28 1Nya 27:12Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa,

Abiezeri kutoka Anathothi,

11:29 2Sam 21:18Sibekai Mhushathi,

Ilai Mwahohi,

Maharai Mnetofathi,

Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,

11:31 1Nya 27:14; Amu 12:13Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini,

Benaya Mpirathoni,

Hurai kutoka mabonde ya Gaashi,

Abieli Mwaribathi,

Azmawethi Mbaharumi,

Eliaba Mshaalboni,

wana wa Hashemu Mgiloni,

Yonathani mwana wa Shagee Mharari,

Ahiamu mwana wa Sakari Mharari,

Elifale mwana wa Uru,

Heferi Mmekerathi,

Ahiya Mpeloni,

Hezro Mkarmeli,

Naarai mwana wa Ezbai,

Yoeli nduguye Nathani,

Mibhari mwana wa Hagri,

Seleki Mwamoni,

Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,

11:40 Yos 15:48; 1Nya 2:50-53Ira Mwithiri,

Garebu Mwithiri,

11:41 2Sam 11:6; 1Nya 2:36Uria Mhiti,

Zabadi mwana wa Alai,

Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini,

Hanani mwana wa Maaka,

Yoshafati Mmithni,

11:44 Kum 1:4Uzia Mwashterathi,

Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri,

Yediaeli mwana wa Shimri,

nduguye Yoha Mtizi,

Elieli Mmahawi,

Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu,

Ithma Mmoabu,

Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai.

Read More of 1 Nyakati 11

1 Nyakati 12:1-22

Mashujaa Waungana Na Daudi

12:1 Yos 15:31; 1Sam 27:2-6Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani, 12:2 Amu 3:15; 20:16; 2Sam 3:19walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):

12:3 Yos 21:18; 1Nya 11:28Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi, 12:4 Yos 15:36; 10:2; 18:21, 25; 1Fal 9:2; Isa 28:21na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi, Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi; Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora; 12:7 Yos 15:58Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.

12:8 Mwa 30:11; 2Sam 2:18; 17:10; 23:14, 29; 23:20; 1Nya 2:17; Mit 28:1Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.

Ezeri alikuwa mkuu wao,

Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu,

Mishmana wa nne, Yeremia wa tano,

Atai wa sita, Elieli wa saba,

Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa,

Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja.

12:14 Law 26:8; Kum 32:30Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000. 12:15 Yos 3:15; Yer 12:5; 49:19Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.

12:16 2Sam 3:19Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake. 12:17 Zek 3:2; Yud 9Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.”

12:18 Amu 6:34; 2Nya 15:1; 2Sam 17:25; 1Sam 25:5-6; 1Nya 2:17Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema:

“Sisi tu watu wako, ee Daudi!

Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese!

Ushindi, naam, ushindi uwe kwako,

pia ushindi kwa wale walio upande wako,

kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.”

Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi.

12:19 1Sam 29:2-4Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”) 12:20 1Sam 27:6Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase. Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake. Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

Read More of 1 Nyakati 12