出埃及記 36 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

出埃及記 36:1-38

1摩西說:「比撒列亞何利亞伯以及所有蒙耶和華賜智慧聰明、有技能、懂得如何建造聖所的人,都要按照耶和華的吩咐去做。」

2於是,摩西召來比撒列亞何利亞伯和所有蒙耶和華賜智慧、有技能、願意參與建造的人。 3他們從摩西那裡領取了以色列百姓奉獻出來建造聖所的一切禮物。每天早上,百姓仍然甘心樂意地來奉獻禮物, 4以致所有建造聖所的能工巧匠都放下自己的工作, 5前來對摩西說:「百姓的奉獻太多了,我們建造耶和華吩咐的聖所用不了。」

6於是,摩西傳令全營:「大家不用再為聖所奉獻禮物了。」百姓這才停止奉獻。 7因為所獻的材料已經足夠建造聖所,而且綽綽有餘。

8工人中的能工巧匠用十幅幔子做成了聖幕,幔子用細麻線和藍色、紫色、朱紅色的線織成,上面精工繡製了基路伯天使。 9每幅幔子的尺寸都一樣,長十二米、寬兩米。 10又把每五幅幔子連在一起,共連成兩幅大幔子。 11然後在每幅大幔子邊緣釘上了藍色的扣環, 12每幅各釘上五十個扣環,都是兩兩相對。 13又做了五十個金鉤,把兩幅大幔子連在一起,成為聖幕。

14比撒列用山羊毛織成十一幅幔子,做聖幕的罩棚, 15每幅幔子的尺寸都一樣,長十三米、寬兩米。 16然後把五幅連成一大幅,餘下的六幅又連成一大幅。 17又在這兩幅大幔子邊緣各釘上五十個對稱的扣環, 18再用五十個銅鉤,把兩幅大幔子連在一起,成為一個罩棚, 19並在罩棚上面蓋一層染成紅色的公羊皮,再蓋一層海狗皮做頂蓋。

20他用皂莢木做支撐聖幕的木板, 21每塊木板長四米,寬六十六釐米, 22上面都有兩個接榫,用來把木板連接在一起。聖幕的所有木板都這樣做。 23聖幕的南面共有二十塊木板, 24在這些木板下面又造了四十個帶凹槽的銀底座,每塊木板下面有兩個,套在木板的兩個接榫上。 25聖幕北面也有二十塊木板, 26木板下面同樣有四十個帶凹槽的銀底座,每塊木板下面有兩個銀底座。 27聖幕的後面,就是西面,有六塊木板, 28聖幕的兩個拐角各有兩塊木板, 29木板的下端連於底座,頂端用一個環固定。兩個拐角都要這樣做。 30這樣後面共有八塊木板,每塊木板下面各有兩個銀底座,一共是十六個銀底座。

31-32他用皂莢木做橫閂,聖幕左右兩邊和後面的牆板上各有五根橫閂, 33攔腰固定牆板的那根橫閂從這端貫穿到那端。 34所有的木板和橫閂都包上金,並在木板上造金環,用來穿橫閂。

35他用細麻線和藍色、紫色、朱紅色的線織成一幅幔子,精工繡上基路伯天使, 36把這幅幔子掛在四根用皂莢木造的柱子上,柱子外面包上金,加上金鉤,四根柱子下面有四個銀底座。 37他又用細麻線和藍色、紫色、朱紅色的線繡製聖幕的門簾, 38用皂莢木做五根掛門簾的柱子,上面有金鉤,柱頂和橫杆包上金。柱子的五個底座是銅造的。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 36:1-38

136:1 Kut 28:3; 25:8; Ay 32:8; Isa 28:26; Mit 2:6; Kut 25:8; Law 4:6; 19:30; Hes 18:5; 30:8; 1Fal 6:16; Za 96:6; 134:2; Isa 63:18; Eze 5:11; Dan 8:13, 14; Ebr 9:1, 2Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu Bwana aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile Bwana alivyoagiza.”

236:2 Kut 31:2, 6; 25:2; 35:2, 26; 1Nya 29:5Ndipo Mose akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Bwana alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi. 336:3 Kut 35:29Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi. 4Ikafika wakati mafundi wote wenye ujuzi waliokuwa wakiifanya kazi yote ya mahali patakatifu wakasimamisha kazi zao, 536:5 2Nya 24:14; 31:10; 2Kor 8:2-3wakaja na kumwambia Mose, “Watu wanaleta vitu vingi kuliko tunavyohitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo Bwana ameagiza ifanyike.”

6Ndipo Mose akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi yote: “Mtu yeyote mwanaume au mwanamke asilete tena kitu chochote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu wakazuiliwa kuleta zaidi, 736:7 1Fal 7:47kwa sababu walivyokuwa navyo tayari vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote.

Maskani Ya Mungu

(Kutoka 26:1-37)

836:8 Kut 26:1; Ay 32:8; Mit 10:8; 15:14; 21:1; Mwa 3:24; 1Fal 6:23; 2Nya 3:10; Eze 1:5-28; 10:1Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. 9Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,36:9 Dhiraa 28 ni sawa na mita 12.6. na upana wa dhiraa nne36:9 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. 10Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. 11Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. 1236:12 Kut 26:5Wakatengeneza pia vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vikaelekeana. 13Kisha wakatengeneza vifungo hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha zile fungu mbili za mapazia pamoja ili maskani ipate kuwa kitu kimoja.

1436:14 Kut 26:7Wakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. 15Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,36:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. na upana wa dhiraa nne. 16Wakaunganisha mapazia matano kuwa fungu moja, na hayo mengine sita kuwa fungu lingine. 17Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. 18Wakatengeneza vifungo hamsini vya shaba ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. 1936:19 Kut 26:14Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.36:19 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.

2036:20 Kut 26:15; 25:5, 10; Hes 25:1; Kum 10:3; Yos 2:1Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 21Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,36:21 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. na upana wa dhiraa moja na nusu,36:21 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5. 22zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 23Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 24na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 25Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini 26na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. 27Wakatengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, 28na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za maskani za upande uliokuwa mbali. 2936:29 Kut 26:24; Za 133:1; Mdo 2:46; 1Kor 1:10Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana. 30Kwa hiyo kulikuwa na mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

3136:31 Kut 26:26Wakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, 32matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. 33Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. 34Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika hayo mataruma kwa dhahabu.

3536:35 Kut 39:38; Mt 27:51; Lk 23:45; Ebr 9:5; 6:19; 10:20Wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye hilo pazia. 36Wakatengeneza nguzo nne za mti wa mshita kwa ajili yake na kuzifunika kwa dhahabu. Wakatengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya nguzo hizo, na kusubu vitako vinne vya fedha. 3736:37 Kut 27:16; Law 16:2Kwa ajili ya ingilio la hema wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. 3836:38 1Fal 7:16; 2Nya 4:12; Yer 52:22Pia wakatengeneza nguzo tano zenye kulabu. Wakafunika ncha za juu za hizo nguzo pamoja na tepe zake kwa dhahabu, na pia wakatengeneza vitako vyake vitano vya shaba.