Zaburi 139 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Zaburi 139:1-24

Zaburi 139

Mungu Asiyeweza Kukwepwa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1139:1 Za 17:3; 44:21; Rum 8:27Ee Bwana, umenichunguza

na kunijua.

2139:2 2Fal 19:27; Za 94:11; Mit 24:12; Yer 12:3Unajua ninapoketi na ninapoinuka;

unatambua mawazo yangu tokea mbali.

3139:3 2Fal 19:27; Ay 31:4Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;

unaelewa njia zangu zote.

4139:4 Ebr 4:13Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,

wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.

5139:5 1Sam 25:16; Za 32:10; 34:7; 125:2Umenizunguka nyuma na mbele;

umeweka mkono wako juu yangu.

6139:6 Za 131:1; Rum 11:33Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu,

ni ya juu sana kwangu kuyafikia.

7139:7 Yer 23:24Niende wapi nijiepushe na Roho yako?

Niende wapi niukimbie uso wako?

8139:8 Kum 30:12-15; Amo 9:2-3; Ay 17:13Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;

nikifanya vilindi139:8 Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania. kuwa kitanda changu,

wewe uko huko.

9Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko,

kama nikikaa pande za mbali za bahari,

10139:10 Za 23:3; 108:6; Isa 41:10hata huko mkono wako utaniongoza,

mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.

11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha

na nuru inayonizunguka iwe usiku,”

12139:12 Ay 34:22; Dan 2:22hata giza halitakuwa giza kwako,

usiku utangʼaa kama mchana,

kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.

13139:13 Za 119:73; Ay 10:11; Isa 44:2, 24; 46:3; 49:5; Yer 1:5Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

14Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

15139:15 Mhu 11:5; Ay 10:11; Za 63:9Umbile langu halikufichika kwako,

nilipoumbwa mahali pa siri.

Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

16139:16 Ay 33:29; Za 90:12macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

Siku zangu zote ulizonipangia

ziliandikwa katika kitabu chako

kabla haijakuwepo hata moja.

17139:17 Za 92:5; Ay 5:9Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu!

Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

18139:18 Za 40:5; 3:5; Ay 29:18Kama ningezihesabu,

zingekuwa nyingi kuliko mchanga.

Niamkapo,

bado niko pamoja nawe.

19139:19 Za 5:6; 6:8; 59:2; Isa 11:4Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu!

Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

20139:20 Za 65:7; Kum 5:11; Ay 21:14-15; Yud 15Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya,

adui zako wanatumia vibaya jina lako.

21139:21 2Nya 19:2; Za 31:6; 26:5; 119:113Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia?

Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?

22139:22 Mt 5:43Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao,

ninawahesabu ni adui zangu.

23139:23 Ay 31:6; 1Sam 16:7; 1Nya 29:17; Za 7:9; Mit 17:3; Yer 11:20; Ufu 2:23Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu,

nijaribu na ujue mawazo yangu.

24139:24 Yer 25:5; 36:3; Za 5:8; 23:2; 143:10Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu,

uniongoze katika njia ya milele.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

诗篇 139:1-24

第 139 篇

上帝的全知和佑护

大卫的诗,交给乐长。

1耶和华啊,你洞察我的内心,

知道我的一切。

2我或坐下或起来,你都知道,

你从远处就知道我的心思意念。

3我或外出或躺卧,你都了解,

你熟悉我的一切行为。

4耶和华啊,我话未出口,

你已洞悉一切。

5你在我前后护卫着我,

以大能的手保护我。

6这一切实在是太奇妙,

太深奥了,我无法明白。

7我去哪里可躲开你的灵?

我跑到哪里可避开你的面?

8我若升到天上,你在那里;

我若下到阴间,你也在那里。

9纵使我乘着晨风飞到遥远的海岸居住,

10就是在那里,

你的手必引导我,

你大能的手必扶持我。

11我想,黑暗一定可以遮蔽我,

让我四围变成黑夜。

12然而,即使黑暗也无法遮住你的视线。

在你看来,黑夜亮如白昼,

黑暗与光明无异。

13你创造了我,

使我在母腹中成形。

14我称谢你,

因为你创造我的作为是多么奇妙可畏,

我心深深知道。

15我在隐秘处被造、在母腹中成形的时候,

你对我的形体一清二楚。

16我的身体还未成形,

你早已看见了。

你为我一生所定的年日,

我还没有出生就已经记在你的册子上了。

17耶和华啊,

你的意念对我来说是何等宝贵,何等浩博!

18我若数算,它们比海沙还多。

我醒来的时候,

依然与你在一起。

19耶和华啊,愿你杀戮恶人!

嗜血成性的人啊,你们走开!

20他们恶言顶撞你,

你的仇敌亵渎你的名。

21耶和华啊,

我憎恨那些憎恨你的人,

我厌恶那些攻击你的人。

22我恨透了他们,

我视他们为敌人。

23上帝啊,求你鉴察我,

好知道我的内心;

求你试验我,好知道我的心思。

24求你看看我里面是否有邪恶,

引导我走永恒的道路。