Isaiah 1 – NIV & NEN

New International Version

Isaiah 1:1-31

1The vision concerning Judah and Jerusalem that Isaiah son of Amoz saw during the reigns of Uzziah, Jotham, Ahaz and Hezekiah, kings of Judah.

A Rebellious Nation

2Hear me, you heavens! Listen, earth!

For the Lord has spoken:

“I reared children and brought them up,

but they have rebelled against me.

3The ox knows its master,

the donkey its owner’s manger,

but Israel does not know,

my people do not understand.”

4Woe to the sinful nation,

a people whose guilt is great,

a brood of evildoers,

children given to corruption!

They have forsaken the Lord;

they have spurned the Holy One of Israel

and turned their backs on him.

5Why should you be beaten anymore?

Why do you persist in rebellion?

Your whole head is injured,

your whole heart afflicted.

6From the sole of your foot to the top of your head

there is no soundness—

only wounds and welts

and open sores,

not cleansed or bandaged

or soothed with olive oil.

7Your country is desolate,

your cities burned with fire;

your fields are being stripped by foreigners

right before you,

laid waste as when overthrown by strangers.

8Daughter Zion is left

like a shelter in a vineyard,

like a hut in a cucumber field,

like a city under siege.

9Unless the Lord Almighty

had left us some survivors,

we would have become like Sodom,

we would have been like Gomorrah.

10Hear the word of the Lord,

you rulers of Sodom;

listen to the instruction of our God,

you people of Gomorrah!

11“The multitude of your sacrifices—

what are they to me?” says the Lord.

“I have more than enough of burnt offerings,

of rams and the fat of fattened animals;

I have no pleasure

in the blood of bulls and lambs and goats.

12When you come to appear before me,

who has asked this of you,

this trampling of my courts?

13Stop bringing meaningless offerings!

Your incense is detestable to me.

New Moons, Sabbaths and convocations—

I cannot bear your worthless assemblies.

14Your New Moon feasts and your appointed festivals

I hate with all my being.

They have become a burden to me;

I am weary of bearing them.

15When you spread out your hands in prayer,

I hide my eyes from you;

even when you offer many prayers,

I am not listening.

Your hands are full of blood!

16Wash and make yourselves clean.

Take your evil deeds out of my sight;

stop doing wrong.

17Learn to do right; seek justice.

Defend the oppressed.1:17 Or justice. / Correct the oppressor

Take up the cause of the fatherless;

plead the case of the widow.

18“Come now, let us settle the matter,”

says the Lord.

“Though your sins are like scarlet,

they shall be as white as snow;

though they are red as crimson,

they shall be like wool.

19If you are willing and obedient,

you will eat the good things of the land;

20but if you resist and rebel,

you will be devoured by the sword.”

For the mouth of the Lord has spoken.

21See how the faithful city

has become a prostitute!

She once was full of justice;

righteousness used to dwell in her—

but now murderers!

22Your silver has become dross,

your choice wine is diluted with water.

23Your rulers are rebels,

partners with thieves;

they all love bribes

and chase after gifts.

They do not defend the cause of the fatherless;

the widow’s case does not come before them.

24Therefore the Lord, the Lord Almighty,

the Mighty One of Israel, declares:

“Ah! I will vent my wrath on my foes

and avenge myself on my enemies.

25I will turn my hand against you;1:25 That is, against Jerusalem

I will thoroughly purge away your dross

and remove all your impurities.

26I will restore your leaders as in days of old,

your rulers as at the beginning.

Afterward you will be called

the City of Righteousness,

the Faithful City.”

27Zion will be delivered with justice,

her penitent ones with righteousness.

28But rebels and sinners will both be broken,

and those who forsake the Lord will perish.

29“You will be ashamed because of the sacred oaks

in which you have delighted;

you will be disgraced because of the gardens

that you have chosen.

30You will be like an oak with fading leaves,

like a garden without water.

31The mighty man will become tinder

and his work a spark;

both will burn together,

with no one to quench the fire.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 1:1-31

11:1 1Sam 3:1; Hes 12:6; 2Fal 14:21; 16:1; 1Nya 3:12-13; 2Nya 26:22; 1Sam 22:1, 5; Oba 1:1; Nah 1:1; Isa 40:9; 44:26Maono kuhusu Yuda na Yerusalemu ambayo Isaya mwana wa Amozi aliyaona wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.

Taifa Asi

21:2 Hag 1:12; Amu 11:10; Kum 4:26; Yer 42:5; Isa 23:4; 63:16; 65:2; Eze 24:3; Mik 1:2; Isa 63:16; Mal 1:6Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia!

Kwa maana Bwana amesema:

“Nimewalisha watoto na kuwalea,

lakini wameniasi mimi.

31:3 Yer 4:22; 9:3-6; Hos 2:8; Ay 12:9; Mwa 42:27; Kum 32:28; Isa 42:25; Ay 12:9; Hos 4:1; Isa 48:8; Hos 4:6; 7:9Ngʼombe anamjua bwana wake,

naye punda anajua hori la mmiliki wake,

lakini Israeli hajui,

watu wangu hawaelewi.”

41:4 Yer 23:14; Eze 39:7; 2Fal 19:22; Isa 1:2; Za 14:3; Kum 32:15; Isa 5:19; 31:1; 5:18; 9:17; 14:20; Za 119:87Lo! Taifa lenye dhambi,

watu waliolemewa na uovu,

uzao wa watenda mabaya,

watoto waliozoelea upotovu!

Wamemwacha Bwana,

Wamemkataa kwa dharau

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli

na kumgeuzia kisogo.

51:5 Yer 2:20; 30:17; 44:16-17; 2:30; 5:3; Ebr 3:16; Isa 31:6; 44:16-17; Mit 20:30; Mao 2:11Kwa nini mzidi kupigwa?

Kwa nini kudumu katika uasi?

Kichwa chako chote kimejeruhiwa,

moyo wako wote ni mgonjwa.

61:6 Kum 28:35; Yer 8:22; 14:19; 30:17; Mao 2:13; Eze 34:4; Lk 10:34; 2Sam 14:2; Za 45:7; 104:15; 38:3; Isa 61:3; 53:5; 30:26Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako

hakuna uzima:

ni majeraha matupu na makovu

na vidonda vitokavyo damu,

havikusafishwa au kufungwa

wala kulainishwa kwa mafuta.

71:7 Kum 28:51; Amu 6:3-6; Isa 62:8; 2Fal 18:13; Law 26:34; 26:16; Yer 5:17; Za 109:11Nchi yenu imekuwa ukiwa,

miji yenu imeteketezwa kwa moto;

nchi yenu imeachwa tupu na wageni

mbele ya macho yenu,

imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni.

81:8 Za 9:14; Isa 10:32; 30:17; 49:21; Ay 27:18Binti Sayuni ameachwa kama kipenu

katika shamba la mizabibu,

kama kibanda katika shamba la matikitimaji,

kama mji uliohusuriwa.

91:9 Rum 9:29; 2Fal 21:14; Mwa 45:7; 19:24; Isa 4:2; 6:13; 27:12; Yer 23:3; Yoe 2:32Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote1:9 Bwana Mwenye Nguvu Zote hapa ni Yehova Sabaoth, yaani Bwana wa Majeshi; pia Warumi 9:29 na Yakobo 5:4.

asingelituachia walionusurika,

tungelikuwa kama Sodoma,

tungelifanana na Gomora.

101:10 Isa 30:9; 28:14; 5:24; 8:20; 13:19; Ufu 11:8; Mwa 13:13; Eze 16:49; Rum 9:29Sikieni neno la Bwana,

ninyi watawala wa Sodoma;

sikilizeni sheria ya Mungu wetu,

enyi watu wa Gomora!

111:11 Amo 6:4; Yer 6:20; Ebr 10:4; Za 50:8; 40:6; Ay 22:3; Isa 66:3; 1Sam 15:22; Mal 1:10Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu,

ni kitu gani kwangu?

Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi,

za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona.

Sipendezwi na damu za mafahali

wala za wana-kondoo na mbuzi.

121:12 Kut 23:17; Kum 31:11Mnapokuja kujihudhurisha mbele zangu,

ni nani aliyewataka ninyi mfanye hivyo,

huku kuzikanyaga nyua zangu?

131:13 Mit 15:8; 1Nya 23:31; Hag 2:14; Yer 18:15; 44:8; 1Fal 11:24; Mit 28:9; Yer 7:9; Isa 41:24; 66:3Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana!

Uvumba wenu ni chukizo kwangu.

Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada:

siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.

141:14 Za 69:3; Kut 12:16; Mal 3:14; Kum 16:1-7; Neh 10:33; Ay 7:12; Hes 28:11-29; Law 23:1-44Sikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi, na sikukuu zenu zilizoamriwa:

moyo wangu unazichukia.

Zimekuwa mzigo kwangu,

nimechoka kuzivumilia.

151:15 Ay 27:9; Kum 31:17; 1:45; Mik 3:4; Hos 4:2; Isa 57:17; 59:2; Kut 9:29; Yoe 3:21; 1Sam 8:18Mnaponyoosha mikono yenu katika maombi,

nitaficha macho yangu nisiwaone;

hata mkiomba maombi mengi

sitasikiliza.

Mikono yenu imejaa damu;

161:16 Yer 4:14; 25:5; Hes 19:11-16; Isa 52:11; Rut 3:3; Yak 4:8; Mt 27:24jiosheni na mkajitakase.

Yaondoeni matendo yenu maovu

mbele zangu!

Acheni kutenda mabaya,

171:17 Mik 6:8; Sef 2:3; Ay 22:9; Isa 33:5; Kut 22:22; Amo 5:14-15; Za 34:14; 72:1; Isa 11:4jifunzeni kutenda mema!

Tafuteni haki,

watieni moyo walioonewa.

Teteeni shauri la yatima,

wateteeni wajane.

181:18 1Sam 2:25; Isa 41:21; 55:7; Ufu 7:14; Za 51:7; Isa 43:9; 41:1; 43:26“Njooni basi tuhojiane,”

asema Bwana.

“Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu,

zitakuwa nyeupe kama theluji;

ingawa ni nyekundu sana kama damu,

zitakuwa nyeupe kama sufu.

191:19 Ezr 9:12; Za 34:10; Ay 36:11; Isa 50:10; 62:9; Kum 30:15-16; Isa 58:14; 65:13; 30:32Kama mkikubali na kutii,

mtakula mema ya nchi,

201:20 Yer 17:27; Hes 23:19; Ay 15:22; 1Sam 12:15; Isa 3:25; 21:17; 34:16; 27:1; 65:12lakini kama mkikataa na kuasi,

mtaangamizwa kwa upanga.”

Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena.

211:21 Isa 57:3-9; Yer 2:20; 3:2-9; 13:27; Eze 23:3; Hos 2:1-13; Amo 6:12; Isa 46:13; 59:14; Mit 6:17Tazama jinsi mji uliokuwa mwaminifu

umekuwa kahaba!

Mwanzoni ulikuwa umejaa unyofu,

haki ilikuwa inakaa ndani yake,

lakini sasa ni wauaji!

221:22 Za 119:119Fedha yenu imekuwa takataka,

divai yenu nzuri imechanganywa na maji.

231:23 Kum 19:14; Amo 5:8; Yer 5:28; Mik 2:1-2; 6:12; Kut 23:8; Isa 10:2; Eze 22:6-7; Isa 1:2; Mik 3:9; Amo 5:12; Hab 1:4Watawala wenu ni waasi,

rafiki wa wevi,

wote wanapenda rushwa

na kukimbilia hongo.

Hawatetei yatima,

shauri la mjane haliletwi mbele yao lisikilizwe.

241:24 Mwa 49:24; Isa 34:2, 8; 47:3; 59:17; 63:4; Yer 51:6; Eze 5:13; Kum 32:43Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi:

“Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu

na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu.

251:25 Yer 9:7; 6:29; Ufu 3:19; Isa 48:10; Kum 28:63; Za 78:38; 2Nya 29:15; Eze 22:22; Za 119:119Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu,

nitawasafisha takataka zenu zote

na kuwaondolea unajisi wenu wote.

261:26 Mik 4:8; Zek 8:3; Yer 31:23; 33:7; Kum 9:24; Mwa 32:28; Isa 32:16; 46:13; 4:3; 48:2Nitawarudishia waamuzi wenu kama ilivyokuwa siku za zamani,

nao washauri wenu kama ilivyokuwa mwanzoni.

Baadaye utaitwa,

Mji wa Haki,

Mji Mwaminifu.”

271:27 Isa 31:6; 59:20; 35:10; 41:14; 62:12; 63:4; 30:15; Hos 2:19; Eze 18:30Sayuni itakombolewa kwa haki,

wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu.

281:28 Yer 4:18; 44:12; 2The 1:8-9; Isa 33:14; 43:27; 48:8; 16:2; Kum 32:18; 32:15; Za 9:5; Yer 16:4Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa,

nao wanaomwacha Bwana wataangamia.

291:29 Eze 6:13; Hos 4:13; Isa 65:3; 42:17; 44:9; 57:5; Za 97:7; Yer 10:14; Za 97:7“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni

ambayo mlifurahia,

mtafadhaika kwa sababu ya bustani

mlizozichagua.

301:30 Za 1:3Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka,

kama bustani isiyokuwa na maji.

311:31 Isa 4:4; 5:24; 9:18-19; 24:6; 33:14; 66:15-16, 24; Yer 5:14; 7:20; Mal 3:2; Mt 25:41Mtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto,

na kazi yake kama cheche ya moto;

vyote vitaungua pamoja,

wala hakuna wa kuuzima huo moto.”