利未記 1 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

利未記 1:1-17

獻燔祭的條例

1耶和華在會幕裡呼喚摩西,對他說: 2「你把以下條例告訴以色列人。

「如果你們有人獻祭給耶和華,要用牛羊作祭物。 3如果用牛作燔祭,必須用毫無殘疾的公牛,在會幕門口獻上,便可蒙耶和華悅納。 4獻祭者要把手放在牛頭上,所獻的燔祭便蒙悅納,為他贖罪。 5他要在耶和華面前宰牛,然後祭司——亞倫的子孫要把牛血灑在會幕門口的祭壇四周。 6獻祭者要剝掉牛皮,把牛切成塊。 7祭司——亞倫的子孫要在祭壇上生火,把木柴擺在火上, 8然後將肉塊、頭顱和脂肪都擺在祭壇燃燒的木柴上。 9獻祭者要用水洗淨牛的內臟和腿。祭司要把這一切都放在壇上焚燒。這是燔祭,是蒙耶和華悅納的馨香火祭。

10「如果用綿羊或山羊作燔祭,必須用毫無殘疾的公羊。 11獻祭者要在祭壇北面,在耶和華面前宰羊。祭司——亞倫的子孫要把羊血灑在祭壇四周。 12獻祭者將羊切成塊後,祭司要把肉塊、頭顱和脂肪擺在祭壇燃燒的木柴上。 13獻祭者要用水洗淨羊的內臟和腿。祭司要把這一切都放在壇上焚燒。這是燔祭,是蒙耶和華悅納的馨香火祭。

14「如果有人用鳥作燔祭,要用斑鳩或雛鴿。 15祭司要把鳥帶到祭壇前,擰下鳥頭,放在祭壇上焚燒;要在祭壇旁放盡鳥血; 16要除掉鳥的嗉子和羽毛,丟在祭壇東邊倒灰的地方。 17祭司要抓著兩個翅膀把鳥撕開,但不可撕斷,然後把鳥放在壇上焚燒。這是燔祭,是蒙耶和華悅納的馨香火祭。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 1:1-17

Sadaka Ya Kuteketezwa

11:1 Kut 3:4; 19:3; 25:22; 40:2; Hes 7:89; 12:4-5Bwana akamwita Mose na kusema naye kutoka kwenye Hema la Kukutania, akamwambia, 21:2 Law 22:18-21; 7:16, 38; 23:38; 27:9; Hes 15:3“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa Bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe au la kondoo na mbuzi.

31:3 Kum 15:21; 12:5-6, 11; Mwa 8:20; Law 6:25; 17:9; 22:19-20, 27; Ezr 8:35; Mal 1:8; Kut 12:5; Ebr 9:14; 1Pet 1:19; Hes 6:16; Isa 58:5“ ‘Kama sadaka hiyo ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la ngʼombe, atamtoa ngʼombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa Bwana. 41:4 Kut 29:10, 15, 36; Law 4:29; 6:25; Eze 45:15; Mwa 32:20, 30; 2Nya 29:23-24; Kut 29:26; 32:30; Isa 56:7; Rum 12:1; Hes 15:25; Flp 4:18; Ebr 10:11Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. 51:5 Kut 29:11, 20; Law 3:2, 8; 8:2; 10:6; 21:1; Hes 15:8; Kum 13:8; Za 50:9; 69:31; Ebr 12:24; 1Pet 1:2Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Bwana, kisha wana wa Aroni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania. 61:6 Law 7:8; Kut 29:17Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande. 71:7 Mwa 22:9; Law 3:5; 6:12Wana wa Aroni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto. 81:8 Kut 29:13; Law 8:20; 9:13Kisha wana wa Aroni walio makuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. 91:9 Kut 29:17, 18; Law 2:2; 3:5; 17:6; 6:22; 9:14; 23:8, 25, 36; Hes 28:6, 19; 18:17; 28:11-13; Mwa 8:21; Efe 2:5Ataziosha sehemu za ndani na miguu yake kwa maji, naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

101:10 Mwa 22:7; Kut 12:5; Law 3:12; 4:23, 28; 5:6; Hes 15:11“ ‘Kama sadaka ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la kondoo au mbuzi, atamtoa mnyama dume asiye na dosari. 111:11 Kut 29:11, 20Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za Bwana, nao wana wa Aroni walio makuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu. 12Atamkata vipande vipande, naye kuhani atavipanga, pamoja na kichwa na mafuta ya mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. 131:13 Kut 29:17; Law 6:22; Kum 12:27Ataosha sehemu za ndani na miguu kwa maji, naye kuhani atavileta vyote na kuvichoma juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

141:14 Mwa 15:9; Lk 2:24; Law 5:7; Lk 2:24“ ‘Kama sadaka ya kuteketezwa inayotolewa kwa Bwana ni ndege, atamtoa hua au kinda la njiwa. 151:15 Law 5:8-9Kuhani atamleta kwenye madhabahu, naye atamvunja shingo na kumnyofoa kichwa na kumchoma juu ya madhabahu. Damu yake itachuruzishwa ubavuni mwa madhabahu. 161:16 Law 4:12; 6:10; Hes 4:13Ataondoa kifuko cha chakula pamoja na uchafu wake na kuvitupa upande wa mashariki wa madhabahu, mahali pale penye majivu. 171:17 Mwa 15:10; Law 5:8Atampasua na kumweka wazi katika mabawa yake, lakini asimwachanishe kabisa, kisha kuhani ataichoma juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.