Jeremiah 28 – NIV & NEN

New International Version

Jeremiah 28:1-17

The False Prophet Hananiah

1In the fifth month of that same year, the fourth year, early in the reign of Zedekiah king of Judah, the prophet Hananiah son of Azzur, who was from Gibeon, said to me in the house of the Lord in the presence of the priests and all the people: 2“This is what the Lord Almighty, the God of Israel, says: ‘I will break the yoke of the king of Babylon. 3Within two years I will bring back to this place all the articles of the Lord’s house that Nebuchadnezzar king of Babylon removed from here and took to Babylon. 4I will also bring back to this place Jehoiachin28:4 Hebrew Jeconiah, a variant of Jehoiachin son of Jehoiakim king of Judah and all the other exiles from Judah who went to Babylon,’ declares the Lord, ‘for I will break the yoke of the king of Babylon.’ ”

5Then the prophet Jeremiah replied to the prophet Hananiah before the priests and all the people who were standing in the house of the Lord. 6He said, “Amen! May the Lord do so! May the Lord fulfill the words you have prophesied by bringing the articles of the Lord’s house and all the exiles back to this place from Babylon. 7Nevertheless, listen to what I have to say in your hearing and in the hearing of all the people: 8From early times the prophets who preceded you and me have prophesied war, disaster and plague against many countries and great kingdoms. 9But the prophet who prophesies peace will be recognized as one truly sent by the Lord only if his prediction comes true.”

10Then the prophet Hananiah took the yoke off the neck of the prophet Jeremiah and broke it, 11and he said before all the people, “This is what the Lord says: ‘In the same way I will break the yoke of Nebuchadnezzar king of Babylon off the neck of all the nations within two years.’ ” At this, the prophet Jeremiah went on his way.

12After the prophet Hananiah had broken the yoke off the neck of the prophet Jeremiah, the word of the Lord came to Jeremiah: 13“Go and tell Hananiah, ‘This is what the Lord says: You have broken a wooden yoke, but in its place you will get a yoke of iron. 14This is what the Lord Almighty, the God of Israel, says: I will put an iron yoke on the necks of all these nations to make them serve Nebuchadnezzar king of Babylon, and they will serve him. I will even give him control over the wild animals.’ ”

15Then the prophet Jeremiah said to Hananiah the prophet, “Listen, Hananiah! The Lord has not sent you, yet you have persuaded this nation to trust in lies. 16Therefore this is what the Lord says: ‘I am about to remove you from the face of the earth. This very year you are going to die, because you have preached rebellion against the Lord.’ ”

17In the seventh month of that same year, Hananiah the prophet died.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 28:1-17

Hanania Nabii Wa Uongo

128:1 Yer 27:1-3; Yos 9:3; 2Nya 36:11Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Bwana mbele ya makuhani na watu wote: 228:2 Yer 27:12“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli. 328:3 2Fal 24:13; Yer 27:16-22Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli. 428:4 Yer 22:24-27; 2Fal 25:30; Hos 7:3Pia nitamrudisha mahali hapa Yekonia28:4 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini. mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walikwenda Babeli,’ asema Bwana, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’ ”

5Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba ya Bwana. 628:6 1Nya 16:36; Za 72:19; 1Kor 14:16; Ufu 1:18; Zek 6:10Akasema, “Amen! Bwana na afanye hivyo! Bwana na ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya Bwana pamoja na wote waliohamishwa. 7Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote: 828:8 Isa 5:5-7; Nah 1:14Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa. 928:9 Kum 18:22; Eze 33:33; Isa 8:20Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa na Bwana ikiwa unabii wake utatimia.”

1028:10 Law 26:13; Yer 27:2; Za 10:13; 1Fal 22:11Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja, 1128:11 Yer 14:14; 27:10; Mit 26:4naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake.

12Kitambo kidogo baada ya nabii Hanania kuivunja nira kutoka shingo ya nabii Yeremia, neno la Bwana likamjia Yeremia: 13“Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma. 1428:14 Kum 28:48; Yer 15:12; 25:11; 27:4-7; Dan 8:15; Yer 39:1Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’ ”

1528:15 Yer 29:31; Mao 2:14; Eze 13:6; Yer 7:4; 20:6; 29:21Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania! Bwana hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo. 1628:16 Mwa 7:4; Kum 13:5; Yer 29:32; Kum 18:20; Zek 13:3Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Bwana.’ ”

1728:17 1Sam 2:9; Ay 21:30; Rum 2:2-3; 2Fal 1:17Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.